Je, Unaweza Kuwa Jasusi Bila Kujijua? πŸ€”

Nakumbuka kuna ishu ilitokea miaka hiyo ya nyuma tukiwa high school, basi asubuhi moja hivi mida ya Saa nne wakaja wazee Fulani hivi umri umeenda na Kaunda suti zao za grey na nyeusi Huku wameshika vimikoba vyao vile vya ngozi vyeusi.

Basi tukaitwa darasa zima, wale wazee wakaingia darasani, darasa kimyaa!, Mzee mmoja akasimama mbele ya darasa akasema nahitaji watu wanne miongoni mwenu lakini atachagua yeye mwenyewe so darasa likae kimya, Yule Mzee akawa anapita kwenye mistari mdogo mdogo anazunguka Tu darasani, baadae akatulia pale mbele basi akachagua watu wanne, Mimi nilikuwemo kwenye hao watu wanne.

Kipindi kile nilihisi Yule Mzee ni mchawi au ni mtaalamu wa saikolojia au mtaalamu wa tabia za watu maana kwenye hao watu wanne Kulikuwa na balance kwasababu Kati ya hao watu wanne kuna wenye sifa za upole, uongeaji Sana, uhuni (usela mavi wa shule ule), uoga au tuseme unyonge...

Tukatolewa hapo Tukapelekwa chumba Kingine (kama hall Fulani hv but ni dogo), tukapewa viti, karatasi nyeupe na Kalamu, wale wazee wakaja Tukaendelea na zoezi Hadi mwisho, Kipindi hicho walimu wote walijifungia ofisini (Ofisi za walimu)...

Baada ya mwaka mmoja nikaanza kuona effects ya lile zoezi sijui kama wale wenzangu waliona effects ya lile zoezi tulilolifanya but mm niliona pale shuleni kwetu Hadi shule za jirani Na Kwa kiasi mtaani, kuna vitu Fulani Fulani pia vilikuwa vinatokea mtaani Kwa Kipindi hicho, Yaani niseme kuna watu kweli Wana uzalendo Sana but huwa wanazidiwa nguvu na mafisi ndio maana inaonekana kama kazi hazifanyiki but wako watu Wana akili nzuri tu ni hiyo basi tu...

Kama hujijui kuwa wewe ni Jasusi basi ww ni "useful idiot" au tuseme Unwitting asset kama tulivyokuwa Sisi kwenye lile zoezi....
 
Aisee! Unajua kwanini huyo Don alikuogopa Mkuu?

Ni kwa sababu in psychology of power, mtu mwenye nguvu huwa anamuogopa zaidi mtu ambaye haongei sana na yule ambaye hawezi kumnunua kwa urahisi kwa ofa ndogondogo.
 
Wow, thank you love ❀️
Umeeleza vyema sana, umenikata kiu wallah
I love the way your mind works…
Asantee kwa maoni na karibu tena
The Thinker πŸ™πŸ™
 
Shukran sana mkuu umeitendea haki mada hii
Asante na karibu tena kila la kheri katika biashara zako za huku daslamu na huko kimanzichana 🀝
 
Wow, thank you love ❀️
Umeeleza vyema sana, umenikata kiu wallah
I love the way your mind works…
Asantee kwa maoni na karibu tena
The Thinker πŸ™πŸ™
Shukrani sana kwa mada nzuri na ya kufikirisha Mi Amor, nimefurahi kuwa sehemu yake, trust your gut and take care my love. ❀️
 
Ila kazi ilipomalizika !.........🀝
 
Shukran sana mkuu umeitendea haki mada hii
Asante na karibu tena kila la kheri katika biashara zako za huku daslamu na huko kimanzichana 🀝
Shukrani sana mkuu, karibu.

Nipo katika viunga vya NY City leo ni miaka 25 tangu wale magaidi Assets wa Osama Bin Laden wafanye yao pale kwenye zile Twin Towers.
 
Asante kwa kisa chako mkuu
Karibu tena
 
Ndiyo hivyo shoga angu Kwan bwana wake wa maana basi ni vile tuu tumemsifia,

Beste nikuambie yule sio rafiki ni sumu sikia alichoniambia

Maimuna kwenye shughuli yangu nahitaji tunzo langu na undugu ufe unafik sitaki

Dada mwenye kope nchi kumi na mbili..... Unafiki hatutaki eeeh
 
Heh vipi tena πŸ˜…πŸ˜…
 
Mwaka fulan tumemaliza Chuo kikuu jamaa akaniambia Njoo mwananyamala sehemu fulan kuna kazi ntakupa!

Nikafika bila kuchelewa, nashangaa hanipi kazi yeye ni chupa monde tunapiga story za kawaida tu Tena ambazo ni Kama za maisha !!

Nikaona Kama vile nisimuulize Kazi nikakaa kimya Maana Kama amelewa Fulani hivi

Baada ya miezi Kama 6 naona jina langu kwenda kufanya kazi Taasisi fulan ya serikali nikashangaa Mbona sijawai Omba kazi pale ??? Lakin kwakuwa mshahara ni mnono kidogo nikabidi nikubali, na kazi inaendana na nilichosomea,

Sasa siku Moja nikakutana na Yule mzee Tena Yaan nikamwambia mzee Kazi ile ulikuwa umeniahidi ni ipi Maana nahisi kuna Kazi nimepata, Ila kwa kuwa mwonekano wake alionekana mtu wa kawaida sana na Kama Kazi ingekuwapo kweli basi nilidhani isingefika niliyopewa kwenye Taasisi ya Umma! Ikabidi kiubinadamu nimuulize mzee Kazi nimepata tayari akanitajia Akasema ni Taasisi fulan right ? Nikasema Ndiyo Akasema yes ! Nikauliza sasa Mbona sikufanya interview? Akasema siku ile nimekuita pale Manyanya ndo interview yenyewe na wale waliokuwa wamekaa counter wanne ndo walikuwa wana access ! Duh nikashangaa Mbona sasa sikwambiwa maana sikuulizwa hata maswali yanayohusiana na kazi ! Akasema Yaan ndo interview yenyewe hiyo!

Sasa nipo kwenye Taasisi hiyo nashangaa meshimiwa waziri ambaye Baadae alikuja kuwa Rais (R.I.P) Akiwa na mtu ambaye sitamtaja Maana Bado yuko hai wakiwa wamekuja eti kwenye taasisi ile wanataka mtu wa kuwaandikia report fulan ya kuweka gazetini na mi nilikuwa fresh graduate wakasema Huyu kijana anaweza kuwa anajua hata computer! Wakamwambia meneja wangu nikawa na kutana nao kule ocean road ! Nashangaa wananiambia tusaidie jambo fulan baaasi ……….

………..

Uzuri Baadae niliachana na kazi Taasisi ile ya Umma nikajikita kimataifa zaidi
 
Ilichukua miezi 6 kuitwa kwenye kazi uliyofanyiwa interview kwenye moja moto moja baridi hii inavutia kusikiliza
Nashangaa wananiambia tusaidie jambo fulan baaasi .................!
Uzuri Baadae niliachana na kazi Taasisi ile ya Umma nikajikita kimataifa zaidi
Safii na hongera sana 🀝
 
Aisee.
Basi kama ndivyo tumeshawafanyia kazi watu bila kujua.
 
"Spies comes in many shapes and size" hii nukuu niliipata kwenye kitabu cha spies and the traitor cha Ben Macintyre....tokea hapo nikajifunza Jambo kwamba hata mfagia ofisi wa pale ndani kwa afisa au mkuu wa wilaya anaweza kuwa njagu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…