Je, Unaweza Kuwa Jasusi Bila Kujijua? 🤔

Je, Unaweza Kuwa Jasusi Bila Kujijua? 🤔

Mabadiliko Madogo Kwenye Ratiba ya Usafirishaji

Ndugu Msimamizi,

Tunaomba kuhakikisha kuwa mzigo wa wiki hii unashughulikiwa kwa uangalifu mkubwa.

Vifaa vya bustani vilivyochelewa kufika vinapaswa kukaguliwa leo asubuhi.
Ifakiwe kufanyika hivyo kabla ya mchana ili kuepuka usumbufu.
Pia, kumbuka kuwa mizigo mingine inasubiri maelekezo zaidi kutoka makao makuu.

Eneo la kupokelea bidhaa linapaswa kuachwa wazi kila wakati.
Pamoja na hayo, angalia ripoti ya mwisho ya mauzo iliyotumwa jana.
Epuka kuchelewesha taarifa yoyote muhimu inayohusu usalama wa shehena.
Ofisi yetu itaendelea kushirikiana nanyi kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa.

Waliohusika na upakiaji wanapaswa kuripoti mara moja.
Eneo la kusini limethibitishwa kuwa salama kwa sasa.
Uangalifu mkubwa unahitajika wakati wa usiku.
Sababu za kiufundi zimetatuliwa kwa ufanisi.
Ikiwa kuna dharura yoyote, tumia njia mbadala ya mawasiliano.

Asante kwa ushirikiano wako.

Wako mtiifu,
Kitengo cha Ugavi
 
Kama Sheikh Mwaipopo au sio ? 😃
Mkuu hata ile ya Sheikh ni mbinu ya kijasusi pia. Kwenye yale maandamano Sheikh alitumika vizuri sana kununua ule msala😂😂😂

Kuna mtu alishawahi kuitumia kwangu nikajaa mazima pasipo kuelewa kuwa wanamambo yao chini kwa chini. Nimekuja kushtuka kwamba nimeuziwa msala ilikua mwishoni kabisa ikabidi niumalize mwenyewe.

Kwakweli kwasababu huyu mtu ni familia namimi nimemuuzia msala 🤣🤣🤣🫵.
 
JASUSI !

Kwa uelewa wangu jasusi ni mtu anayehusika na kukusanya au kupeleka taarifa kwa siri kwa mtu, taasisi au ofisi nyingine
Mara nyingi anajua anachokifanya na anaweza kulipwa kwa kazi hiyo
Maana yake anajua kabisa mimi nafanya ujasusi kwa ajili ya mslahi fulani
Anaweza kua jasusi kwenye siasa
Anaweza kua jasusi kwenye biashara nk......

Mimi naelewa hivyo kama sipo sahihi naomba nisahihishwe

Lakini swali langu la msingi liko hapa
👇
Je, unaweza kuwa jasusi bila kujijua? 🤔

Yaani, inawezekana watu wakawa wanakutumia wewe kukusanya taarifa mbalimbali huku wewe ukifanya hivyo bila kujua kwamba taarifa hizo zinatumika kwa shughuli za kijasusi?

Mfano, unaweza kuwa unaulizwa maswali fulani, unaombwa taarifa kuhusu watu au sehemu fulani, au unaambiwa ufuatilie jambo fulani ukidhani ni kitu cha kawaida
Kumbe taarifa unazokusanya zinapelekwa mahali pengine na kutumika kwa malengo ambayo wewe huyajui

Sasa unawezaje kutambua kua unatumika kufanya ujasusi au unafanywa kua chanzo cha taarifa

Ni dalili zipi ukiziona ujue hapa kuna namna natumika kufanya Ujasusi

Swali la nyongeza ikiwa kweli mtu huyo anatumika kuafanya ujasusi hata kama mwenyewe hatambui
Je huyo ni jasusi au ni chanzo cha taarifa ?

Chombezo Dar es Salaam ni nyeusi angani ⚫️
ShesRise_1 ✋️
Huyo ni raia mwema
 
Mabadiliko Madogo Kwenye Ratiba ya Usafirishaji

Ndugu Msimamizi,

Tunaomba kuhakikisha kuwa mzigo wa wiki hii unashughulikiwa kwa uangalifu mkubwa.

Vifaa vya bustani vilivyochelewa kufika vinapaswa kukaguliwa leo asubuhi.
Ifakiwe kufanyika hivyo kabla ya mchana ili kuepuka usumbufu.
Pia, kumbuka kuwa mizigo mingine inasubiri maelekezo zaidi kutoka makao makuu.

Eneo la kupokelea bidhaa linapaswa kuachwa wazi kila wakati.
Pamoja na hayo, angalia ripoti ya mwisho ya mauzo iliyotumwa jana.
Epuka kuchelewesha taarifa yoyote muhimu inayohusu usalama wa shehena.
Ofisi yetu itaendelea kushirikiana nanyi kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa.

Waliohusika na upakiaji wanapaswa kuripoti mara moja.
Eneo la kusini limethibitishwa kuwa salama kwa sasa.
Uangalifu mkubwa unahitajika wakati wa usiku.
Sababu za kiufundi zimetatuliwa kwa ufanisi.
Ikiwa kuna dharura yoyote, tumia njia mbadala ya mawasiliano.

Asante kwa ushirikiano wako.

Wako mtiifu,
Kitengo cha Ugavi
Asante kwa maoni mkuu
Karibu tena kwenye mijadala mingine zaidi
 
JASUSI !

Kwa uelewa wangu jasusi ni mtu anayehusika na kukusanya au kupeleka taarifa kwa siri kwa mtu, taasisi au ofisi nyingine
Mara nyingi anajua anachokifanya na anaweza kulipwa kwa kazi hiyo
Maana yake anajua kabisa mimi nafanya ujasusi kwa ajili ya mslahi fulani
Anaweza kua jasusi kwenye siasa
Anaweza kua jasusi kwenye biashara nk......

Mimi naelewa hivyo kama sipo sahihi naomba nisahihishwe

Lakini swali langu la msingi liko hapa
👇
Je, unaweza kuwa jasusi bila kujijua? 🤔

Yaani, inawezekana watu wakawa wanakutumia wewe kukusanya taarifa mbalimbali huku wewe ukifanya hivyo bila kujua kwamba taarifa hizo zinatumika kwa shughuli za kijasusi?

Mfano, unaweza kuwa unaulizwa maswali fulani, unaombwa taarifa kuhusu watu au sehemu fulani, au unaambiwa ufuatilie jambo fulani ukidhani ni kitu cha kawaida
Kumbe taarifa unazokusanya zinapelekwa mahali pengine na kutumika kwa malengo ambayo wewe huyajui

Sasa unawezaje kutambua kua unatumika kufanya ujasusi au unafanywa kua chanzo cha taarifa

Ni dalili zipi ukiziona ujue hapa kuna namna natumika kufanya Ujasusi

Swali la nyongeza ikiwa kweli mtu huyo anatumika kuafanya ujasusi hata kama mwenyewe hatambui
Je huyo ni jasusi au ni chanzo cha taarifa ?

Chombezo Dar es Salaam ni nyeusi angani ⚫️
ShesRise_1 ✋️
Mkuu, jibu ni ndio.

Waweza kuwa jasusi bila kujijua kwa aina mbili ambazo idara au taasisi za usalama hutumia.

1. Kama mtu wao (asset)

2. Mtoa taarifa (informant)

Majasusi wenyewe hupenda kutumia watu wa kawaida sana kupata taarifa zao kwasababu wao ndo wabobezi na walosomea kazi hiyo.

Waweza kukutumia kupata siri, kuwafanyia kazi fulani, kutuma kitu mahala na kupata nafasi ya kuingia sehemu ambayo ina ulinzi mkali (restricted area).
 
Mkuu, jibu ni ndio.

Waweza kuwa jasusi bila kujijua kwa aina mbili ambazo idara au taasisi za usalama hutumia.

1. Kama mtu wao (asset)

2. Mtoa taarifa (informat)

Majasusi wenyewe hupenda kutumia watu wa kawaida sana kupata taarifa zao kwasababu wao ndo wabobezi na walosomea kazi hiyo.

Wawaweza kukutumia kupata siri, kuwafanyia kazi fulani, kutuma kitu mahala na kupata nafasi ya kuingia sehemu ambayo ina ulinzi mkali (restricted area).
Aaah kumbee aisee!
Asante sana mkuu🙏
Karibu kama una nyongeza zaidi
 
Aaah kumbee aisee!
Asante sana mkuu🙏
Karibu kama una nyongeza zaidi

Huyo mtu wao (asset) na huyo mtoa taarifa wao huitwa kwa kiingereza Unwitting asset au Unwitting informant.

Katika ulimwengu wa leo katika mataifa yote hii mbinu imekuwa ni muhimu sana na inokuwa na teknolojia.

Nchi zinoongoza kwa sasa duniani kwa kazi kama hizi ni Russia, China, Iran, Ukraine na Marekani.

Kwa mfano Russia ina assets zake duniani kote na kwa nchi kama Marekani na zile za Ulaya kila siku kimyakimya huwakamata hawa assets na informants na wengine hurudishwa makwao na wengine hufikishwa mahakamani na kufungwa wakipatikana na hatia.

Asset au informant akivuka mpaka na kuingia nchi ingine shughuli hubadilika na huitwa "Espionage".

Ntamalizia baadae ni kwa vipi Jasusi mwenyewe hupata taarifa nyeti kutoka kwa mtu wa kawaida kabisa hata akiwa mpiga deki hapo ofisini kwako.

Au labda nimwachie mazee wengine wamalizie.
 
Back
Top Bottom