Je, unazijua Haki za Mtoto ikiwa Wazazi wake wametengana?

Je, unazijua Haki za Mtoto ikiwa Wazazi wake wametengana?

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
1608109190249.png

Kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 kifungu cha 26 (1) inaeleza kuwa baada ya wazazi kutengana au kuachana (kwa kuzingatia masharti ya sheria ya ndoa) mtoto atakuwa na haki zifuatazo:-

(a) Kuendelea kupata elimu bora aliyokuwa akiipata kabla ya wazazi wake kutengana au talaka;

(b) kuishi na mzazi ambaye, kwa maoni ya Mahakama, ana uwezo wa kulea na kumtunza mtoto katika maslahi bora ya mtoto; na

(c) kumtembelea na kukaa na mzazi mwingine wakati wowote mtoto atapohitaji, isipokuwa mpangilio huo ukiingiliana na ratiba yake ya shule au mafunzo.
 
Upvote 3
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom