Je, unazijua vest wanazovaa wachezaji kwa ndani?!

Je, unazijua vest wanazovaa wachezaji kwa ndani?!

Inside10

Platinum Member
Joined
May 20, 2011
Posts
34,776
Reaction score
42,933
Screenshot_20250723-020513.jpg

JE UNAIJUA HII VEST YA CATAPULT?

-Kuna vest flani hivi wachezaji wamekua wakizivaa wawapo uwanjani au mazoezini, watu wengi wamekua wakitamani kujua zile ni vest za kazi gani au kwanini huwa zinavaliwa.

majibu ni haya hapa.

- Zile vest kitaalamu zinaitwa GPS VESTS. Lakini mara nyingi kifuani hua zinaandikwa Catapult ambao ndio watengenezaji wa hizi vest.

- Catapult ni neno la kigiriki lenye maana ya manati!! Hizi vest zinaitwa hivyo kutokana na muundo wake kufanana na manati. (YES MANATI HAYA YA KUWINDIA)

Sasa tuangali je zinakazi gani?

- Hizi vest hua ni maalumu kwa ajili ya kuwekea vifaa vya GPS tracker. Ambapo mchezaji akiivaa hii vest kwenye eneo la mgongo kuna ka eneo kadogo ambapo hio GPS tracker hua inapachikwa.

Je hizo GPS zinakazi gani?

-Gps tracker kazi yake kubwa ni kufatilia mienendo ya mchezaji akiwa uwanjani.
kwamaana kwamba Mchezaji akivaa hii GPS tracker, Benchi la ufundi linaweza kujua yafuatayo.

a) Amekimbia umbali gani uwanjani
b) Amefika maeneo gani kwa sana uwanjani
c) Amehusika mara ngapi kwenye matukio ya kimpira
d) Nguvu alizotumia uwanjani
Etc.

-Ripoti hii inasaidia bench la ufundi kujua mwenendo wa kikosi chao na sehemu za kuboresha hasa kwenye eneo la kiufundi pamoja na physique ya mchezaji.

Sasa mtu anaweza kuuliza kama hizo GPS hazimuumizi mchezaji awapo uwanja kama akidondoka au anavokimbia.

-jibu ni Hapana haviumizi kwasababu hizo vest zimetengenezwa kwa material maalumu ambayo yanamlinda Mchezaji kutodhurika na hivi vi GPS na ndio maana eneo la kukaa hio GSP in juu ya mgongo sehemu ambayo ni ngumu kufikika hata ikitokea mchezaji anaudondoka.

Credit said hemed wakanda republic
 
Hizi nizitafute ninunue niwavishe wajumbe wa ccm wa kata ili niweze kujua kama kuna mijengeo kuelekea kwa mgombea mwenzangu .

Maana nimeanza kustuka kwangu wanakula ila nasikia kwa huyo jamaa wanakula ni heri nitumie njia hii kuwabaini ili niwakatae .

Nitazinunua alafu niwadanganye ni bullet proof wakati huu wa hatari tunaopambana na nafasi za chama chetu
 
JAMBO jema ILA SINA HAKIKA kama HIZI za HUKU Zina KUWA na huo MFUMO WA kujua yaliyopo kwa mchezaji Haina tofauti na mtuu kuvaa SAA kuaminisha WATU NAYE ana SAA kumbe hata haisemii ni mbovh show off za kijinga na MANISHA kwa hapa bongo. ILA kwa wenzetu Zinaa MANA KUBWA sana mcheza ji AKITOKA uwanjani wanaandika amekimbia kilomita ngapi na kwa spidi GANI MFANO Gareth bale PINDI YUPO Tottenham WALIDAI Kuna mechi bale aliikimbia kwa spidi kiasi KWAMBA alivunja rekodi ya Usain bolt mita mia aliikimbia kwa muda mchache SANA umeona HIYO



Kwishaa



Bro Alex on da beats yoow
 
Hizi nizitafute ninunue niwavishe wajumbe wa ccm wa kata ili niweze kujua kama kuna mijengeo kuelekea kwa mgombea mwenzangu .

Maana nimeanza kustuka kwangu wanakula ila nasikia kwa huyo jamaa wanakula ni heri nitumie njia hii kuwabaini ili niwakatae .

Nitazinunua alafu niwadanganye ni bullet proof wakati huu wa hatari tunaopambana na nafasi za chama chetu
Wajumbe watafurahi sana
 
Back
Top Bottom