Je, ungependa nini kiwemo kwenye Katiba Mpya? Mimi napendekeza Ruzuku ya Vyama vya Siasa iondolewe!

Je, ungependa nini kiwemo kwenye Katiba Mpya? Mimi napendekeza Ruzuku ya Vyama vya Siasa iondolewe!

Mimi ninapendekeza yafuatayo kwenye katiba mpya;
1. Cheo cha Makamu wa raisi kiondolewe abakie waziri Mkuu tu. Hawa watu wawili ni mzigo kwa Taifa.
2. Cheo cha mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya viondolewe wabakie wakurugenzi tu
3. Mawaziri wasiwe wabunge
4. Mabalozi wa shina wasiwe na vyama bali wawe chini ya mkuu wa kata.
5. Iwepo sheria kali sana ya kulinda mapato ya Serikali ili kuzuia wizi wa pesa
6. Kuwe na sheria kali ya kuzuia watu kujenga jenga ovyo ovyo Mipango miji iwekewe kipambele wakiangalia miaka hamsini au mia moja ijayo
7. Mabalozi wa shina wasiwe na vyama bali wawe chini ya mkuu wa kata.

Kwa leo ni hayo tu nitaendelea siku nyingine.
 
Mimi napendekeza kuwe na sera za nchi na si za vyama ukifika muda wa uchaguzi kila chama kitaandaa ilani itakayoeleza namna gani watatekeleza hayo mawazo au malengo makuu ya maendeleo ya nchi.Hii itazuia kila serikali kuja na vipaumbele vyake mara baada ya kuunda serikali mfano enzi za Jk tulikuwa tunaimba uchumi wa gesi kipindi cha Magu akaanza uchumi wa viwanda na kipindi cha sasa tunaimba uchumi wa tozo.
 
Marais kama waliiba au kuchezea pesa wachukuliwe hatua!
Hicho ndio kitu pekee kitawafanya marais wakie shimu kiti hicho kiti cha urais kuliko kujibambikizia mali za Mama Tanzania [emoji1241] bila kujali wana nchi [emoji26]
 
Back
Top Bottom