Je, ungependa nini kiwemo kwenye Katiba Mpya? Mimi napendekeza Ruzuku ya Vyama vya Siasa iondolewe!

Waziri wa Katiba na Sheria ameshapuliza kipyenga cha mchakato wa Katiba Mpya hivyo ni vema tukaanza kuchangia mawazo

Binafsi napendekeza Ruzuku ya vyama vya Siasa iondolewe ili vyama vijifunze Kujitegemea ili vikiingia madarakani visiwe Mchwa wa kutafuna Kodi za Wananchi

Toa mapendekezo yako wahusika watayaona na kuyachukua kutoka hapa

Karibu
Naunga mkono hoja, tena pendekezo kama hili nami nililitoa kwa Blaza Ruzuku kwa vyama vya Siasa: Mnaonaje tumshauri Rais Magufuli aifutilie mbali ruzuku hii? Ni ufisadi Mungu akamtwaa kabla ya kulitekeleza hili, na kiukweli linatekelezaka maana Wenye Matumaini na Upinzani Kushika Dola!, Sahauni! CCM Inajiandaa Kuua Kabisa na Kuuzika Jumla !.
P
 
Fafanua kuhusu kundi maalum na wajumbe wake watatoka wapi?
Wanaweza kua ni wananchi, Bodi fulani ya watu wenye weredi yenye watu waliochaguliwa na wananchi kwa kupigiwa kura na si kura za Siasa, wanaweza kuwepo, watu wenye hekima na heshima, madaktari, wanasheria, wasomi wa kilimo nakadharika kulingana na uhitaji wa waTanzania
 
Binafsi ningependa kwenye katiba mpya. Tuwafungulie MASHTAKA wale wote waliofanya kazi kwenye serikali ya awamu ya Tano. Wote nasisitiza wote. Pia tuwafute kazi jeshi zima la polisi tuanze upya nasisitiza askari polisi wote tuwafukuze kazi warudishe unfom na silaha zetu zote tuanze upya
 
Mimi napendekeza Rais asiwe kinara wa kuhamasisha ufisadi katika nchi kama ilivyo sasa hivi
 
Binafsi ningependa kwenye katiba mpya. Tuwafungulie MASHTAKA wale wote waliofanya kazi kwenye serikali ya awamu ya Tano. Wote nasisitiza wote. Pia tuwafute kazi jeshi zima la polisi tuanze upya nasisitiza askari polisi wote tuwafukuze kazi warudishe unfom na silaha zetu zote tuanze upya
Mbali na hizo, Semeni pia Kuwa Rais akifia madarakani, mkaimu wake, akomee siku 90, na baada ya hapo, Uchaguzi huru ufanyike, na yeye asishiriki mpaka awamu inayofuata akitaka aombe kama asiye kuwa kwenye mgumu, siyo kama mtu aliyemo kwenye mamlaka.

Hii itasaidia kuepusha watu kuwa na unafiki wa kujipendekeza uchawa katika umri ambao hata chawa hawamo miilini mwao!

Sent from my TA-1004 using JamiiForums mobile app
 
Niseme Mimi au useme wewe mbona Kila mtu kaulizwa. What the FCK wrong with you?
 
Waziri wa Katiba na Sheria ameshapuliza kipyenga cha mchakato wa Katiba Mpya hivyo ni vema tukaanza kuchangia mawazo.

Binafsi napendekeza Ruzuku ya vyama vya Siasa iondolewe ili vyama vijifunze Kujitegemea ili vikiingia madarakani visiwe Mchwa wa kutafuna Kodi za Wananchi.

Toa mapendekezo yako wahusika watayaona na kuyachukua kutoka hapa.

Karibu
Ruzuku ikiondolewa maana yake chama tawala ndicho pekee kitakacho survive kwa sababu hazina ipo mikononi mwake !!
 
Makanisa na misikiti kujengwa uraiani liwe ni kosa , katiba ielekeze wanaohitaji kuanzisha kanisa au msikiti wapewe maeneo yenye ukubwa wa namna gani.
 
Waziri wa Katiba na Sheria ameshapuliza kipyenga cha mchakato wa Katiba Mpya hivyo ni vema tukaanza kuchangia mawazo.

Binafsi napendekeza Ruzuku ya vyama vya Siasa iondolewe ili vyama vijifunze Kujitegemea ili vikiingia madarakani visiwe Mchwa wa kutafuna Kodi za Wananchi.

Toa mapendekezo yako wahusika watayaona na kuyachukua kutoka hapa.

Karibu
Chipsi mayai iwekwe katika tunu za taifa pamoja na singeli
 
Yangu ni kwenye uwajibikaji
Viongozi wa kuchanguliwa wawekewe mfumo wa kuwajibika kwenye ahadi ambazo watakuwa wanazitoa wenyewe kulingana na mazingira yao.Kwa mfano
1. Ikiwa ametimiza ahadi zake muhimu kwenye eneo lake kwa 80% na zaidi ndo apite bila kupingwa kwenye chama na uchaguzi mkuu.
2. Ikiwa ametiza ahadi zake muhimu kwa zaidi ya 50%,wagombea wengine wagombee nae ndani ya chama na serikali.
3. Ikiwa hajatimiza ahadi zake kufikia 50% mfumo umteme moja kwa moja yaani aisruhusiwe kuiona hata fomu ya ndani ya chama...yaaani abaki huko aliko.
 
Waziri wa Katiba na Sheria ameshapuliza kipyenga cha mchakato wa Katiba Mpya hivyo ni vema tukaanza kuchangia mawazo.

Binafsi napendekeza Ruzuku ya vyama vya Siasa iondolewe ili vyama vijifunze Kujitegemea ili vikiingia madarakani visiwe Mchwa wa kutafuna Kodi za Wananchi.

Toa mapendekezo yako wahusika watayaona na kuyachukua kutoka hapa.

Karibu
Yohana Mbatizaji unapendaga ugomvi na Chadema wewe!!!
 
Back
Top Bottom