Je, ungependa nini kiwemo kwenye Katiba Mpya? Mimi napendekeza Ruzuku ya Vyama vya Siasa iondolewe!

Je, ungependa nini kiwemo kwenye Katiba Mpya? Mimi napendekeza Ruzuku ya Vyama vya Siasa iondolewe!

Mapendekezo yangu ni:
1. Vyama vya siasa viwe vitatu tu.
2. Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ihamishiwe TAKUKURU
3. Mikataba yote ya Serikali na haswa ya miradi mikubwa iwekwe wazi kabisa na wahusika walioandaa huo mkataba watangazwe wazi na wawe wameweka sahihi document ya kula kiapo kuwa wako tayari kushtakiwa kama mkataba utabainika kutokuwa n manufaa kwa Taifa
4. Sheria za nchi zipitiwe upya na kuboreshwa ili ziendane na wakati. Zipo sheria nyingi zimepitwa na wakati.
5. ..... nitaendelea baadaye..
Hiyo number 3 iko poa sana kwani tumeibiwa mno kwa sababu ya maslahi binafsi au ukilaza
 
Waziri wa Katiba na Sheria ameshapuliza kipyenga cha mchakato wa Katiba Mpya hivyo ni vema tukaanza kuchangia mawazo

Binafsi napendekeza Ruzuku ya vyama vya Siasa iondolewe ili vyama vijifunze Kujitegemea ili vikiingia madarakani visiwe Mchwa wa kutafuna Kodi za Wananchi

Toa mapendekezo yako wahusika watayaona na kuyachukua kutoka hapa

Karibu
Chadema tumekuangalia muda mrefu, Sasa naona unavuka mipaka, tutakufukuza
 
Wabunge walipwe fixed salary yenye makato yoote kuanzia kodi na mifuko ya hifadhi ya jamii... sitting allowance ziondolewe, mafao walipwe kama wastaafu wengine...
Ni kweli kabisa inakuwaje mbunge analipwa sitting allowance na perdiem jml tsh 320000 kwa siku anayohudhuria kikao na mwisho wa mwezi analipwa mshahara kwani alipogombea hakujua kwamba wajibu wake wa kwanza ni kuhudhuria vikao vya bunge ambavyo vitampatia mshahara mwisho wa mwezi
 
Pendekezo lingine ili kuwe na mgawanyo wa madaraka Rais asiruhusiwe kuteua wakuu wa mihimili mingine mfano jaji mkuu na majaji wengine wa mahakama kuu au ya rufani hao wachaguliwe na chombo kingine kwa kuzingatia sifa za kitaaluma na kiuzoefu zitakazoanishwa
Pia dhana ya kusema nchi hii kuna utawala wa kisheria na sheria ni msumeno ionekane kwa kila raia akifanya kosa achukuliwe hatua kusiwe na baadhi ya watu eti wana kinga ya kutoshtakiwa
 
Kwa kuwa maji ni uhai hiyo haki iwe fundamental right ambayo inaweza kudaiwa hata kwa kuishtaki serikali mahakamani kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake kwa walipa kodi
 
Waziri wa Katiba na Sheria ameshapuliza kipyenga cha mchakato wa Katiba Mpya hivyo ni vema tukaanza kuchangia mawazo

Binafsi napendekeza Ruzuku ya vyama vya Siasa iondolewe ili vyama vijifunze Kujitegemea ili vikiingia madarakani visiwe Mchwa wa kutafuna Kodi za Wananchi

Toa mapendekezo yako wahusika watayaona na kuyachukua kutoka hapa

Karibu
  1. Wabunge wawe kimikoa no viti maalumu
  2. Marais wasijengewe majumba wakistaafu hakuna upendeleo watumishi wote wawe sawa
  3. Maneno Mungu wabariki viongozi kwenye national anthem yafutwe
  4. Neno waheshimiwa lifutwe na liwe haraam wote tuitane ndugu inatosha
  5. Viongozi washitakiwe hakuna mtu kuwa juu ya sheria
  6. Scale za malipo kwa watumishi wote wa umma wakiwepo wabunge na viongozi wote zipangwe na wananchi
 
Ikitokea kwa bahati mbaya Rais wa nchi akafariki kuwe na kipindi cha mpito cha miezi 6 then uchaguzi wa Rais ufanyike na muda huo nchi iongozwe na waziri mkuu cheo cha makamu wa Rais kisiwepo kwani hakina tija ni mzigo kwa walipa kodi
 
  1. Wabunge wawe kimikoa no viti maalumu
  2. Marais wasijengewe majumba wakistaafu hakuna upendeleo watumishi wote wawe sawa
  3. Maneno Mungu wabariki viongozi kwenye national anthem yafutwe
  4. Neno waheshimiwa lifutwe na liwe haraam wote tuitane ndugu inatosha
  5. Viongozi washitakiwe hakuna mtu kuwa juu ya sheria
  6. Scale za malipo kwa watumishi wote wa umma wakiwepo wabunge na viongozi wote zipangwe na wananchi
Ni kweli kwani hiyo dua wanaombewa na viongozi waovu waliotia taifa hili katika mikataba ya kimangungo ambayo imesababisha dhahama na madeni ya ajabu ajabu wakijificha kwenye kivuli cha kuwa na kinga ya kutoshtakiwa
 
Waziri wa Katiba na Sheria ameshapuliza kipyenga cha mchakato wa Katiba Mpya hivyo ni vema tukaanza kuchangia mawazo

Binafsi napendekeza Ruzuku ya vyama vya Siasa iondolewe ili vyama vijifunze Kujitegemea ili vikiingia madarakani visiwe Mchwa wa kutafuna Kodi za Wananchi

Toa mapendekezo yako wahusika watayaona na kuyachukua kutoka hapa

Kuhusu elimu, vijana mitaala ifundishwe njia za kutatua changamoto kwenye jamii husika na changamoto za kesho kuanzia darasa la kwanza.

Kijana akimaliza hata darasa la saba/ kidato cha nne ana uwezo wa kujiajiri.

Fani kama kilimo bora chenye tija, chakula kizuri kwa afya na jinsi ya kupika, jinsi ya kuzuia magonjwa kutumia chakula, kuishi vizuri.

Jinsi ya kujenga nyumba, ku-repair baiskeli gari, laptops, computers, phone ziwe compursory kuanzia shule za msingi.

Watoto wafundishwe njia sahihi za kutumia pesa (financial literacy) na accounting, biashara.

Elimu iwepo kwa ajili ya kutatua changamoto zinatoitesa jamii. Iende na wakati sio kukariri vitu visivyomsaidia mwanafunzi au jamii.
Umegusa Chaka la chatu hapo ukitaka watu wakupopoe kwa mawe na virungu gusa ruzuku watakuua Mimi naunga mkono hoja Kila chama kitumie aseti na rasilimali zake
 
1. Katiba itoe tafsiri kamili na sifa ya mtu kutambulika kama mtanzania. Kama eneo la nchi na mipaka yake linatambulika basi na watu wake wanapaswa kuainishwa kikatiba, sifa na hadhi za kuwa mtanzania.
2. Ardhi ya Tanzania iwe ni rasilimali ya watanzania, badala ya ardhi kuwa mali ya Serikali kwa uangalizi wa Rais, ardhi itokanayo na urithi wa kila mtanzania pamoja na ile vijiji irasimishwe kwa kila raia, kila kijiji na hati zitolewe. Ardhi ya hifadhi, Ardhi ya akiba na mito na maziwa vitambuliwe kikatiba na kuwekewa utaratibu wa matumizi endelevu.
3. Katiba iweke wazi wajibu wa mtanzania kuchangia kwenye pato la taifa kwa kulipa kodi na Serikali ihakikishe kila raia anapata elimu, kuajiriwa, matibabu na hifadhi jamii hasa kwa wazee, watoto na watu wenye ulemavu. Kiinua mgogo iwe kwa kila mtanzania aliyeitumika nchi hii. Serikali ilipe mafao kwa wazee na wale wanaokosa kazi baada ya kuhitimu.
4. Katiba ikazie siasa ya ujamaa na kujitegemea, iwe mwiko kwa Serikali kutembeza mabakuli ya kuomba misaada. Hii tabia ya kuanzisha miradi kwa kutegemea bajeti za wahisani, ifanywe na NGO, makampuni na mashirika binafsi, sio Serikali
Itaendelea....
 
5.Kwenye uchaguzi, ili kuondoa utata, kuwe na uchaguzi wa duru mbili. Mshindi apatikane kwa kuvuka nusu ya kura zote halali zilizopigwa na mshindi wa kwanza na wa pili kwenye duru ya kwanza washindanishwe kwenye duru ya pili ambayo ndio mwamuzi.
6. Matokeo kama yana mushkeli yapingwe mahakamani!. Rais na viongozi wote wakuu, waondolewe kinga ya kutoshtakiwa wawapo madarakani. hii itapunguza idadi ya miungu watu na matumizi mabaya ya madaraka.
 
7. Muungano uvunjwe Tanganyika ibaki kama nchi na Zanzibar vilevile. Kila nchi iwe na Rais wake kama ilivyokuwa hapo zamani kisha tuingie kwenye Jumuia ya Afrika Mashariki kama nchi mbili... AU.. Tanzania bara itengeneze majimbo yanayolingana na Zanzibar ili tuunde nchi moja Tanzania, ambayo wakuu wa majimbo wataongoza Serekali ya majimbo yao yanayo jitegemea kama lilivyo jimbo/nchi ya Zanzibar kwenye muungano huku Serikali kuu na Rais wa JMT akiendesha nchi akiwa Dodoma.
 
Moja ya sheria ninazotaka zifanyiwe maboresho nihizi zinazo husu wabakaji, sheria zetu zimeelekezwa kubana kundi moja tu ambalo ni watoto wa kiume

Nahii hata kama kosa hilo linafanywa na wahusika wawili kwa maana ya kwamba utakuta mwanafunzi wa kike anaingia katika mausiano ya mapenzi na mwanafunzi wa kiume wote kwa hiyari yao

Sasa inapotokea msichana huyo akapata mimba basi mtoto wa kiume huesabika kama mbakaji na mwisho wa siku anahukumiwa na kwenda jela

wakati huohuo huyu binti pamoja na kwamba alishiriki kikamilifu kutenda uzinifu huo, yeye hubaki mitaani na kuendelea kusambaza uzinifu mtaani

sheria hiyo inasahau kuwa hawa wote ni wanafunzi wenye akili na utashi wa kujuwa mema na mabaya

Mapendekezo yangu inapotokea wanafunzi wakafanya uzinzi na mmoja wao akapata mimba basi wawili hao kwa pamoja kama ni kifungo wahukumiwe wote

Wakatumikie adhabu yao ili wakitoka wamlee mtoto wao kwa pamoja nahii itasaidia walau kupunguza tamaa za watoto wa kike lakini pia nawao wajue kuwa akifanya ngono zembe akapata mimba jela inamuhusu

Maana tunahubiliwa kilasehemu kuwa mtoto wa kike na wakiume wote nisawa wana akili sawa na haki pia ya kufanya maamuzi juu ya miili yao wanayo
 
1.Napendekeza mishahara ya wabunge ikatwe kodi
2,kima cha chini cha elimu ya mgombea ubunge iwe shahada ya kwanza.
3. spika wa bunge asitoke chama tawala,
4. makamu wa raisi atokee kwenye chama kilichishika nafasi ya pili kwa wingi wa kura
5.wananchi wawe na nguvu ya kufukuza wabunge wao wasiowajibika vzuri
6.umri wa kugombea uraisi uwe kuanzia miaka 30
7.Kila baada ya miezi 3 raisi aandae mdahalo utakaokuwa live kupitia social network yeyote inayowafikia zaidi watanzania wawe live kutoa kero zao na yeye azijibu na atoe suluhu yake
8. Kuwe na wagombea binafsi
9. Tuwe na serikali moja tu kama aiwezekan basi muungano huvunjwe
10.huduma ya afya ndio iwe bure na ni haki ya kila mtanzania
11. Kusiwe na mipaka ya ajira na umiliki wa ardhi kusiwe na utanganyika wala uzanzibar kuwe na utanzania tu sote tuwe na haki sawa ya kuajiriwa popote pale hiwe zanzibar au tanga au popote tanzania hiii na sote tuwe na haki sawa ya umiliki wa ardhi popote pale yaani
12 raisi na viongozi wowote wale washitakiwe wakifanya uhalifu hata kama wapo madarakani
 
Bunge iwe NI KAZI ya kujitolea ili tuwapate wazalendo HALISI.

Vetting ya Majaji na Mahakimu itafutiwe mchujo ambao utazingatia kuwajua makanjanja wanaotumia uhakimu kupora haki.

SERIKALI iwe na watumishi wachache wenye tija Wale wasiotimiza wajibu wao waondolewe kunatakiwa kuwe na ufuatiliaji wa utendaji kazi katika maeneo yote.

Muungano uchunguzwe upya IKIWEZEKANA tuone namna Bora ya kufanya Kwa kadri wanainchi watakavyo ona inafaa.
 
Back
Top Bottom