Je, ungependa nini kiwemo kwenye Katiba Mpya? Mimi napendekeza Ruzuku ya Vyama vya Siasa iondolewe!

Je, ungependa nini kiwemo kwenye Katiba Mpya? Mimi napendekeza Ruzuku ya Vyama vya Siasa iondolewe!

Kuhusu elimu, vijana mitaala ifundishwe njia za kutatua changamoto kwenye jamii husika na changamoto za kesho kuanzia darasa la kwanza.

Kijana akimaliza hata darasa la saba/ kidato cha nne ana uwezo wa kujiajiri.

Fani kama kilimo bora chenye tija, chakula kizuri kwa afya na jinsi ya kupika, jinsi ya kuzuia magonjwa kutumia chakula, kuishi vizuri.

Jinsi ya kujenga nyumba, ku-repair baiskeli gari, laptops, computers, phone ziwe compursory kuanzia shule za msingi.

Watoto wafundishwe njia sahihi za kutumia pesa (financial literacy) na accounting, biashara.

Elimu iwepo kwa ajili ya kutatua changamoto zinatoitesa jamii. Iende na wakati sio kukariri vitu visivyomsaidia mwanafunzi au jamii.
 
Kuhusu makazi napendekeza serikali kujenga nyumba na kuhamasisha watu binafsi na sekta binafsi, uongozi wa vijiji, wilaya mikoa kujenga makazi.

Kwa mpangilio maalum. Vitu kama shule, vyuo, hospitali, maduka, viwanja vya michezo, miundombinu ya maji, umeme, barabara pamoja na ajira, kazi ziende sambamba na makazi mapya.
 
Afya kwa wote iwe bure na nzuri. Universal heathcare, hata viongozi wote na matajiri wasikimbilie kutibiwa nje.

Serikali inaweza kuingia ubia na hospitali, vyuo, makampuni muhimu duniani kuanzisha matawi yao hapa kwa nafuu ya kupata eneo, vifaa na watendaji kwa gharama nafuu.

Masharti yawe kuajiri wazawa kwa kazi tusizozohitaji wataalamu ambao hatuna. Lakini kazi ndogondogo waachie wazawa.
 
Waziri wa Katiba na Sheria ameshapuliza kipyenga cha mchakato wa Katiba Mpya hivyo ni vema tukaanza kuchangia mawazo

Binafsi napendekeza Ruzuku ya vyama vya Siasa iondolewe ili vyama vijifunze Kujitegemea ili vikiingia madarakani visiwe Mchwa wa kutafuna Kodi za Wananchi

Toa mapendekezo yako wahusika watayaona na kuyachukua kutoka hapa

Karibu
1. Kinga ya Rais iondolewe, kabla, wakati na baada ya uongozi wake
2. Matokeo ya kura za urais yapingwe mahakamani
3. Rais apewe mshahara na atumie mshahara wake ambao utakatwa kodi katika kumtunza akiwa Ikulu
4. Familia ya Rais isiwe na kinga, isitumie hela za umma
5. Waziri asiwe mbunge. Mbunge akiteuliwa kuwa waziri, ubunge wake ukome, achaguliwe mbunge mwingine
6. Kuwepo na mgombea Binafsi (iruhusiwe kuwa Rais au Mbunge ambaye hatokani na vyama vya siasa)
7. Viongozi wa mihimili asiteuliwe na Rais
8. Iondolewe nafasi ya Makamu wa Rais abaki Rais na Waziri Mkuu
9. Mwenyekiti wa Chama asiwe Kiongozi katika serikali
10. Cheo kimoja kwa mtu mmoja (kofia zaidi ya moja iondolewe)
11. Mwenyekiti wa TRA awe ni mfanyabiashara si mfanyakazi wa serikali
Naishia hapa kwa leo

NB: Sheria itungwe ili Mtu yeyote atakayehusika na uandaaji au upitishwaji wa katiba hii, asiruhusiwe kugombea uongozi wa nchi hii kwa miaka 20 ijayo na wala asiajiriwe serikalini ili kuondoa uwezekano wa watu kujitungia katiba kwa manufaa yao.
 
Mimi nataka viongozi wote, elimu ya chini iwe degree moja.
Napendekeza wananchi wote wahusishwe hata darasa ya saba wapewe nafasi, asilimia kadhaa, kutetea maslahi ya wadau wao. Sababu wanajua changamoto zao na jinsi ya kuzitatua kuliko ambao hawajapitia changamoto hizo.

Muhimu kila kundi liwakilishwe. Demokrasia halisi, jumuishi. Babu yako inawezekana hajui kusoma au darasa la saba lakini ana busara, akili kubwa, madini, mchango kwa taifa.
 
Wabunge/Madiwani wa Viti maalum ✖️

Wakuu wa Mikoa na Wilaya ✖️
Ma DED kusimamia uchaguzi ✖️

Mamlaka ya Rais kupunguzwa ✔️

Tume Huru ya uchaguzi ✔️

Mgombea Binafsi ✔️

Matokeo ya Urais kupingwa katika mahakama isiyo ingiliwa na wanasiasa ✔️

Uraia pacha ✔️

Muungano wa Serikali 2 ✖️

Muungano wa Serikali 3, au kuwepo na Serikali 1 tu, au Muungano wenyewe usiwepo kabisa ✔️

Kupunguza ukubwa wa Serikali ✔️

Kupunguza idadi ya Wabu nge kwenye Bunge la JMT ✔️

Vyama vya wafanyakazi kuwa taasisi huru, zisizo fungamana na serikali ✔️
 
Sekta kama ualimu, unesi, udaktari, polisi, jeshi, zipewe hadhi inayostahili na kulipwa vizuri.

Sekta binafsi iondolewe ukiritimba, kodi zisizo na kichwa wala miguu na longolongo kuanzisha biashara kulipa kodi, kupata vibali na kuuza mazao na products zao nje ya nchi.

Serikali iwasaidie sekta binafsi kuuza vitu nje na kuwasaidia vijana kusafiri kufungua macho (Gap year).
 
Waziri wa Katiba na Sheria ameshapuliza kipyenga cha mchakato wa Katiba Mpya hivyo ni vema tukaanza kuchangia mawazo

Binafsi napendekeza Ruzuku ya vyama vya Siasa iondolewe ili vyama vijifunze Kujitegemea ili vikiingia madarakani visiwe Mchwa wa kutafuna Kodi za Wananchi

Toa mapendekezo yako wahusika watayaona na kuyachukua kutoka hapa

Karibu
Katiba ni msimamo, ni imani, ni nadhiri. Kama imani yangu ni Serkali 2 na wewe unataka Serkali 1 na mwingine serkali 3, hakuna sababu ya kutoa maoni. Kila Chama kitoe Ilani yake ikijieleza kwa nini wanataka Serkali 2 au 1 au 3, halafu Wananchi wapige kura ili mshindi tumjue na aweke serikali anayoiamini.
 
Waziri wa Katiba na Sheria ameshapuliza kipyenga cha mchakato wa Katiba Mpya hivyo ni vema tukaanza kuchangia mawazo

Binafsi napendekeza Ruzuku ya vyama vya Siasa iondolewe ili vyama vijifunze Kujitegemea ili vikiingia madarakani visiwe Mchwa wa kutafuna Kodi za Wananchi

Toa mapendekezo yako wahusika watayaona na kuyachukua kutoka hapa

Karibu
Napendekeza kuondoa vyama vya siasa, kuwe na chama kimoja tu Cha kuongoza nchi, ila Serikali iwajibishwe na kundi maalumu pale inapoleta shida, kufanya Siasa ni kutumia pesa ambazo masikini wanazihitaji ili wapate huduma
 
Napendekeza wote tupitie JKT litakaloboreshwa ukimaliza kidato cha nne kwa miezi sita, hata la saba, hawajaenda shule kabisa wapewe nafasi kujifunza na kufundishwa na walisoma hapo JKT.

Kufundishwa maadili, uongozi bora, jinsi ya kupambana na wahalifu, kutumia silaha, kilimo, chakula bora, uzalendo na kuilinda nchi.
 
Kupunguza mishahara ya wabunge
Serikali ya majimbo ianzishwe na kuondoa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wakajiajiri na wao au kuwa na mishahara sawa na walimu na kada nyingine
 
Rais wa Tanzania lazima atoke Tanganyika,
Haiingii akilini kisiwa chenye watu milion mbili, kitoe marais wawili kuongoza watu milion 60,

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app

Muungano uangaliwe upya. Maslahi ya wengi, ya taifa yawe kipaumbele kwa nchi mbili husika.

Rais akifa madarakani, kipindi cha mpito na uchaguzi mpya ndani ya miezi mitatu.
 
Mimi napendekeza,kuwe na ulazima kushitakiwa "YEYOTE ATAKAYEMBAMBIKIA KESI MTU"
Mwingine.

Uhahitaji katiba mpya, mfumo sahihi, majaji hawachaguliwi, kuteuliwa na Rais bali na tume maalum inakayohusisha wadau wote Tanzania na kuhitimishwa na kuhakikiwa na Bunge.

Waende kwenye tume na bungeni kujitetea ( confirmed) jinsi gani watahakikisha haki inatendeka. Historia zao ziangaliwe. Waulizwe maswali magumu.

Kazi yao iwe kwa miaka miwili halafu wanagombea tena tukiangalia historia yao, utendaji wao, maamuzi yao miaka miwili iliyopita. Hivyo hivyo kwa rais na viongozi wote.
 
Napendekeza kuondoa vyama vya siasa, kuwe na chama kimoja tu Cha kuongoza nchi, ila Serikali iwajibishwe na kundi maalumu pale inapoleta shida, kufanya Siasa ni kutumia pesa ambazo masikini wanazihitaji ili wapate huduma
Fafanua kuhusu kundi maalum na wajumbe wake watatoka wapi?
 
Napendekeza kuondoa vyama vya siasa, kuwe na chama kimoja tu Cha kuongoza nchi, ila Serikali iwajibishwe na kundi maalumu pale inapoleta shida, kufanya Siasa ni kutumia pesa ambazo masikini wanazihitaji ili wapate huduma
Muhimu kusiwe na chama kabisa. Vyama vinaleta utengamano. Ubinafsi. Maslahi ya kichama kwanza badala ya Taifa kwanza.

Kila Mtanzania aweze kugombea na kuwakilisha jamii yake.
 
Back
Top Bottom