adriz
JF-Expert Member
- Sep 2, 2017
- 17,595
- 39,893
Moja kwa moja...
Jf imekuwa tofauti na mitandaoni wengine watu wengi tunatumia majina na picha fake kama utambulisho wetu wachache sana wanaotumia utambulisho wao halisi , hali hii inaelekea ugumu kukutana na kuwajua Wana Jf mtaani tofauti na mitandao mengine. Na mtu anaweza kujutajia account zake mitandao mengine ila sio Jf.
Tukija upande wangu nilijua Jf kipindi nipo Kidato Cha kwanza 2015 nikawa naperuzi kwa kiswasadu kutumia freebasics kama guest , wakati nipo form three 2017 nikajiunga rasmi . Kipindi hiko nilikuwa comfortable watu kunijua kama nipo Jf nilianza nyumbani na mtaani kuuliza watu kama wapo Jf huku nikiwapa Faida zake na rafiki zangu kipindi hiko mtaani walinipa jina "Mzee wa Jamii " wengine wakanipa jina "Mzee wa freebasics" maana nilikuwa najitenga karibia kila siku masaa mengi kwa siku kila wakichungulia wananikuta nipo Jf au freebasics nikiperuzi.
Upande wa shuleni O_level baada ya kuonekana mtaalamu sana darasani na nauelewa mkubwa wa mambo mbalimbali watu wakipeana stori za uwongo almaarufu kama chai Mimi nakuja kupinga kwa facts kiasi ambacho nikawa maarufu nje ya ukipanga wa darasani nikawa kama gugo yao owatu wakibishana kitu shuleni au kukitokea jambo Lina utata katika kila sekta linaletwa kwangu kama judge nifanye uchambuzi na kutoa conclusion
Baadhi ya Wanafunzi wakawa wananifuata kwamba unique information zangu natoa wapi nikawaambia mara nyingi napenda kujisomea vitabu na Kuna mtandao natumia unaitwa Jf una madini ya kutosha , uchambuzi na habari za uhakika kutoka sehemu mbalimbali unanisaidia sana kukuza Maarifa na kupata taarifa mbalimbali . Nikawaekekeza jinsi ya kujiunga mmoja nikamtajia hadi ID yangu tukutana humu siku Moja.
Nilipofika Advance nilikuwa sitaki kabisa mtu kujua kuwa natumia Jf kabisa nakumbuka siku Moja class Wanafunzi wenzangu katika stori zao wakaitaja Jf nikauliza ndio kitu gani wakasema mtandao Fulani hivi wa Wazee na mambo ya Siasa , nikawauliza unajiungaje wakaniambia utajizeesha huko hapakufai kumbe Mimi ni Expert member kabisa nipo kitambo nilikuwa nawachora tu .
Nilipofika chuo vilevile nilikuwa sitaki watu wafahamu kuwa nipo Jf na wakati natumia nahakikisha hakuna mtu ananiona pembeni , sasa kuna siku wakati natumia Kuna rafiki alikuwa nyuma sikumuona vizuri na wakati naperuzi akastuka akasema kumbe upo Jf , niligeuka kwa hasira sana nikasema hapana sipo Kuna kitu nilikuwa nagugo kikaniketa Jf . Bahati nzuri hakuona ID yangu basi akaniona mshamba kwa kuwa sijui Jf na mimi nikajifanya mshamba zaidi nikamuacha awe ananielekeza kuhusu Jf kumbe namchora tu yeye ndio kaijua juzi tu.
Kuna sehemu nilikuwa napiga kibarua cha muda , mfanyakazi mwezetu alitumwa kazi na boss aende mahali Kuna jambo akalikamilishe , baada ya kumaliza hiyo mission tukamuuliza umewezaje kumaliza kazi kwa urahisi licha ya ugeni ? akasema aliienda Jf akasearch na kusoma maoni kwenye nyuzi fulani akapata maelekezo yote akayafanyia kazi . Nikajifanya Jf sijui akashangaa kweli mtu kama Mimi sijui Jf akaahidi kunielekeza kutumia na kunisaidia kufungua akaunti Jf . Huyo jamaa alikuwa mtu mjuaji kazini , mcheshi na mjanja sana nilikuwa najifanya boya ili nimtege anitajie akaunti yake Jf nikamcheke chooni maana kwa haiba yake nikaImagine lazima ID yake itakuwa maarufu sana na tutakuwa tunabishanaga hata Jf maana tulikuwa tunachangamsha kijiwe kazini kwa topic ngumu na kubishana.
Mpaka sasa sipo comfortable mtu yeyote kujua natumia Jf na kujua ID yangu ndio kabisa sitamani , ikitokea kitu nimeiona Jf nilieleza kwa mtu au rafiki yangu nasema tu nimeona taarifa mtandaoni bila kuitaja Jf ila kupeana namba na mtu Jf kukutana na kuwasiliana kwa jia ya kawaida na kuwa marafiki kutokea Jf hilo nipo comfortable nimefanya sana ...
Je , kwa upande wako vipi watoto wako , mkeo , mumeo , marafiki , ndugu , wafanyakazi wenzako na classmate upo comfortable wao kujua kuwa upo Jf na kuijua ID yako ?
#UziTayari