Je, USA kuivamia Iran ili kumuunga mkono Israel kwenye vita inayoendelea ni mwanzo WW3

Je, USA kuivamia Iran ili kumuunga mkono Israel kwenye vita inayoendelea ni mwanzo WW3

BANDOKITITA

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2022
Posts
1,625
Reaction score
3,014
Binafsi ninaona kitendo cha USA kuipiga Iran km sehemu ya kuungana na Israel ni mwanzo wa vita kuu ya 3 ya dunia.

Kwanza Washirika wote wa Iran akiwemo Russia ilishaonya mapema mpango wowote wa USA kuingia moja kwa moja ktk hiyo vita.

Pili, kwa mjibu wa sera za Iran nchi yoyote ikiivamia lazima ijibu kwa ukali zaidi.

Kwa alichokifanya USA nchi nyingi zinaanza kujiona km siyo salama hivyo kumuunga mkono Iran itakuwa ni chaguo lao sahihi.

Swali ni je km vita ya 3 ikitokea hali itakuwaje ukiangalia uwezo wa NATO na Iran allies ( North korea, Russia, Pakistan, China etc)
 
Mh! hakuna vita ya tatu ndugu watatusuana washirika tu lakini jua mataifa mengi mno yanaogopa vita maana hata ukishinda utakuwa hoi kwa kila kitu!, so usifikiri kirahisi tu WW3.
Hata zile mbili zilizopita hazikufaa kuitwa WORLD WAR maana mataifa mengine hata yalikuwa hayajui kinachotokea, pia wakoloni ndo walikuwa wanawachukua watu kwa lazima wakapambane kitu ambacho kwasasa hakuna anaeweza kufanya hivyo!.

By the way sasahivi unapoona jambo limetokea ni limeratibiwa, calculation zimeshapigwa nyingi!.
 
Urusi pindi anaanza vita na Ukraine alisemaga, nchi yeyote itakayojaribu saidia Ukraine, atabadili historia ya dunia.
Watu wakasema hii ni ww3
 
Mataifa mengi hususan ya kiarabu, hayampendi muiran japo hawasemi ila ukiangalia matendo na mwenendo wao utajua Kuna issue. May be waungane this time round
 
Hakuna kitu kinaitwa vita ya dunia. Mtu atapigwa ataamua kutulia tu kutafakari hasara. Kumbuka hata Mmarekani katumia gharama kubwa mno kurun zile ndege mpaka Iran na kupiga mabomu ya G 57. Ni silaha za Gharama mno. Na hapo kumbuka kafanya hivyo kuwatisha visabengo wengine kama kina Hisbola, Houth na wengineo wanamchokoza yeye na last born wake Israel
 
Hakuna cha ww3 wala nini, iran atachapwa peke yake na hakuna ma kumsaidia, umoja wa makobazi ulijadili ila hawatathubutu kuingia vitani kumsaidia
 
Binafsi ninaona kitendo cha USA kuipiga Iran km sehemu ya kuungana na Israel ni mwanzo wa vita kuu ya 3 ya dunia.

Kwanza Washirika wote wa Iran akiwemo Russia ilishaonya mapema mpango wowote wa USA kuingia moja kwa moja ktk hiyo vita.

Pili, kwa mjibu wa sera za Iran nchi yoyote ikiivamia lazima ijibu kwa ukali zaidi.

Kwa alichokifanya USA nchi nyingi zinaanza kujiona km siyo salama hivyo kumuunga mkono Iran itakuwa ni chaguo lao sahihi.

Swali ni je km vita ya 3 ikitokea hali itakuwaje ukiangalia uwezo wa NATO na Iran allies ( North korea, Russia, Pakistan, China etc)

Iran yuko na nani? Hakuna cha WWW3 wala nini.
 
Ni mwanzo wa iran kufanya jaribio live la nuclear bombs ....natabiri kuwa siku si nyingi jaribio la bomu kufanyika...labda ashauriwe na marafiki zake wa china na urussi kutokufanya
 
Mimi nachokiona Marekani wameamua kuitoa Sadaka Israel ili watimize mpango wao wa kushambulia Nuclear za Iran.
Kinachotokea Israel Marekani na Netanyahu wanakijua na walijua kitatokea but kwao wanaona hasara yake ni ndogo kuliko Iran kuwa na Nuclear.
WAKIHAKIKISHA WAMESHAMBULIA NUCLEAR HAWATAJIBU SHAMBULIZI LOLOTE DHIDI YA IRAN
Na Iran asipoona Mashambulizi tena atatulia so Vita itaishia hapo
 
Hakuna WW3 hizo porojo za Russia kutishia walimwengu.

Kama ni kweli vianze nasi tuone vina kuwaje.
 
Kwanza ndugu mleta mada futa kichwani kitu kinachoitwa VITA YA DUNIA. Hakujawahi kuwa na vita ya dunia ya I wala ya II, hii habari imeenezwa na baadhi ya nchi za magharibi na ulaya kwa lengo la wao kujikweza tu.

Wewe hujiulizi kwan:-
1. Congo na Rwanda wanapigana miaka yote husikii wakiita vita ya dunia?
2. Palestine kila mara inapingana na Israel husikii wakiita vita ya dunia?
3. Russia inapingana na Ukraine mwaka wa tatu huu husikii wakiita vita ya dunia?
 
Mtu ndio kapigwa hivyo,mukiendeleza fyokofyoko mtaletewa kichwa cha Ayatollah kwenye sinia la wali.
 
Niwaombe wachangiaji tuchangie bila mihemko ya upande wa imani. Mada imeletwa ili watu kuchangia maoni siyo kushambulia mada kwa mlengo wa kidini.

Haya twende kazi
 
Hakuna kitu kiitwacho vita ya 3 ya dunia,sasa hivi zile nchi zilizounga vita ya pili ya dunia zimekua nchi huru tofauti na miaka ile ambayo zilikua zinatawaliwa na Uingereza
Nchi nyingi sasa hivi zinapambania kujenga uchumi haziwezi kuingia ktk mgogoro au vita ambazyo havina msaada na vitadhoofisha uchumi wa nchi zao.
 
Back
Top Bottom