Je, ushawahi kukumbwa na hali ya kumchukia mtu bila sababu?

Je, ushawahi kukumbwa na hali ya kumchukia mtu bila sababu?

Gracious philipo

New Member
Joined
May 1, 2023
Posts
4
Reaction score
5
Je, ndugu ushawahi kukumbwa na hii hali ya kumchukia mtu bila sababu?

Hii hali imekuwa ikinipata kwa nyakati tofauti kulingana na eneo nililopo yaani najikuta namchukia mtu fulani, hajawahi nikosea chochote lakini najikuta tu nafsi yangu haimpendi hata kumuona tu.
 
Hakunaga chuki isiyo na sababu.

Yawezekana hata maelezo yako yakawa sababu.

Umelelewa vibaya....unajikuta na wivu na kila aliekuzidi kitu mwisho wivu unageuka chuki
 
Huwa inatokea nasikia ukiwa na mimba.

Mie huwa inanikuta siku chache kabla ya period...inapotea yenyewe baada ya muda.
 
Je, ndugu ushawahi kukumbwa na hii hali ya kumchukia mtu bila sababu?

Hii hali imekuwa ikinipata kwa nyakati tofauti kulingana na eneo nililopo yaani najikuta namchukia mtu fulani hajawahi nikosea chochote lakini najikuta tu nafsi yangu haimpendi ata kumuona tu
Kapime kama una mimba
 
Hakunaga chuki isiyo na sababu ..
Yawezekana hata maelezo yako yakawa sababu...

Umelelewa vibaya....unajikuta na wivu na kila aliekuzidi kitu mwisho wivu unageuka chuki
Hapana ndg sio hivyo maana kuna mwingine najikuta namchukia lakini hana kitu chochote cha kunizidi kabisa.
 
Mimi haijawahi kunitokea... ila nadhani inaweza ikawa kweli hiyo hali ipo, maana unaweza kuta mtu amekuzidi kila kitu kuanzia uzuri, hela na kila kitu ila anakuonea wivu wewe usiye na chochote.
 
Hiyo ni hali ya kawaida wala usijipe shida.

Waswahili husema damu haziendani.

Wala hakuna sababu eti kakuzidi uzuri, kipato n.k

Nyie mnaopinga hamuoni huku JF watu wanachukiana mpaka kutukanana ilhali hawajuani?

Wakati mwingine unampenda mtu bila sababu pia.
 
Back
Top Bottom