Wazazi huona mengi ambayo huenda wewe hukuyaona kwa huyo binti.
Kwa kukukataza kuendelea kuwa naye haikuwa wanakuonea wivu au wana chuki juu yako, hapana, isipokuwa wanataka mtoto wao atue kwenye kiota kilicho salama.
Amini nakuambia, wazazi wamekuepusha na janga kuu.
Ila na hii ya kuwaita wazazi wako maboya si jambo la kukubalika kwenye jamii wa watu waliostaarabika.
Kama umelisema hilo kwa hasira tu, basi jitahidi kuzidhibiti hasira zako.
Nikijibu swali lako; sijawahi kuwaona wazazi maboya kwa ajili ya mapenzi.
SUKAH