Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Katika moja ya hotuba zake muhimu kwa nchi hii wakati wa uhai wake Mwalimu Nyerere aliwahi kutoa utabiri kuwa upinzani wa dhati nchini utatoka ndani ya CCM.
Kutokana na kujitokeza kwa mwanasiasa, Bernard Membe kudai kuwa amepania kuchukua fomu ya kugombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kwa tiketi ya CCM, ndiko kunakonifanya nione kuwa utabiri wa Mwalimu Nyerere unaweza kuanza kutimia katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Kwa maelezo anayotupa yeye mwenyewe, Bernard Membe, kuwa amepania kugombea nafasi ya Urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kwa tiketi ya CCM, tena akiendelea kusisitiza kuwa Kuna kundi kubwa sana la wanaccm linalomwunga mkono kwa uamuzi wake huo, ila kwa sasa hatawataja kwa kuhofia kuwa watafukuzwa ndani ya CCM, kutokana na uendeshwaji wa chama hicho ambao umejaa vitisho na kutotaka kusimamia Katiba ya chama chao kwa hivi sasa.
Ingawa Mheshimiwa Membe, anaweza hesabika kuwa siyo mwanachama tena wa CCM, kwa kile kinachodaiwa kuwa amefukuzwa uanachama wa CCM, hata hivyo yeye mwenyewe amekaririwa akisema kuwa kikao kilichomfuta uanachama cha Kamati Kuu ya CCM ni batili, kwa kuwa kikao pekee cha kumfukuza yeye uanachama wake kilipaswa kuwa cha Halmashauri Kuu ya CCM, ambacho hadi sasa hakijakaa.
Pamoja na madai yake ya uvunjaji huo wa wazi wa Katiba ya CCM, katika kuvuliwa uanachama wake, Mheshimiwa Membe, kwa ujasiri mkubwa.na bila unafiki, ameendelea kudai kuwa yeye bado ni mwanachama halali wa CCM, kwa mujibu wa Katiba ya CCM.
Katika hali halisi inaonekana kuwa wapo wanaccm wengi nchini, ambao hawaafiki kwa mambo yanavyoendeshwa hapa nchini, ya uminywaji wa haki za binadamu, ukandamizaji wa demokrasia, kuvifungia vyombo makini mbalimbali vya habari na matumizi ya vyombo vya dola kuminya upinzani, kwa manufaa ya chama cha CCM , kwa hiyo wapo nyuma ya Mheshimiwa Membe, ambaye amejitokeza bila hofu yoyote, pamoja na hatari anayoiona kwake ya utawala huu wa "mkono wa chuma" kwa lengo la kuiokoa nchi yetu, isiendelee kuzama katika utawala huu usiozingatia Katiba ya chama chao wala Katiba ya nchi, ambayo viongozi wakuu wote wa nchi, waliapa kuitii na kuitekeleza kabla hawajaanza utumishi huo wa Umma
Hebu tusubiri tuone kama alivyotuambia yeye mwenyewe, Bernard Membe, kuwa lolote linaweza tokea, kati ya hivi sasa hadi mwezi October mwaka huu!