Kutokuheshimu katiba,
Kutokuheshimu sheria,
Ubabe,
Uonevu,
Kutokufuata mazuri yaliyoanzishwa na watangulizi,
Kujifanya anajua kila kitu.
Vyama vya Upinzani vipo kikatiba,vinaruhusiwa kufanya Shughuli za kisiasa kikatiba.
Suala la kudai katiba mpya sio la C hadema,Ni la Watanzania wote,wakiwemo wa dini zote,vyama vyote,wanaCCM,wakulima,wafanyakazi,wafanyabiashara,wanafunzi,vikundi mbalimbali na watu wenye mahitaji maalumu.
Chadema wanadai wao kama wao,na wengine hawajakatazwa kudai katiba nzuri.
Katiba mpya ikija,wote tutafaidi wanaoitaka na wale "wanaojifanya kuikataa".
Yule bwana hakuheshimu chochote,hakuheshimu viongozi waliomtangulia Wala viongozi wa dini.
Alijiona Yuko juu ya kila kitu.
Hakua na hoja zenye nguvu,Bali alikua na hoja za mabavu.
Legasi aliyotuachia Ni mabavu katika kila kitu.
Nchi haitawaliwi kwa mabavu nchi inatawaliwa kwa kufuata katiba Bora na busara.
Kuna msururu wa watawala wababe Sana duniani Leo hii hawapo madarakani,wengine wapo magerezani na wengine makaburini Dunia wameiacha,mabavu ya Nini?
Hamjifunzi tu?
Kwa Nini msiache upendo mkakumbukwa kwa mema milele?