Hayati Dr John Pombe Joseph Magufuli kuna mengi ya kukumbuka uliyoyafanya na kuyatekeleza wakati wa uhai wako hapa duniani lkn mimi nitakumbuka haya yafuatayo kwa uchache.
1.Uchapa kazi wako tangu ukiwa waziri hadi ukiwa Rais na hadi unatutoka.
2.Usimamizi wa Rasilimali za nchi yetu.
3.Ujenzi wa Miundo mbinu kama vile barabara,Reli,madarasa,hospital na umeme,
4.Kuthibiti ujambazi wa kutumia siraha
5.Kurejesha nidhamu kazini kwa watumishi wa Umma
6 Kutokomeza kabisa mauwaji ya albino
7.Kutetea wananchi wa kipato cha chini ktk utawala wako.
Yapo mengi ya kukumbuka ila mimi nimechagua haya saba tu ili waje wengine nao watukumbushe mengine.
Ayubu14:1. Siku za mwanadamu ni chache mno Nazo zimejaa taabu.