Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?
Huyu mzee anahitaji kwenda kumzika mwanaye, tumchangie aende chato kwa chochote utakachojariwa! Ametoa number yake ya simu!
Daaah! Mungu na maajabu yake, usimdhihaki mtu maana huijui kesho yako, namkumbuka kibajaji akimkejeli mamvi
 
Kama kichwa cha habari hapo juu,nimeamini mheshimiwa Rais Maghufuli alipendwa na watu wengi,hasa ni kutokana na utendaji kazi wake wa kasi. Ndani ya muda mfupi kafanya mambo makubwa. Nitazungumzia baadhi ya mabadiriko aliyoyafanya kwa muda mfupi na yameleta sura mpya na yenye tija
1. Fry over za Tazara na Ubungo kiukweli zimeleta mabadiriko makubwa na muonekano mpya na sura tofauti ya mji.

2. Uwanja wa ndege JKN hasa Terminal 3 imeleta sura nzuri na ya kimataifa kabisa.

3. Makao makuu Dodoma. Ameufanya uwe mkoa wa kibiashara sasa. Umekuwa mji uliochangamka. Imeongezewa na ikulu ya Chamwino,imeufanya mji wa Dodoma kupendeza.

4. Bwawa kubwa la umeme. Hili likimaliziwa litakuwa mkombozi wa umeme kwa nchi yetu.

5. Utendaji maofisini angalau ulikuwa umebadirika baada ya yeye kuingia madarakani. Kiasi chake kulikuwa na watendaji kujituma.

6. Upande wa rushwa,alijitahidi sana kuipunguza kwa kiasi kikubwa,japo si rahisi kuimaliza,lakini kwa kiasi kikubwa watu walikuwa wanaogopa kwa kiasi fulani kuhusu rushwa. Hasa zile ziara zake za kustukiza ziliwafanya idara nyingi za serikali kuogopa kwa kiasi fulani.

7. Ujenzi wa barabara za kuunganisha nchi kila pembe ya nchi.

8. Sekta ya madini,japo tulikuwa bado lakini alijitahidi sana kuwabana wawekezaji upande wa madini,ili nchi nayo tuweze kunufaika.

9. Alivyoingia tu madarakani alianza moja kwa moja kufunga mirija ya mafisadi hasa eneo la bandarini. Alipambana sana. Alinifurahisha sana. Hasa zile ziara za kustukiza pale bandarini,zimeleta mabadiriko makubwa sana pale bandarini.

Yapo mengi lakini hayo ndio nimeyaona.

Buriani mheshimiwa Rais Maghufuli. Tutakukumbuka kwa mabadiriko makubwa
 
Chuma ,,alifanya mengi mazuri kuliko mabaya hata ayo mabaya yalikuwa na sababu mwendo kaumaliza jemedari wetu pumzika kwa amani.
 
Mimi nitakumbuka hotuba zake.
Anko alikuwa ana nanga sana.
Yani anakuharibia hachagui cha kusema. Hahahaa
 
Ulitaka mpk uone? Yeyote mwenye mamlaka kinachofanyika chin yake anatakiwa kuwajibika.
Kamuuwa nani? Weka ushahidi hapa ukishindwa kaa kimya kojoa ulale.

Kwa kuwa upo kwa ajili ya kupinga na kukosoa kila kitu endelea hivyo hivyo mimi nitamkumbuka kama raisi wangu au unataka nikukumbuke wewe?
 
Nitamkumbuka kwa kubomolewa kwa nyumba za Kimara Hadi Kiluvia.
 
Shehe wa mkoa wa Mwanza amesema waislamu watamuenzi hayati Magufuli kwa sababu ndiye aliyewezesha Bakwata kuwa na msikiti mkubwa kuliko yote Afrika ya mashariki...
Ule msikiti bila usimamizi wake usinge isha.

Kipindi cha nyuma gadaf alitoa hela ujengwe.

Msikiti pale waliishia kuweka tu jiwe la msingi.

Magufuli kwenye kusimamia mambo hana mfano aise

Ova
 
Loho mbaya na kuwatesa wafanyakazi pasipo kujali maslahi yao
Ujenzi wa sgr
Kuua bei za mazao mfano korosho mbaazi nk
Utumbuaji
Ununuzi wa ndege
Ujenzi wa vituo vya afya kajitahidi sana
 
Back
Top Bottom