Kama kichwa cha habari hapo juu,nimeamini mheshimiwa Rais Maghufuli alipendwa na watu wengi,hasa ni kutokana na utendaji kazi wake wa kasi. Ndani ya muda mfupi kafanya mambo makubwa. Nitazungumzia baadhi ya mabadiriko aliyoyafanya kwa muda mfupi na yameleta sura mpya na yenye tija
1. Fry over za Tazara na Ubungo kiukweli zimeleta mabadiriko makubwa na muonekano mpya na sura tofauti ya mji.
2. Uwanja wa ndege JKN hasa Terminal 3 imeleta sura nzuri na ya kimataifa kabisa.
3. Makao makuu Dodoma. Ameufanya uwe mkoa wa kibiashara sasa. Umekuwa mji uliochangamka. Imeongezewa na ikulu ya Chamwino,imeufanya mji wa Dodoma kupendeza.
4. Bwawa kubwa la umeme. Hili likimaliziwa litakuwa mkombozi wa umeme kwa nchi yetu.
5. Utendaji maofisini angalau ulikuwa umebadirika baada ya yeye kuingia madarakani. Kiasi chake kulikuwa na watendaji kujituma.
6. Upande wa rushwa,alijitahidi sana kuipunguza kwa kiasi kikubwa,japo si rahisi kuimaliza,lakini kwa kiasi kikubwa watu walikuwa wanaogopa kwa kiasi fulani kuhusu rushwa. Hasa zile ziara zake za kustukiza ziliwafanya idara nyingi za serikali kuogopa kwa kiasi fulani.
7. Ujenzi wa barabara za kuunganisha nchi kila pembe ya nchi.
8. Sekta ya madini,japo tulikuwa bado lakini alijitahidi sana kuwabana wawekezaji upande wa madini,ili nchi nayo tuweze kunufaika.
9. Alivyoingia tu madarakani alianza moja kwa moja kufunga mirija ya mafisadi hasa eneo la bandarini. Alipambana sana. Alinifurahisha sana. Hasa zile ziara za kustukiza pale bandarini,zimeleta mabadiriko makubwa sana pale bandarini.
Yapo mengi lakini hayo ndio nimeyaona.
Buriani mheshimiwa Rais Maghufuli. Tutakukumbuka kwa mabadiriko makubwa