Leo Machi 17, 2023 imetimia miaka miwili tangu alipofariki Rais wa Awamu ya Tano, Dkt. John Pombe Magufuli.

Dkt. Magufuli alifariki wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mzena, Dar es Salaam.


 
1. Siasa zisizo za chuki
2. Kutokuwa m'kabila.
3. Uwazi na ukweli.
4.
 
Kama ufisadi ulifanyika chini yake na yeye hakukemea hizo tabia chafu basi tutamuita fisadi pia.

Unyama wa kina Sabaya alikiri kuwa alikuwa anayafanya yote kwa kutumwa na mteule wake.

Wewe hapo unaanzaje kumtetea huyo mtu?
Nimesema ana mabaya yake lakini sio ufisadi.
Hapana .

Kwa fedha za ndani na Mikopo ya kinenki yenye masharti ya kibiashara Mtu asiye mwadilifu asingeweza kufanya aliyoyafanya hata Kwa miaka 30.
Acheni utani kabisa.

Hata kipofu anaona.

Fedha zimehamishwa Magufuli alipoanza kuugua na walikua wameplan mpango huo wakaona umetiki . Wakaanza kuhamisha fedha akiwa ameshaanza kuumwa.

Magufuli akiwa mzima hakuna hata mia wangeweza kuzihamisha .

Alizuia pesa kuingia na kutoka kinyemela.

Sabaya ni mhuni kama wahuni wengine.
JPM adui yake mkubwa alikua ni ufisadi kwa hiyo maeneo yaliyokuwa na wezi na wakwepa Kodi kama Arusha na Kilimanjaro, Mwanza ,Dar es salaam n.k hao Kwa kweli akiwawekea vizuizi vya kufa mtu. Hao hata kukunyofoa nyongo wangekunyofoa alimradi unyooke .
Hivi mkoa wa Arusha wewe unauna ni mkoa wenye binadamu wanaojali utu mbele ya pesa. Arusha hata Mwanamke mbele ya pesa ni mnyama kuliko chatu.

Acheni mambo yameshapita lakini kuna watu kwanza aliwachelewesha walitakiwa wawe wameshafagiliwa wakaisha. Bado alikua na huruma sana Arusha ni mkoa wenye watu wanyama sana na wanaofanya biashara za unyama sana. Matajiri Arusha walikua wanawindana kama wanyama . Kila mmoja alikua anawaza kumaliza mwenzake ili atajirike .

Rushwa Arusha ni kubwa sana kila mahali , ni mkoa usia na kitu haki ya mnyonge.

Hata Mrema alipokuwa Waziri wa mambo ya ndani aliwahi kuutuliza Mji wa Arusha Kwa mtutu wa Bunduki . Arusha bila chuma huwezi kuwacontrol wafanyabiashara wale wanyama kuliko koboko.
 
Mbona Sabaya alikiri kabisa kuwa maovu aliyokuwa anafanya alitumwa na Jiwe?
 
Mbona Sabaya alikiri kabisa kuwa maovu aliyokuwa anafanya alitumwa na Jiwe?
Sasa ulitegemea asemeje wakati JPM ameshakufa . ?
Hata ungekua wewe ungesema hivyo kujitoa hatiani.

Hivi JPM anaweza akamtuma Sabaya akafire mtu au amwingizie mtu chupa matakoni. Au apore mke wa mtu.

Hapana Sabaya alikua ni mnyama TU.

Hawa Vijana wa CCM linapokuja suala la sifa na madaraka hua ni wanyama sana.
Ulimuona mtoto wa Waziri Simbachawene akimtukana Polisi mwenye umri sawa na baba yake ? Kile ni kiburi Cha pesa sio kwamba alitumwa . Vijana wanaopata pesa za kuteuliwa na kuwa na madaraka makubwa Juu ya watu mara nyingi wanakua na kiburi kupitiliza . MTU kama Mo huwezi ukamuona akimtukana Hata mgambo.

Tutofutishe watendaji waliojipatia fedha Kutokana na kuugua Kwa JPM na uadilifu wake.

Ukitaka Ujue SERIKALI Corrupt kwenye unaangalia kwenye wizara zifuatazo:-
Wizara ya fedha ,
Nishati na Madini,
Maliasili ,
Ujenzi.
Dunia nzima hizo ndizo wizara zenye watendaji wenye Kashfa KUBWA za mabilioni. JPM hakuwavumilia kwenye wizara hizo.

Na kama ni Wizi angetumia Mali asili Sio pesa za Plea bargain. Ambazo kimsingi aliyepewa mamlaka ya kubagain ni DPP ambaye angeweza kubagain na kupewa rushwa Ili afute kesi Kwa pesa kidogo na asingethubutu kumshirikisha JPM.

Mimi sijawahi Kumuunga mkono alipokuwa hai kutokana na kuminya Demokrasia tuu lakini mambo mengine nilikua namsikilizia kwanza anavyofanikisha mikakati yake Kwa haraka .
Kwa Sasa nimemsamehe madhaifu yake yote na Mungu ampe makao mema Huko Peponi . Amina .
Kuna maeneo nilimponda sana Lakini Kwa Sasa haiwezi kujitokeza na kujisemea siwezi kumlaumu kwenye Yale yasiyo na Majibu ya Haki na yaliyotendeka na wengine kama Sabaya. Wawajibike wenyewe
 
Jiwe hakuwa muadilifu kabisaufisadi mwingi sana 1.5 trillion
 
Jiwe hakuwa muadilifu kabisaufisadi mwingi sana 1.5 trillion
Hapana.

Fedha zilitoroshwa wakati alipokuwa Mgonjwa.

Ameugua muda Mrefu.

Hata alipokufa watu walikomba pesa benki kuu.


Ni kwaida Kwa nchi zisizo na mfumo mzuri au zenye mfumo Wa kupeteuliwa na MTU mmoja.

Ndio Maana mara zote Rais akistaafu wanakomba pesa zote benki kuu.

Ili ukweli ubainike ni lazima Kija chama kingine Ili CCM ijipambanue yenyewe.

Watu wanaiba na kumwekea mzigo marehemu. Sio Sawa.

JPM hajawahi kuiba FEDHA za umma Kwa sababu muda WOTE alilikua anatafuta pesa za Miradi Sio za kuweka Kwa wachina . Hakutaka Hata Madini yaende Kwao kinyemela sembuse pesa.
Tutakua tunapata dhambi kubwa sana kumsingizia MTU aliyefanya mambo ambayo yasingefanyika Hata Miaka 30 ijayo.
 
Wakati wa utawala wako hatukuzoea kuona umeme ukikatika kila siku, lakini sasa ni ovyo kabisa.

Wakati wa utawala wako hatukuzoea kuona bei za vitu zikipanda kila siku, lakini sasa ni ovyo kabisa.

Wakati wa utawala wako hatukuzoea kuona vitendo vya rushwa vikishamiri, lakini sasa ni ovyo kabisa.

Wakati wa utawala wako hatukuzoea kuona vibaka wakitapakaa mitaani, lakini sasa ni ovyo kabisa.

Wakati wa utawala wako hatukuzoea kuona uzembe katika kazi za umma, lakini sasa ni ovyo kabisa.

Wakati wa utawala wako hatukuzoea kuona Tanzania ikiwa shamba la Bibi, lakini sasa ni ovyo kabisa.

Ahsante sana mpendwa wetu, JPM. Ulipigana kiume, mwendo umeumaliza, pumzika kwa AMANI, Baba yetu JPM. Amina.
 
Kichwa cha habar kinajieleza

Km ilivyo ada ya sis waswahili mara zote huwa tunasisitiziana kuwa marhum huwa anatajwa kwa mazur yake ila mabaya tunamuachia muumba kwa sabab yey ndie anajua yakin ya mtu km alishatubia au laa.

Lengo la uzi huu ni kumkumbuka msukuma mmoja hv wakuitwa Pombe Magufur akiwa anatimiza miaka miwil tangu roho iache mwili.

Binafs namkumbuka mno pale alipogoma kutuwekea kifungo cha nyumban wakat coronavirus imechachamaa huku Bint Mwalimu kila uchwao akitutangazia idad ya wagonjwa wanaoongezeka kutokana na virus vya corona

Je ww unamkumbuka kwa jambo gani???
Sent from my Infinix X6816 using JamiiForums mobile app
View attachment 2555843
 
Yoshua bin Sira.38:16-23
16Mwanangu, mlilie mtu aliyekufa;
lia kwa uchungu, kuonesha huzuni yako.
Uuzike mwili wake kwa heshima ipasavyo,
wala usipuuze mazishi yake.
17Lia kwa uchungu na kwa moyo,
hudhuria matanga kama anavyostahili marehemu,
omboleza siku mbili tatu usije ukasemwa;
kisha ufarijike kutokana na huzuni yako.
18Maana huzuni huweza kusababisha kifo,
na huzuni ya moyo hunyonya nguvu za mtu.
19Mtu akiondolewa duniani huzuni imekwisha,
lakini maisha ya maskini, huulemesha moyo.
20Usiruhusu moyo wako kutawaliwa na huzuni;
ifukuze huzuni, ukifikiria mwisho wako.
21Usisahau kwamba hakuna kurudi nyuma,
humsaidii marehemu chochote na unajidhuru mwenyewe.
22Kumbuka, utakufa kama alivyokufa,
jana yeye, kesho wewe.
23Marehemu anapowekwa kupumzika kaburini,
nako kumkumbuka kuachwe;
nawe usiendelee kumlilia roho yake ikisha ondoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…