Habari za uzima waungwana wenzangu?, Amani ya bwana iwe nasi ktk kpnd hiki kigumu cha maombolezo ya msiba wa muungwana mwenzetu, aliekua kiongozi muungwana wa nchi yetu mh. Hayati JJP MAGUFULI.
Unapotaka kuuelezea ufanisi au kinyume chake utendaji wa iliokua serikali chini ya Mh Rais Hayati Dk John joseph POMBE MAGUFULI ni vizuri ukajikita kwa yale u
liokutendea uongozi wake ww binafsi au jamii yako na si vinginevyo.
Naamini uongozi huo ilikua ngumu kuutabiri kwamba alielia leo atalia milele au kesho atacheka? Na aliecheka leo atacheka milele au kesho atalia?
Mzee Magufuli anakua SIMBA ASIEFUGIKA ki-hisia wala ki-tabaka fulani kwa kua ktk utendaji wake kila tabaka lilia na kila tabaka lilicheka. kuna masikini/WANYONGE walicheka lkn pia kuna WANYONGE/masikin walilia, dini zote zilicheka na dini zote zililia pia, kwenye siasa kuna wapinzani walilia lkn pia kuna wapinzani walicheka, hata Ndani ya chama chake ccm wapo waliolia na wapo walicheka, Matajiri wapo waliolia na kufiliska ktk uongozi huu, lkn pia wapo walionifaika na kutoboa zaidi ktk uongozi wake na huezi kuwaambia kitu ktk uongozi wa mzee Magufuli,uksema ukabila kuna walio toka kanda ya ziwa walifurahia Sana uongozi huu lkn pia wapo waliokasirishwa Sana na uongozi huu.
Ni hivyo hivyo ktk maeneo mengine, huezisema eti mzee Magufuli alifugwa ki-hisia/ki-tabaka fulani hapana aligusa nyanja zote kama zilivyo pata utamu ndivyo zilivyoonja machungu pia, na uktaka kumsema sema kwa upande wako uongozi huu ulikutenda vp? Kama uliwajbshwa pia utuambie kbs uliwajbshwa kwa mapungufu yko au ulionewa na mungu wako anatosha kia shahid, maana wote wanaolalamika,wanalalamikia mapungufu ya utendaji kazi wa serikali ya mzee Magufuli tu, wanajaribu kutuaminisha kua walionewa ila wao wako perfect.
Mzee Magufuli hakua mwehu wakuvamia watu hovyo na kuwawajibsha bila kuchokozwa au kufuata sheria, so waliojchanganya walishughurikiwa kwelikweli na waliomuheshim pia walinufaika kwelikweli,
Niseme tu akiwa binadam kama mimi na wewe pia mzee Magufuli hakua mkamilifu [emoji817] anamapungufu yake!
Yapo mengi Sana ya kumuongelea mzee Magufuli kwa utamu/uchungu inategemea ulikua upande gn, lkn itoshe tu kusema wale ambao waliguswa vibaya na utawala wake (ambao ni wachache)kwa makusudi au labda kwa mapungufu yake kama binadam, turejee vitabu vyetu vya dini ambavyo vinatuelekeza kusamehe ili na sisi tusamewe, tusilaum ili na sisi tusije tukalaumiwa.
ASSALAM ALAYKUM