christeve88
JF-Expert Member
- Aug 11, 2018
- 2,841
- 4,531
Rais Magufuli hakubagua upinziani, alipenda upinzani wenye dira ya mendeleo sio upinzani wa kukosoa kosoa na kukejeli kila kitu. Magufuli alikuwa mtu smart ndio maana wale wapinzani smart almost wote aliwachukua akawaingiza serikalini. Wapinzani wa nchi hii wengi walipoteza dira kipindi cha utawala wa Magufuli sababu iko wazi tu, Magufuli alideal na makundi ambayo ndiyo yanaupa nguvu upinzani ikiwa yataachwa bila kutatuliwa kero zao, mfano machinga, bodaboda mama lishe nk. Agenda muhimu kam kupambana na ufisadi nazo zilimpa credit, ndio sababu wapinzani wazalendo walihama wakabaki wale wenye maslahi toka nje na wachache wazalendo walibaki.Kuna clip moja ambayo vyombo vya habari wanairudia rudia mara kwa mara.
Clip yenyewe ni moja ya hotuba ambazo hayati Magufuli alizitoa wakati wa uhai wake.
Maneno yanayosemwa kwenye clip hiyo ndiyo ambayo ni mada yangu kuu, kwenye uzi wangu huu.
Anatamka kuwa "Mtanikumbuka kwa mema wala si kwa mabaya yangu, nawasihi tusibaguane kwa vyama vyetu vya siasa, wala ukabila na udini na kamwe tusiache kumwabudu Mungu wetu" mwisho wa kunukuu.
Kwa maelezo hayo na namna alivyokuwa akiiendesha nchi hii vina umbali kama kutoka mbinguni hadi duniani!
Hebu turudie baadhi ya matamshi yake wakati akiwa hai.
Mkinichagulia mpinzani mtakuwa mnajichelewesha wenyewe maendeleo yenu!
Nyinyi wenyewe ndiyo mlifanya makosa safari iliyopita kwa kuchagua mbunge wa upinzani, safari hii msirudie kosa hilo!
Kaskazini (hususani mkoa wa Kilimanjaro) mlipendelewa sana katika awamu zilizopita, hivi sasa na nyinyi subirini, wakati maendeleo ninapopeleka kwingineko(akimaanisha mikoa ya kanda ya ziwa)
Wakati akiyatamka maneno hayo, alijua fika kuwa nchi yetu toka tupate Uhuru, imejengwa katika misingi ya umoja wa kitaifa, ambayo hatubaguani kwa vyama vya siasa, ukabila wala dini zetu, kwa maana nyingine ni yeye aliyetaka kuligawa Taifa hili.
Vile vile akifahamu kuwa tokea mwaka 1992, nchi yetu iliandika ndani ya Katiba ya nchi kuwa nchi yetu itakuwa ya mfumo Wa vyama vingi, jambo ambalo hayati Magufuli, alionekana wazi wakati Wa uhai wake kuwa anauchukia mfumo huo na alikuwa akitamani nchi yetu irejee kwenye mfumo wa chama kimoja!
Lakini haishangazi kwa hayati Magufuli kutamka maneno hayo, kwa kuwa tunajua fika kuwa alkkuwa ni mtu wa "double standards"
Anatamka Leo kuwa maendeleo hayana chama, wakati kesho yake anawaambia wapiga kura kuwa msinichagulie betri na gunzi!
Kuna wapinzani wanadhani kuwa baada ya Magufuli kufariki upinzani utakuwa haraka, wanasahau kuwa upinzani wa kweli unatoka kwa wananchi na sio kwa wanasiasa, wanasiasa wao husimamia zile hoja za wananchi hasa wale wanyonge. Image ya upinzani wa Tanzania hasa CHADEMA inaharibika kwa kasi kwa kuwa wameanua kuhushi kiharakati zaidi kuliko kama chama kikukuu cha upinzani. Mtu mmoja anaweza kuharibu image ya chama halafu wote mkaonekana sio wazalendo au hampendi maendeleo ya nchi. Upinzani unabidi uwe option B au chaguo la pila kwa walioko chama tawala, sasa tujiulize ni rahisi kwa mwanasiasa wa sasa wa ccm kuhamia chadema kama ilivyokuwa ? na kama sivyo basi kutakuwa na shida fulani. Zamani ilikuwa ni fahari kuwa chadema ila kwa sasa ukiwa huko unajihisi sio mzalendo kutoka na mrengo wa baadhi ya watu ndani ya chama.