Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?
Tanzania ingekuwa mbali kiuchumi,Treni ya SGR ingekuwa imefika Mwanza,Selikari yote ingekuwa imehamia Dodoma, Magereza yangekuwa yamejaa wahujumu uchumi,rushwa ingekuwa imekwisha kabisa,wanyonge ndiyo wangekuwa wanaongoza inchi,
Ongezea na ya kwako,,,,
Rushwa isingeweza kuisha. Alifanya mengi mazuri lakini naye alikuwa ana watu wake ambao walikuwa wanapga deal bila kuguswa.
Mfano makonda alianza kamata pesa sana akiwa rc wa mkoa wakati mshahara wa rc unajulikana asingeweza kumiliki magari na mali alizokuwa nazo, same to sabaya, dpp akawa na tuhuma za kupiga pesa kwa anaoingia nao prebargain.
Ilikuwa anaondoa wapigaji wa utawala fulani anatengeneza wa utawapa mpya.
Aliwaondoa wakina rugumi akatengeneza wengine sasa wamejirudia kwenye anga zao.
 
Huyo ambaye Zitto Kabwe alimwita kuwa ni mshamba ndio unasema alikuwa bingwa wa propaganda kiasi cha kuwazidi wajanja kwa wananchi kumuamini yeye badala ya kuwaamini watoto wa mjini?
Wewe propaganda zako zitafika wapi ilhali alieshika vyombo vya habari mpaka mitandao ni yeye.

Ukimsema vibaya kesho haupo, utake utaeneza propaganda zake usitake basi kaa kimya kwa muda ili usije kalishwa kimya milele.
 
Tanzania ingekuwa mbali kiuchumi,Treni ya SGR ingekuwa imefika Mwanza,Selikari yote ingekuwa imehamia Dodoma, Magereza yangekuwa yamejaa wahujumu uchumi,rushwa ingekuwa imekwisha kabisa,wanyonge ndiyo wangekuwa wanaongoza inchi,
Ongezea na ya kwako,,,,
Watu wengi wangekuwa wamepotea, ila kali zaidi ulilosema ni nchi kuongozwa na wanyonge 🤔🤔
Propaganda zake zilikua hatari sana. Hivi hao wanyonge aliwatoa kwenye unyonge wao aliwatumia tu mtaji wake wa kisiasa
 
Prons
Kwenye miundo mbinu kama barabara, reli, umeme wa uhakika, usambazaji wa Maji kama inchi ingekua imepiga hatua

Cons
ufinyu wa demokrasia, ufinyu wa ajira, ukandamizwaji kwa watu wenye mawazo na fikra kinzani.
 
Tanzania ingekuwa mbali kiuchumi,Treni ya SGR ingekuwa imefika Mwanza,Selikari yote ingekuwa imehamia Dodoma, Magereza yangekuwa yamejaa wahujumu uchumi,rushwa ingekuwa imekwisha kabisa,wanyonge ndiyo wangekuwa wanaongoza inchi,
Ongezea na ya kwako,,,,
General Mbuge angekuwa Mkuu wa Majeshi
 
Huduma za kijamii zingekua bora zaidi ya sasa
Sipingi kuwa Maza haupigi mwingi anajitahidi kwakweli
 
Wewe propaganda zako zitafika wapi ilhali alieshika vyombo vya habari mpaka mitandao ni yeye.

Ukimsema vibaya kesho haupo, utake utaeneza propaganda zake usitake basi kaa kimya kwa muda ili usije kalishwa kimya milele.
Mbona mitandaoni alikuwa anakosolewa kama humu JF yameelezwa mengi tu ya kumkosoa wakati akiwa bado hai, labda kumkosoa hadharani kitu ambacho hatuna utamaduni huo na ndio maana hata sasa hakuna ukosoaji wa aina hiyo.
 
Mbona mitandaoni alikuwa anakosolewa kama humu JF yameelezwa mengi tu ya kumkosoa wakati akiwa bado hai, labda kumkosoa hadharani kitu ambacho hatuna utamaduni huo na ndio maana hata sasa hakuna ukosoaji wa aina hiyo.
Kwamba kina Roma, Lissu na Lema walikua wanakosoa wakiwa jf sio??

Hao wote walikula kona baada ya uhai wao kuwekwa rehani kisa ukosoaji, alietia neno kuhusu elimu yake mpaka leo hajulikani alipo.

Haukua uhuru bali uoga, sasa hivi uoga bado upo ila makali ya adhabu kidogo yamepungua na sio ya waziwazi.
 
Wasalaam
Ukiangalia na kusikiliza hyo video utagundua tunaongozwa na viongozi wa aina gani, tumepotezwa na tunaenda shimoni.

 
1739389078189.jpg
 
Kwamba kina Roma, Lissu na Lema walikua wanakosoa wakiwa jf sio??

Hao wote walikula kona baada ya uhai wao kuwekwa rehani kisa ukosoaji, alietia neno kuhusu elimu yake mpaka leo hajulikani alipo.

Haukua uhuru bali uoga, sasa hivi uoga bado upo ila makali ya adhabu kidogo yamepungua na sio ya waziwazi.
Kwahiyo mkuu unataka kusema maovu ya Jiwe yamekuja kuongelewa baada ya yeye kufariki?
 
Barabara na miundombinu yenye kiwango cha juu. Mikocheni yote.ingekuwa na.lami.saa hii
 
Kwahiyo mkuu unataka kusema maovu ya Jiwe yamekuja kuongelewa baada ya yeye kufariki?
Mengi yameongelewa baada ya yeye kudanja hata hivyo wengi hawajari maana kilichopo kinawanufaisha, na Jiwe alikua sehemu ya system sio rahisi kumtuhumu kwa mengi utacompromise system nzima.

Si waona yule mmiliki wa star tv nae alitoa nyongo baada ya Jiwe kudanja, yule kijana nae akakimbilia ughaibuni akatoa jitabu baada ya jiwe kudanja.
Japo bado huwezi muongelea vibaya vibaya Jiwe mpaka sasa maana bado prezidaa aliyepo ni zao lake.
 
Trump kapiga pini bila watu kujiandaa.

Ulaya nayo na Japani wanaenda kupita mulemule bila watu kujiandaa .

Watu wameshitukizwa !!.
🔴CCM Ilikuwa na Dhamira Njema, Lakini Wana CCM Wameisaliti

CCM ilipozaliwa mwaka 1977, tuliikusanya kutoka kwa TANU na ASP, tukisema hiki ni chama cha wakulima na wafanyakazi! Hii haikuwa maneno matupu. Ilikuwa imani. Ilikuwa dhamira. Tuliweka msingi wa ujamaa na kujitegemea tukiamini kuwa taifa letu halitaachia rasilimali zake zichezewe na wachache. Tukasema kwamba serikali ya chama lazima ihakikishe uchumi unamnufaisha kila Mtanzania, si wachache wenye nguvu ya fedha!

Lakini leo, naona CCM inaishi kwa jina tu. Wanaosema ni chama cha wakulima na wafanyakazi ni wao kwa maneno, lakini kwa vitendo, chama kimekuwa cha wachache wenye fedha na ushawishi wa kisiasa. Wamekiuka misingi yao wenyewe.

🔴Katiba ya CCM Inasemaje, na CCM Inafanya Nini?

Katika Ibara ya 9 ya Katiba ya CCM, chama kiliahidi kusimamia ujamaa na kujitegemea, kuhakikisha kuwa rasilimali za nchi zinawanufaisha wananchi wote. Tukasema taifa hili lazima lijitegemee kwa kilimo chake, viwanda vyake, na kazi za wananchi wake.

Lakini leo, watu wale wale waliokabidhiwa chama wamekiuka ahadi zao wenyewe:

Madini yanachimbwa na wageni, wenyeji wanabaki watazamaji.

Mashamba yanaota magugu, wakulima hawana pembejeo, hawana masoko.

Mashirika ya umma yameuzwa kwa bei ya kutupwa, halafu serikali inarudi kuyakomboa kwa gharama kubwa!

Ajira kwa wafanyakazi imekuwa ndoto. Vijana wanahangaika huku nchi ikikumbatia wawekezaji wa kigeni badala ya kuwaendeleza wazawa!

Ndugu zangu, hii siyo CCM tuliyoianzisha. Hii ni CCM ya matumbo ya watu wachache!

🔴Ubinadamu na Ubinafsi: CCM ya Leo Imeongozwa na Tamaa

Kuna tofauti kati ya ubinadamu na ubinafsi. Binadamu anatakiwa kujali wenzake, kuhakikisha kila mmoja anapata haki yake. Lakini ubinafsi ni sumu inayowafanya wachache wale, wengi wabaki na njaa. Leo CCM haiongozwi tena na utu. Inaongozwa na tamaa ya mali na madaraka.

Ujamaa haukuwa mzigo. Ujamaa ulikuwa njia ya kuhakikisha kila Mtanzania anafaidika na rasilimali za nchi yake. Lakini sasa, sera za uchumi zimegeuzwa kuwa biashara za wachache. Serikali inashindwa kusimamia rasilimali kwa sababu waliopo madarakani hawajali tena misingi ya chama. Wamekaa meza moja na wenye fedha, wamesahau maskini waliowapa uongozi.

🔴Wanachama wa CCM Wamegeuka Mashabiki Badala ya Wasimamizi

CCM ingekuwa na nguvu kama wanachama wake wangekuwa waangalizi wa nidhamu ya viongozi wao. Lakini leo, wanachama wa CCM siyo tena walinzi wa rasilimali, wamekuwa mashabiki wa viongozi wabovu!

Wanaimba majina ya viongozi badala ya kuwauliza wanatekeleza vipi misingi ya chama.

Wanapiga makofi kwa wale wanaovunja katiba yao wenyewe.

Wanapigia kura wale wanaouza nchi badala ya wale wanaoijenga.

Chama chenye wanachama wa aina hii hakina uhai. Kimebakia kama nembo tu, kama bendera inayopepea kwa upepo wa fedha na siyo upepo wa uzalendo.

🔴Je, CCM Bado ni Chama cha Wakulima na Wafanyakazi?

Leo, mtu akiniuliza je, CCM bado ni chama cha wakulima na wafanyakazi? Ningemuuliza:

Mkulima yuko wapi katika mipango ya CCM?

Mfanyakazi anafaidika vipi na rasilimali za taifa?

Kwa nini mikataba ya madini, gesi, na mafuta haijawahi kuwekwa wazi kwa wananchi?

Kwa nini serikali inalia kuhusu ajira lakini haina mpango wa kuhakikisha viwanda vya ndani vinaajiri watu?

CCM imekwepa maswali haya kwa sababu haina majibu.

🔴Hitimisho: CCM Lazima Iamke au Isambaratike

Nitasema kama Mwalimu: CCM inatakiwa kurejea kwenye misingi yake. Ikiwa wanachama wake hawataamka na kudai chama chao kirejee kwenye misingi ya ujamaa, basi chama kitakuwa hakina maana tena.

CCM siyo vibanda vya biashara vya wachache. CCM siyo jukwaa la matajiri wachache kujilimbikizia mali. CCM ni chama cha wananchi! Lakini kama hakiwezi tena kuwalinda wakulima na wafanyakazi, basi CCM itakuwa historia tu, kama majina ya vyama vilivyopotea duniani.

Wanachama wa CCM, amka sasa! Chagua viongozi waadilifu. Wawajibishe wale wanaouza nchi. Rudisheni chama kwenye misingi yake. Laiti ninyi mngekuwa walinzi wa rasilimali zenu, taifa hili lingekuwa mahali pa neema kwa wote.

Julius Kambarage Nyerere, akisema kwa sauti ya uzalendo kutoka moyoni!

🇹🇿Asante kwa kuwa sehemu ya safari hii ya tafakari na maarifa! Falsafa ni mwanga wa akili na dira ya maisha--Usiruhusu giza la kutokujua likuzuie kuona upeo mpana wa fikra. Endelea kufuatilia ukurasa huu, kwani kila wazo jipya ni hatua kuelekea hekima. Tafakari, hoji na usiache kufikiri.🇰🇪

Follow
 
Bado Serikali ya CCm Inatambua umuhimu wa kujitegemea.
Hakuna chama kingine chenye Sera hii ...wengine wote ni vibaraka wa mabwanyenye waliopo kuhatarisha Ustawi wa Sera ya ujamaa na kujitegemea
 
Back
Top Bottom