Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?
Mgao mbona upo tu ni vile Tanesco walupigwa marufuku kutangaza.Nenda kwenye special uzi wa Tanesco uone malalamiko bado yako palepale tu
Alijitahidi kwenye suala la umeme,mgawo haukuwa kivile kama utawala uliyomtangulia!

Ova
 
Hawa watu walikuwa makundi 3:

1. Waliokuwa wakila mkate kwa kazi ya kusifia
2. Waliokuwa wakiwinda mkate
3. Waliokuwa wakifuata mkumbo na wale waliokosa habari za undani na za ukweli

Makundi mawili hapo juu kazi yao imeisha na sasa wanahamishia majamvi kwa Mh. Samia Suluhu ili adhma yao itimie au iendelee kutimia.

Hili kundi la tatu hili linaanza kufunguka baada ya kuanza kupata habari sahihi na za undani.

Media sasa kidogo zinafunguka.

Mpaka 2022 Magufuli hatasifiwa na kundi lolote.
 
Mgao wa umeme umeendelea pia katika utawala wa Magufuli tofauti pekee ilikuwa ni lugha tu iliyotumika. Siku za nyuma mgao ulikuwa ukitangazwa rasmi na kila mtu alijua tupo kwenye mgao lakini kipindi cha Magufuli hatukuwahi kuambiwa rasmi kuwa na mgao lakini kukatika kwa umeme muda mrefu kulikuwepo na maelezo ya Tanesco yalikuwa yapo kipropaganda sana.
 
Alijitahidi kwenye suala la umeme,mgawo haukuwa kivile kama utawala uliyomtangulia!

Ova
Sawa lakini haukuisha.Mi.ungesema maji sawa kajitahidi sana.Ingawa sii watanzania wote wenye maji safi.na salama
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Alijitahidi kwenye suala la umeme,mgawo haukuwa kivile kama utawala uliyomtangulia!


Ova
 
Wacha magazeti ya Mwanahalisi yafunguliwe utaona kitakachotokea. Ufisadi aliopiga kupitia kampuni yake ya construction utakaa wazi wote na jamaa Wana hasira sana maana walinyamazishwa kwa hila.
 
Ukweli mchungu, nilikuwa mkosoaji mkubwa wa baadhi ya sera za Magufuli lakini kuna mengi aliyafanya. Nami kama binadamu siwezi kusema mabaya yake kwa sasa bali mema aliyotutendea. Miaka ya 2015 kurudi nyuma ulikuwa unaingia hapo k/koo ni kelele za majenereta tu kisa mgao wa umeme. Lakini kwa miaka 6 tu ya utawala wake yote tulisahau. Watanzania tutapigwa pigo kubwa sana kama tusipoona mazuri haya.
Madawa ya kulevya kupotea, semina zisizo na akili, safari zisizo na tija, mishahara kwa wakati, nidhamu kazini, heshima kwa wote, majambazi kupungua, hadithi za kuteka magari kuisha, wanawake kulala chini, vifaa tiba kuwepo mpaka vile ambavyo hatujui kuvitumia etc

Haya yoote hawayaoni, wanaona tu pesa zilizopigwa na wapambe nuksi ambao alikuwa anawatumbua kila leo bila huruma...
 
Mobutu alitangaza offer ya kuwapeleka Ufaransa wasichana bikra. Watoto wa masikini kusikia offer ya kusoma Ufaransa walijitokeza kwa wingi. Mobutu aliwaambia kuna treat ya kutembea mto Kongo kwa boat.
Kumbe mganga wake alimwambia anahitaji kafara la mabinti bikra. Alizamisha boat na mabinti wote walifariki.
 
Tafsiri ya WANYONGE kwenye kichapisho chako lina maana sawa na WASHAMBA
 
Acha uongo .mgao wa umeme ulipungua baada ya miradi ya kinyerezi 1 na 2 kukamilika na ilikuwa ni miradi aliyoianzisha Kikwete.
 
Kwa kuwanyonga wanyonge, mauaji ya akina ben saa8, azory, kangoye na kushadadia waliouwawa kibiti na kutupwa baharini na Kwa wizi ule wa kura alidhani angeishi milele.

Jizi kama nini la ela kt akaunt za watu, tena tunaomba moto wa milele uanze kulichomea kabulini na lifufuliwe likiwa na pingu mikononi.

Hakika hakuna Rais aliyegusa maisha ya Watanzania wengi kama Magufuli.
 
wanasiasa wote waendelee kucheza na akili za wanyonge lakini waelewe vizuri kuwa hakuna nguvu ya kuutenganisha utu na upendo wa Magufuli na wananchi wanyonge wa Tanzania.
IMG-20210412-WA0044.jpg
 
Back
Top Bottom