Nashangaa sana kusikia wafuasi na wapinzani wa Ccm kushadidia upuuzi usio na maana kuwa Legacy ambayo watu wanatakiwa kuachwa nayo ni kujenga miundo mbinu, shule na huduma za afya.

Ni kweli ili kiongozi makini ukubalike lazima taifa lako liwe na miundo mbinu mizuri, huduma za afya na elimu nzuri.

Lakini je mbona mnasahau kuwa lazima kiongozi atengeneze hali na utashi wa raia kupinga ufisadi na rushwa?

JPM aliweza kujenga hiyo hali ndani ya mioyo ya watanzania. Ni Legacy kuu aliyoiacha hapa Tanzania.
 
Legacy pekee itakayokumbukwa kwa muda mrefu ni ile kutembea na fedha za umma katika misafara yake na kuzigawa kwa malofa ili aweze kutafuta kiki.
 
Kwani aliyekuambia ataka ufisadi ni nani? Je wewe binafsi ulishanusa ufisadi kwenye haki za msingi za watanzania ikiwa ni pamoja na zile za kikatiba? Au mpaka tufanyeje nini ili uelewe mambo hayakuwa sawa, Hadi awamu ya sita inafanya kazi kubwa kurejesha hali sawa. Au shida ni kukwamia awamu iliyopita, au ulikuwa mnufaika wa mfumo wa awamu husika.
 
Tutamkumbuka kwa kumtuma Sabaya jimbo la Hai kwenda kulawiti wananchi kisa ni jimbo la upinzani.Magufuli was a hopeless sinner who died for a good reason.
 
Kitu Hayati John amenifanya niweze kumuweka kweny kumbukumbu zangu ni kitendo cha kuwezesha
1. umeme vijijini hivyo kutengeneza fursa nying zaid kwa wanainch
2. Elimu bure kwa kuwezesha watoto wengi kupata elimu bila malipo
3. Nizamu makazini kwa namna ambavyo watumishi waliacha kufanya Kazi kwa mazoez
4. Udhubutu wa kuanzisha miladi mikubwa ya kimkakati ambayo ilikuwa na dira ya kukuza uchumi wa taifa na wa mtu mmoja mmoja(SGR & uzalishaji umeme bwawa la rufiji)
 
Nitamkumbuka kwa uteuzi wake wa viongozi wa hovyo kama Sabaya na Makonda.

Nitamkumbuka kwa ukaidi wake na dharau dhidi ya viongozi wa dini waliomkosoa.
 

Nianze kwa kusema kuwa mimi sio mwana CCM wala CHADEMA. Mimi huwa napenda uongozi mzuri na kiongozi mzuri na sio chama alichotokea. Hayati Dr. Magufuli alifanya mambo mengi sana na aliumiza wengi kwa ajili ya public interests na huu ndio ukweli haijalishi watu wakapinga.

Toka afariki, na usukani kukamatwa na Mheshimiwa Mama Samia kuna mambo mengi yametokea ambayo kwa wengi hasahasa sie wapenda haki yanatupa Faraja sana. Vivyo, hivyo kuna mabadiliko ambayo kimsingi yatatufanya tumkumbuke hayati Magufuli tu.

Mwenzenu baada ya kuhitimu sijabahatika kuajiliwa sasa nina miaka 2 mtaani. Alhamudulillah, nimefungua saloon ya kunyoa na pia nina duka la vinywaji baridi hapa mtaani kwetu.

Kinachonifanya nimkumbuke John Pombe Magufuli ni swala la umeme shughuli zangu zimesimama kwa sababu ya umeme. Kwaa siku umeme unakata hovyo hovyo bila sababu za msingi. Na taarifa haitolewi.

Tangu Jtatu, mfumo wa kununua umeme mtandaoni haufanyikazi, LUKU imeisha tangu jana saa 7 alasiri mpaka sasa mfumo unasumbua, wafanyakazi wangu (Kinyozi na muuza duka) siwalipi posho maana hakuna kazi bila umeme.

Kipindi cha mwendazake, kabla ya umeme kukata tulikuwa tunapewa taarifa, na haikuchukua muda, unarudi. Mfumo wa ununuaji wa LUKU ulisumbua kwa dakika chache tu.

Kwani Mama Samia si ulikuwa msaidizi wa rais John Pombe Magufuli, hakukuachia mbinu za kukomesha janjajanja za wafanyakazi TANESCO? Kama unaona waziri hafai tumbua weka mwingine. Tumia nguvu. Waafrika wengi bado ni washenzi sio wa kuwadekeza na kuwabeba mgongoni kwa mbeleko ya demokrasia na protoko.

Ni hayo tu jamani, nimeanza kumkumbuka John Pombe Magufuli.

UPDATE:

Jamani ili uelewe nilichoandika, weka hisia pembeni, tumia akili!

Sijasema kipindi cha JPM umeme haukukatika.
 
Hivi kipindi cha Magufuli umeme si kuna kipindi ulikuwa unakatika nchi nzima hadi watu wakaanza kuhisi kuna mgao wa kimya kimya?

Nakumbuka ilikuwa mwezi Februari mwaka huu hadi watu wakaanza kuhoji hiyo reli ya SGR itatengenezwaje

Hebu soma nyuzi hizi za kipindi cha JPM watu wakilalamikia mgao wa umeme wa kimya kimya




 
Hayati Dr. Magufuli alifanya mambo mengi sana na aliumiza wengi kwa ajili ya public interests na huu ndio ukweli haijalishi watu wakapinga.
Kuvuruga uchaguzi mkuu uliopita ilikuwa ni kwa public interest?

Kununua viongozi wa upinzani ilikuwa ni kwa public interest?

Kumtwaga marisasi yote lissu ilikuwa ni kwa public interest?

Kufungia account za watu na kuwapora fedha zao ilikuwa ni kwa public interest?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…