Nianze kwa kusema kuwa mimi sio mwana CCM wala CHADEMA. Mimi huwa napenda uongozi mzuri na kiongozi mzuri na sio chama alichotokea. Hayati Dr. Magufuli alifanya mambo mengi sana na aliumiza wengi kwa ajili ya public interests na huu ndio ukweli haijalishi watu wakapinga.
Toka afariki, na usukani kukamatwa na Mheshimiwa Mama Samia kuna mambo mengi yametokea ambayo kwa wengi hasahasa sie wapenda haki yanatupa Faraja sana. Vivyo, hivyo kuna mabadiliko ambayo kimsingi yatatufanya tumkumbuke hayati Magufuli tu.
Mwenzenu baada ya kuhitimu sijabahatika kuajiliwa sasa nina miaka 2 mtaani. Alhamudulillah, nimefungua saloon ya kunyoa na pia nina duka la vinywaji baridi hapa mtaani kwetu.
Kinachonifanya nimkumbuke John Pombe Magufuli ni swala la umeme shughuli zangu zimesimama kwa sababu ya umeme. Kwaa siku umeme unakata hovyo hovyo bila sababu za msingi. Na taarifa haitolewi.
Tangu Jtatu, mfumo wa kununua umeme mtandaoni haufanyikazi, LUKU imeisha tangu jana saa 7 alasiri mpaka sasa mfumo unasumbua, wafanyakazi wangu (Kinyozi na muuza duka) siwalipi posho maana hakuna kazi bila umeme.
Kipindi cha mwendazake, kabla ya umeme kukata tulikuwa tunapewa taarifa, na haikuchukua muda, unarudi. Mfumo wa ununuaji wa LUKU ulisumbua kwa dakika chache tu.
Kwani Mama Samia si ulikuwa msaidizi wa rais John Pombe Magufuli, hakukuachia mbinu za kukomesha janjajanja za wafanyakazi TANESCO? Kama unaona waziri hafai tumbua weka mwingine. Tumia nguvu. Waafrika wengi bado ni washenzi sio wa kuwadekeza na kuwabeba mgongoni kwa mbeleko ya demokrasia na protoko.
Ni hayo tu jamani, nimeanza kumkumbuka John Pombe Magufuli.
UPDATE:
Jamani ili uelewe nilichoandika, weka hisia pembeni, tumia akili!
Sijasema kipindi cha JPM umeme haukukatika.