Ki ukweli, JPM alikomesha mambo mengi ya ubabaidhaji. Ndugu yangu, siyo umeme tu, kwa sasa kuna mambo mengi ya ovyo yamerudi kwa speed ya Kimbunga.
Wakati wa JPM hatukuzoea kusumbuliwa na vibaka, lakini siku hizi kumekuwa na ujambazi, unyang'anyi wa kutumia silaha na uozo mwingi sana umeanza kushamiri karibu kila kona.
Tuombe Mungu atusaidie huku na sisi tukiendelea kupambana.
RIP, JPM Baba yetu. Tutakukumbuka.
 
Exactly 👊
 
Yani sasa hivi mtu hata akinyeshewa mvua atalia kumkumbuka Magufuli.

Kama vile kipindi cha Magufuli mvua zilikuwa hazinyeshi.
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA YA MANUNUZI YA LUKU KWENYE OFISI ZA TANESCO ZA MIKOA NA WILAYA

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake kuwa, huduma ya manunuzi ya LUKU inapatikana kwenye ofisi za TANESCO za Mikoa na Wilaya, wakati wataalamu wetu wakiendelea na kazi ya utatuzi wa manunuzi kupitia njia za kielektroniki.

Tunaomba uvumilivu wakati wataalamu wetu wakiendelea na kazi kuhakikisha tatizo hilo linatatuliwa.

Tutaendelea kutoa taarifa kadri huduma itakavyo kuwa ikirejea na njia mbadala za kupata huduma.

Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza

Kituo cha miito ya simu makao makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100

Tovuti: www.tanesco.co.tz

Mitandao ya kijamii

Twitter: www.twitter.com/tanescoyetu

Facebook Tanesco Yetu

Imetolewa na:-
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu
Mei 19, 2021.
 
Unacheza na maneno lakini nia yako ni kushambulia awamu ya Mama kuwa ni dhaifu. kwa tasarifa yako umeme ulianz kusumbua kabla hata ya Mwendazake hajaenda zake! Yapo maeneo, tena Dar es Salaam, umeme haukuwa wa uhakika. kwanini unataka Mama amtumbue waziri wa umeme, lakini hukutaka Mwendazake amtumbue?
 
Kwa sisi tunaoishi vijijini inakuaje? Tufunge safari mpaka Wilayani Tsh. 7000 ili kununua umeme wa 3500?
 
acha ujinga bana,unadhani ni faida gani unapata kukaza mishipa unaandika uongo!!!!tanzania nzima ipi ambayo chato haipo sasa!!!

mimi naishi mombasa ukonga dsm,mara ya mwisho umeme kukatika,ulikaa masaa 12 baada ya nguzo kugongwa na gari 2018,na walipita kutanganza,siku nyingine ukikatika ni haizidi nusu saa umerudi.unzungumzia jenerator,unajua generator ýa kusukuma fridge inaukubwa gani???kama mmeanza kampeni zenu za kuuza majenereta kama 2012 mseme mapema.

inawezekana hapo ulipo hujui kama tatizo limeanza toka jumatatu,sababu baba yako alinunua umeme mwingi wa laki nzima,na hauna dalili ya kwisha.
 
Ttcl hawahusiki kwa chochote mkuu. We sema tu huna uelewa wa hii mifumo inavyofanya kazi. Mfumo wa LUKU huko linked kati ya Tanesco, ega, na MNOs. Tanesco kama mtoa huduma ya umeme, ega akiwakilisha serikali na tra ktk kukata kodi, MNOs ni mobile network operators ambao wana electronic interface na wateja kupitia simu. TTCL ni mojawapo ya hawa MNOs. Ukimlaumu TTCL ktk hili basi walaumu na voda, tigo airtel na halotel. Pia kuna third part kama wale wenye mashine za luku kama maxcom.
 
Haisaidii
Muombee tu apumzike kwa amani,
Alieshika usukani sasa ni mama yetu Samia Suluhu Hassan,mama la mama!
Tanzania oyeeeee
 
Haisaidii
Muombee tu apumzike kwa amani,
Alieshika usukani sasa ni mama yetu Samia Suluhu Hassan,mama la mama!
Tanzania oyeeeee
hatukatai ni mama yenu,ila msiharibu kazi sababu hawezi kuwachapa.hiki ndicho tusichotaka.
 
hata simu yako ikizima na kuwaka maramoja kwa siku,utaipuuzia.

ila ikizima isiwake jumla utaanza kuogopa.jtatu ilivyoanza kusumbua ulisikia kuna mtu anapiga kelele??watu walijua ni kawaida kwa vitu kama hivi kutokea kuna binaadam kule.
 
Kuna wajinga wamezusha eti umeme haununuliki kwenye simu nimewasceenia nilinunua Jana kupitia TIGO pesa saa 11 jioni wameingia mitini. Matendo anajifanya Mama ni mwiba Kwa vibaraka WA Dicteta waliachwa ndio maana wanampaka Mama matope asiyostahili.
Tanesco wametolea taarifa tatizo lipo...wewe mwanaJF unapingana nao..sijui tukuweke kwenye kundi gani?
 
Mama ana roho nzuri, mpole, msamehevu na muelewa, kwa sifa hizi za mama watendaji wa sekta nyingi watavurunda.
mikumi mingine kwa mama.
Si juzi tu mlikuwa mkimponda kwa sababu ati haishughulikii Chadema ninyi jamaa ni vigeugeu sana
 
Hivi kwani Mama Samia si alikuwa msaidizi wa rais John Pombe Magufuli, hakumuachia mbinu za kukomesha janjajanja za wafanyakazi TANESCO?.

Kama anaona waziri hafai atumbue aweke mwingine, atumie nguvu maana waafrika wengi bado ni washenzi sio wa kuwadekeza na kuwabeba mgongoni kwa mbeleko ya demokrasia na protokal.
 
Mambo mengi ya hovyo yanarudi. Juzi niliongea na ndugu yangu wa tanga kasema Lile kundi la watoto wa ibilisi limerudi baada ya kutokomezwa kipindi Cha Magufuli. Kwa Sasa hata polisi hawajali Tena kulinda raia wanasubiri mgao toka kwa waporaji tuu.
Labda mh rais Hana mpango wa kuendeleza mazuri ya JPM anataka kuendeleza ya JK.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
kwamba kipindi chake umeme ulikuwa haukatiki?

umesahau mpaka nyuzi za malalamiko zilivyotamalaki humu Jf?
Soma Tena hajasema ulikuwa haukatiki. Ila ilikuwa Mara chache na ulirudi baada ya muda mfupi.
Umesahau bwawa la mtera kuisha maji ili watu wanunue majenereta? Nchi inaenda kubaya Kama hulioni hili Basi Tena.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Watu wameshaanza kurudi kama zamani kwa kufanya kazi kwa mazoea na bila hata chembe ya wasiwasi, siku hizi watoa huduma kwenye taasisi za serikali wameanza kuwa na viburi, hakunawa kumuogopa tena. Tunarudi enzi za Msoga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…