Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?
Ukipata nafasi ya kusafiri,kuzunguka mikoa tofauti tofauti ndio utagundua kuwa taifa limepoteza mtu muhimu sana,maana ni mpaka kule ulikokuwa hutarajii kuona maendeleo kuko vizuri...
Barabara nyingi zimejengwa wakati wa Mkapa na Kikwete! Bado unaendelea tu kumtukuza? Nyinyi ndiyo mlio changia kumvuruga mzee kwa unafiki wenu ulio pitiliza.
 
1.Chato International Airport
2.Chato National Park
3.Trafic light Chato
4.3 star hotel Chato (TANAPA)
5.Bohari ya kanda madawa Chato
6.Hospital ya rufaa Chato
7.Stadium (proposa)
8.CRDB Chato
Chuo cha VETA Chato
Library Chato
 
Wafanyakazi hewa + Vyeti feki. Ila ninampongeza kwa kuleta nidhamu serikalini na kuwakomesha wauza sembe.
Utawala wake uliniathiri kiasi Fulani, ila jambo moja alilokuwa ananifurahisha ni kuwakomesha wahindi kumzoea.

Wahindi nadhani huko waliko Leo kila nyumba kunapikwa kachori na kucheza kuchukuchu hotae.
 
Nitamkumbuka kwa
1. kuyazima maisha ya kaya ZA waliokuwa watumishi wa serikali zaidi ya 12,000 na kudhulumu pension yao, sijui wasemacho huko waliko
2. watumishi kutopandishwa mishahara kwa kipindi chote cha utawala wake
3. Watumishi wengi kutopandishwa madaraja
4. Serikali kutochunguza suala la Tundu Lissu kupigwa risasi
5. Kunyima haki ya kuchagua kiongozi umtakaye
6. Teuzi zisizofuata taratibu-maded, madas nk. Kursus konyne cha taratibu-maded sheria
7. Kila kitu kafanya yeye badala ya serikali
8. Wanaccm kujiona wao ndio haswaaaaa wenye nchi na kunyanyasa wengine
9. Uongo wa serikali kwa mengi. kuugua kwake ni mfano
10. Kuwatia uoga watu kuzungumza mambo ya serikali.
11. Kutunga sheria kandamizi
12.Kufunga magazeti.

Yaaani yote haya, vile alivyotendewa Tundu Lissu kuanzia kupigwarisasi na kunyimwa halo zake PAMOJA na kuharibu chaguzi ZA serikali za mitaa na huu Mkuu, sijui kans dhambi hizi zitasameka kwa sababu bado wengi wana huzuni mioyoni wao.

Ila nilipenda misimamo yake hasa katika kusimamia na kutekeleza alichokiamini hata kama ni kwa makosa. Alifanikiwa.

Mwenyezi Mungu amsamehe dhambi kama zipo kwa haya, na ampe pumziko jema ktk maisha ya yajayo.
 
Kikwete alikuta bia 500 mpaka anaondoka akaacha 2500.
Magufuli alikuta bia 2500 mpaka anakufa kaacha 1800, hili wengi hawalioni kabisa.

Sikuwahi kupanda treni toka nizaliwe ila mwaka 2020 nimepanda Deluxe kwenda Moshi, hili umuhimu wake utaonekana baada ya treni kufa na kuanza nauli za 80k kwenda Moshi.

Kabla ya 2015 ilikua ni kawaida kusikia matukio ya ujambazi tena karibu na vituo vya Polisi, ila toka 2015 mpaka sasa sijaskia jambazi aliesalimika kwenye ujambazi,na matukio yamekuwa machache sana.
 
Ana mabaya seroous sana, ila nitamkumbuka kwa mazuri haya.

1. Kueneza umeme vijijini
2. Kujenga vituo vya Afya nchi nzima.
3. Kupambana na rushwa
4. Kuanzisha masoko ya dhahabu
5. Kudeal na unyonyaji kwenye madini
6. Nidhamu ya kazi na uwajibikaji kwa civil servants
7. Kutuonyesha kuwa si lazima tufuate njia ya wengi(kujiamini)
8. Bwawa la Nyerere
9.Katufundisha uthubutu.
 
Maisha magumu na madeni mazito kufikia mahali "wapo" wasemao wamewahi kufikiri kujikili!!
 
Back
Top Bottom