Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?
Binafsi nimeuzunika na kuna mengi nimenufaika siwezi kutaja kimoja kimoja ila alikuwa mtu makini sana sana kwa wananchi wa daraja la kati na chini kabisa.

R.I.P my president tutaonana baadae.
 
RAIS ASIYEJALI ASIYE NA CHEMBE YA UTU!
He was in a class of his own,,special case..
Nitamkumbuka kwa kusisitiza kuhamia dodoma,,miradi mikubwa kama reli ya umeme,bwawa la umeme,barabara etc
 
Mi kiukweli nilikuwa nafurahia mabarabara yalivyopanuliwa na kila sehemu lami tu ( kwa sisi wakazi wa dar)

Yaan mi nilikuwa ni kuteleza tu barabarani hadi raha...

RIP John
 
Nitamkumbuka kwa mema yenye tija na maendeleo kwa nchi yetu. Hakika ni Rais wa kipekee kwangu aliutendea haki utendaji kazi wake bila kumuogopa binadam yeyote. Mungu ampumzishe kwa amani kiongozi wetu aliyekuwa na uthubutu wa kufanya mambo.

[emoji992][emoji992][emoji992][emoji992][emoji992] [emoji992][emoji992][emoji992][emoji992][emoji992][emoji992][emoji992][emoji992]l[emoji992][emoji992][emoji992][emoji992]
 
"Nitumbue au nisitumbue?"
"Tumbuaaaaaa"

Hakutoa ajira kwa vijana huku akijua wanadharaulika na mashemeji huko mtaani.

Asubuhi njema, Asubuhi njema, Asubuhi njema.
 
Ukipata nafasi ya kusafiri, kuzunguka mikoa tofauti tofauti ndio utagundua kuwa taifa limepoteza mtu muhimu sana, maana ni mpaka kule ulikokuwa hutarajii kuona maendeleo kuko vizuri.
 
1. Maana halisi ya demokrasia na utawala wa sheria kimatendo
2. Malipo ya Makufuru kwa Mungu muumbaji ni hapa hapa
3. Utawala wa wasiojulikana ndani ya dola huru
4. maumivu kwa wapinzani
5. Ukanda ya ziwa
6. Kushamiri kwa ukabila; na kutuachia vipande vya taifa letu
RIP John Bwana amekupenda zaidi. Pumzika sasa
 
Kurudisha wanafunzi shuleni during corona outbreak.
Magufuli ni kamanda na ameshaumaliza. Mwendo apumzike kwa amani[emoji120]
 
Kwa kweli sijafurahi kabisa kumpoteza kiongozi mahiri kama john pombe magufuli alikua hodari sana katika uongozi wake mianya ya rushwa alikomesha, uonevu, huduma katika taasisi za kiserikali zilikua zikitolewa kwa heshima na bila ubaguzi, kajenga miradi mingi sana nchini, elimu bure, miundombinu, hudumu hospitalini ziliboreshwa, huduma za maji mikoa mbalimbali alitoa fedha miradi ikamilishwe, uwanja wa ndege wa mwl Julius Nyerere aliukarabati kwa ufupi Rais wangu kifo chako John Pombe Magufuli umeniachia simanzi moyoni mwangu,
Huyu si ndiye aliyeiba kura uchaguzi uliopita au siyo yeye?
 
Back
Top Bottom