Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?
Watanzania ni viumbe wanafiki sana Duniani. Nlijifunza kitu kwa wazungu.

"Mzungu anaweza kusema kabisa Komeo simkubali,simpendi ila jambo hili alilifanya lilikuwa zuri. Lakini bado simpendi"

Sisi Waswahili tukimchukia mtu tunamchukia na kila analolifanya hata kama jema. Tunendeleza mihemko,jazba na chuki binafsi. Hata jamaa akitembea juu ya maji lets say baharini au ziwani tutasema
"jamaa anatumua vumbi sana na kuchafua mazingira"

Mazuri ya Magufuli:
1. Miradi ya madaraja kupunguza msongamano ni miradi mizuri iliyotumika kwa pesa za watanzania. Hata kama kuna waliowaza before lakini kuwaza si kutenda

2. Mradi wa SGR ni mradi superb kwa ajili ya maendeleo ya mikoa husika na Tanzania kwa ujumla. Miaka ya nyuma mradi kama huu ungekwamishwa sana kwa sababu ya wamiliki wa magari ya mizigo kutoupenda kabisa. Aliweza kuchukua hatua.

3. Daraja la Busisi na miradi mingi ya Barabara nchi nzima. Lakini alijitahidi sana kuzuia Ufisadi uliokuwa umeota mizizi awamu zilizopita.

Mabaya ya Magufuli.
1. Aliamini mtu anayempiga au asiyekubaliana naye ni adui yake. Hivyo akasababishwa kuzungwa na wanafiki wengi sana ndani na nje ya chama chake isipokuwa wapinzani wachache.

2. Alikuwa anaamini WAPINZANI WOTE NI WAPIGA DEAL TU kama ambavyo aliona waliokuwa wakipiga deal kupitia siasa awamu zilizopita.

3. Aliamini Wafanyiabiashara wengi walikuwa wapigaji kama ilivyokuwa awamu za awali. Hivyo akagombana nao wengi sana hasa pia waliokuwa kweli wapigaji kama akina Manji Kwa Mujibu wa Chadem List of Shame na Mafisadi Papa.

MIMI MTANZANIA NIMEISHIA HAPO.

Pia nakaribisha mapozi mengi tu kwa wale ambao watu wao watakuwa wameguswa. Hamna cha kunifanya Hili ni Jukwa Huru sijavunja sheria yoyote ile.
Naona Moderator unapambana kila namna upate pa kuuficha huu uzi.
 
Legacy ya JPM imeandikwa mioyoni mwa watanzania asilimia 90% ambao wengi wao ni wananchi wasafi, wapambanaji, ambao tangu mwanzo wamekuwa wakipata mahitaji yao kwa jasho lao kama maandiko yalivyosema.

Nyie mliozoea kujitajirisha kwa kunyonya damu za watu, mlikiona cha mtemakuni. Mungu alimuleta JPM kutuonesha ni kwa kiasi gani tunachezewa na tumekuwa tukichezewa.

JPM katuonesha njia ni rais bora kuwahi tokea duniani . Hakuogopa mtu kwa sababu ya cheo chake au pesa zake.

Haijalishi mtukane kiasi gani, historia itabakia mioyoni mwetu, na tutairithisha kwa vizazi na vizazi hata isipofundishwa mashuleni.

Kipindi chake, mafisadi papa yalikamatwa...Ruge, Seth na mengine madhamini ya CCM.

Kipindi chake thamani ya madini ilionekana, mikataba ya kipumbavu ilibadilishwa.

Kipindi chake, mapato ya kodi yaliinuka na watoto walisoma bila malipo.

Daima atabakia mioyoni mwetu.
 
Mkuu Lala Upumzike.. Upate Akili ya Kutafuta Ugali wa Watoto wako Kesho
Hadi kuniona humu jua kuwa natumia hela, nina miradi yangu mingi tu ambayo hata nikiamua kutokufanya kazi mpka miaka 100 ijayo nitaendelea kula vizuri na kusomesha ndugu, familia na wasiojiweza kama navyofanya sasa.
 
Hadi kuniona humu jua kuwa natumia hela, nina miradi yangu mingi tu ambayo hata nikiamua kutokufanya kazi mpka miaka 100 ijayo nitaendelea kula vizuri na kusomesha ndugu, familia na wasiojiweza kama navyofanya sasa.
Pole Sana Watu wenye Miradi ya Aina Hiyo Huwa hawana Akili Kama zako. Hata hivyo shukuru nimekujibu koment yako. Goodday
 
... nani ana muda wa kumtuma nani na ukweli uko wazi hivyo? ... acha wakina Diallo waseme ukweli utakaotuweka huru! UNAFIKI TUPA KULEE!
1625872978074.png
 
Kaka nisaidie kuelewa maniki yako.
Mwanzoni unasema unaleta habari hapa kama Jamiforums ni "sehemu ya kuongea ukweli".
Baadaye unamsifu kiongozi ambaye serikali yake ilijitahidi kunyamazisha Jamiiforums kwa kuilazimisha kutoa siri ya majina ya wachangiaji.
Hayo mawili yanalingana kivipi?
 
Back
Top Bottom