Naona Moderator unapambana kila namna upate pa kuuficha huu uzi.
 
Legacy ya JPM imeandikwa mioyoni mwa watanzania asilimia 90% ambao wengi wao ni wananchi wasafi, wapambanaji, ambao tangu mwanzo wamekuwa wakipata mahitaji yao kwa jasho lao kama maandiko yalivyosema.

Nyie mliozoea kujitajirisha kwa kunyonya damu za watu, mlikiona cha mtemakuni. Mungu alimuleta JPM kutuonesha ni kwa kiasi gani tunachezewa na tumekuwa tukichezewa.

JPM katuonesha njia ni rais bora kuwahi tokea duniani . Hakuogopa mtu kwa sababu ya cheo chake au pesa zake.

Haijalishi mtukane kiasi gani, historia itabakia mioyoni mwetu, na tutairithisha kwa vizazi na vizazi hata isipofundishwa mashuleni.

Kipindi chake, mafisadi papa yalikamatwa...Ruge, Seth na mengine madhamini ya CCM.

Kipindi chake thamani ya madini ilionekana, mikataba ya kipumbavu ilibadilishwa.

Kipindi chake, mapato ya kodi yaliinuka na watoto walisoma bila malipo.

Daima atabakia mioyoni mwetu.
 
Mkuu Lala Upumzike.. Upate Akili ya Kutafuta Ugali wa Watoto wako Kesho
Hadi kuniona humu jua kuwa natumia hela, nina miradi yangu mingi tu ambayo hata nikiamua kutokufanya kazi mpka miaka 100 ijayo nitaendelea kula vizuri na kusomesha ndugu, familia na wasiojiweza kama navyofanya sasa.
 
Hadi kuniona humu jua kuwa natumia hela, nina miradi yangu mingi tu ambayo hata nikiamua kutokufanya kazi mpka miaka 100 ijayo nitaendelea kula vizuri na kusomesha ndugu, familia na wasiojiweza kama navyofanya sasa.
Pole Sana Watu wenye Miradi ya Aina Hiyo Huwa hawana Akili Kama zako. Hata hivyo shukuru nimekujibu koment yako. Goodday
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚... Kabla wewe na huyo uliyemtaja hajazaliwa, maisha yalikuwepo, na yataendelea kuwepo.
 
Kaka nisaidie kuelewa maniki yako.
Mwanzoni unasema unaleta habari hapa kama Jamiforums ni "sehemu ya kuongea ukweli".
Baadaye unamsifu kiongozi ambaye serikali yake ilijitahidi kunyamazisha Jamiiforums kwa kuilazimisha kutoa siri ya majina ya wachangiaji.
Hayo mawili yanalingana kivipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…