Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?
Nitamkumbuka kwa kuwaletea watanzania umaskini na ufukara maradufu, Mara dahari kuliko watangulizi wake ?

Nidhamu ipi Serikalini wakati utendaji umeshuka sana kutokana na go slow attitude ya Wafanyakazi wengi kwa kutoongezewa mishahara? Nidhamu ipi ya kufukuza watu kiholela bila kufuata taratibu husika ambazo zinalinda haki ya Wafanyakazi?
Kweli ndugu, yani was kukumbukwa hapa ni walioteseka na kufa chini ya utawala wake, yeye asahaulike kama hakuwahi kuwepo vile, worst president yet!
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Nawawakumbuka kina ben SAANANE,AZORY GWANDA NA Wengine ila pia namkukumbuka kwa upendo wake kwa ccm hata kama ni kwa uovu. Nawaz huyu MUNGU Ndio hutoa viongozi mbona huyu mambo mengi mabaya yalifanyika kwa awamu yake? Ila MUNGU AMSAMEHE TU
 
Mazuri yake yote, yanafutwa na ukatili wa kuua watu na kuwapoteza.
 
Watu wanaomsifu Meko wanaangukia ktk moja ya makundi haya;

1- Makada was CCM, hawa wanamsifu bila choice, wakati mwingine kinafiki, kwasabu wasiposifu waaonekana wasaliti.
2- Watu wasio wapambanaji (kula kulala), hawa hawaoni changamoto za kiuchumi ambazo watu wapambanaji wanaziona kwenye utafutaji, hawa ni kuamka, kula, kuangalia muvi na kulala.
3- Watu ambao hawajui lolote linaloendelea duniani, hawa huangalia TBC muda wote, so wamejazwa na propaganda za kipuuzi za TBC, wakiambiwa tupo kwenye vita ya uchumi wanaamini, hawajiulizi "ni nani atapoteza muda kupambana na maskini?", wakiambiwa sisi ni tajiri, wanashangilia tu.
 
Kwenye kusimama kwakwe njiani.

Mwananchi: mheshimiwa raisi mimi limenikuta abc nimeenda abc, sasa mwaka wa sita nazungushwa.

Magufuli: Haya mama nimekusikia, mkuu wa wilaya yupo wapi?

Mkuu wilaya; kanyoosha mkono

Magufuli: haya mpe mic

Magufuli: ili swala unalijua?

Mkuu wa wilaya: ndio mheshimiwa ili jambo limeenda abc kaambiwa asubiri, blah blah

Magufuli: Nyie sikilizeni mko hapo kutatua shida za watu, sio msubiri mpaka mimi nije .... etc na vichambo vyake.

Magufuli: haya OCD na nyie wasaidizi wangu chukueni number ya huyo mama asisumbuliwe mmenisikia.

Magufuli: mama usijali, nitalifuatilia.

RIP Magufuli
 
1. Tanzania ni nchi tajiri, in terms of natural resources
2. Tumechezewa mno kwa muda mrefu
3. Tumeibiwa mno kwa muda mrefu
4. Tukiamua tunaweza (kuondokana na huu umaskini wa kujiletea wenyewe.
5. Natural resources ni zetu (siyo zao) tuzitumie kuleta mabadiliko ktk maisha ya watu wetu na kujiletea maendeleo.
#4 ndo inanigusa zaidi!
 
Watu wanaomsifu Meko wanaangukia ktk moja ya makundi haya;

1- Makada was CCM, hawa wanamsifu bila choice, wakati mwingine kinafiki, kwasabu wasiposifu waaonekana wasaliti.
2- Watu wasio wapambanaji (kula kulala), hawa hawaoni changamoto za kiuchumi ambazo watu wapambanaji wanaziona kwenye utafutaji, hawa ni kuamka, kula, kuangalia muvi na kulala.
3- Watu ambao hawajui lolote linaloendelea duniani, hawa huangalia TBC muda wote, so wamejazwa na propaganda za kipuuzi za TBC, wakiambiwa tupo kwenye vita ya uchumi wanaamini, hawajiulizi "ni nani atapoteza muda kupambana na maskini?", wakiambiwa sisi ni tajiri, wanashangilia tu.

Acha kutuaminisha ya kuwa wewe ndio unaijua nchi hii, binafsi mimi sio mtu wa siasa kabisa nayasema haya kwa jicho lisilolenga na kuona siasa. JPM alikuwa kiongozi mzuri hata kama alikuwa na mapungufu ni ya kibinadamu na alilazimika kufanya aliyoyafanya kwa manufaa na maslahi ya nchi na sio maslahi binafsi.
 
1-Kuua ni mapungufu ya kibinadamu?
2- kubambikia watu kesi ni mapungufu ya kibinadamu?
3- kupenda kuabudiwa kama Mungu ni mapungufu ya kibinadamu?

Hauko sawa wewe
 
1-Kuua ni mapungufu ya kibinadamu?
2- kubambikia watu kesi ni mapungufu ya kibinadamu?
3- kupenda kuabudiwa kama Mungu ni mapungufu ya kibinadamu?

Hauko sawa wewe

Kamuuwa nani? Weka ushahidi hapa ukishindwa kaa kimya kojoa ulale.

Kwa kuwa upo kwa ajili ya kupinga na kukosoa kila kitu endelea hivyo hivyo mimi nitamkumbuka kama raisi wangu au unataka nikukumbuke wewe?
 
Maandiko ni mengi mitandaoni kwa sasa hivyo tusichoshane kwa bandiko refu.

Marehemu Dr JPM ulifanya mengi wakati wa uhai wako kama ilivyo kwa binadamu wengne, sisi siyo Malaika. Maisha yetu yana pande mbili kama sarafu, mema na mabaya. Na haya ndio yanayosalia kama kumbukumbu pale uhai wako unapofikia kikomo.

Kwa mimi nimeamua kumkumbuka Rais JPM kwa kufikisha umeme kijijini kwetu mwaka 2016, kijiji chetu kimepakana na barabara kuu ya Arusha- Moshi ila la ajabu kuchepusha umeme tu uingie kijijini ilishindikana tangu uhuru.

Sasahivi nikienda kwa mama eti panawaka km mjini.

Kwaheri baba ngoja sisi tuendelee na safari japo nasi hatujui tamati yetu.
 
Hakikisha kabla hujaondoka, usiondoke na damu za watu zinakulilia kama damu ya Habili.
 
Mimi nakumbuka mateso alotupa yamenifanya niwenafikiria sana ili nipate pesa kwa jambo lolote nnalofanya
 
Raha ya milele umwangazie eeh bwana.

Mabibi na mabwana alikuwa na mengi kama alivyosema mwenyewe:

Ametutoka jembe letu JPM:

Vita vya uchumi viko pale pale.

One down, tusikate tamaa tutashinda hii vita.

Aluta continua victoria acerta!
 
Vita gan ? Sasa au in five years mmefanya Jambo gani la maana .

Think twice eti vita ya uchumi yaan chawa wa ccm niwapuuzi.
 
Back
Top Bottom