Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kusitisha uhamisho wa wafanyakazi bila sababu za msingi matokeo yake usaliti ktk ndoa ulizidi, wajanja wa connection ndio waliweza kuhama walala hoi tumeozea vijijini.Kwa kweli sijafurahi kabisa kumpoteza kiongozi mahiri kama john pombe magufuli alikua hodari sana katika uongozi wake mianya ya rushwa alikomesha, uonevu, huduma katika taasisi za kiserikali zilikua zikitolewa kwa heshima na bila ubaguzi, kajenga miradi mingi sana nchini, elimu bure, miundombinu, hudumu hospitalini ziliboreshwa, huduma za maji mikoa mbalimbali alitoa fedha miradi ikamilishwe, uwanja wa ndege wa mwl Julius Nyerere aliukarabati kwa ufupi Rais wangu kifo chako John Pombe Magufuli umeniachia simanzi moyoni mwangu.
Moderator wamenikosea, kwa nini wameunganisha Uzi Wangu Kwenye Uzi Wa Randy ortonAisema yeye ni jiwe bana, hii chuma mmeitoa wapi jamani?
Umeweza kumuelezea vzr sana kwa maneno machache.Rais wa ovyo, mbinafsi aliyependa kutukuzwa... Wajanja wakamjulia... wakamtanguliza.
Alitaka kwenda haraka haraka mwenyewe badala ya kuunganisha wengine na kuwa imara zaidi ili kwa pamoja tufike mbali zaidi.
Yako wapi sasa.
Ila wajinga wataona yeye ndo yeye.
Umejitahidi sana mkuu ingawa kuna mengi sana umeyaacha likiwemo la kufuga na kulealea vijana wahuni waliokua wanaharibu sana taswira ya uongoz wake, konda boy na wenzie.Nitamkumbua Magufuli kwa ukatili wake wa kutisha
1. Kuvunja nyumba za wananchi wa Kimara - Mbezi bila chembe ya huruma ila wale wa mwanza aliwaachia
2.Kupora Korosho za wananchi wa mikoa ya kusini kwa mtutu wa bunduki, hii hali iiwatia wananchi umasikini
3. Bila kujali kuwa watu wameshahudumu serikalini kwa muda mrefu na wanategemea kustaafu, akapitisha hoja ya uhakiki na kuwafukuza maelfu ya watu hao Huku akiwaacha bila kuwagusa wanasiasa na wateule wake katika hilo zoezi
4. Kubabikizia watu kesi za uhujumu uchumi, kuwatesa kupitia mfumo wa mashitaka na kuzisababishia familia zao maumivu makubwa na hali ngumu
5. Kuendelea kuwashikilia mamia ya masheikh walioko jela huku akisamehe wabakaji akina Babu Seya
6. Kukataa kuwapa watumishi wa serikai stahiki zao kwa wakati, ikiwemo kupandishwa madaraja na nyongeza za ishahara
7. Kuharibu chaguzi zote zilizofanyika chini ya serikali yake, kuanzia zile za marudio, serikali za mitaa na uchaguzi mkuu, Alidhuluu haki ya wananchi kuchagua viongozi wao
8. Magufuli alitunga sheria kandamizi, na kuvuruga misingi ya katiba. Kafanya kia jitihada kulifanya bunge liwe butu, kuiweka mahakama mfukoni etc
9. Magufuli alikuwa na kauli mbaya zisizo na staha mfano "sisomeshi wazazi, serikali siyo iliyoleta tetemeko, baki na mavi yako nyumbani, nitapiga mashangazi.. etc"
10. Alikuwa na miradi kadhaa au mpango wa miradi kadhaa ambayo ni white elephant mfano, uwanja wa ndege Chato, Midege,Mpango wa Uwanja wa mpira Chato
11..Magufuli alikuwa mdini, huhitaji kuwa mwanasayansi wa elimu ya jamii kuona kuwa teuzi zake ziliaia sana watu wa imani moja
12. Magufuli alikuwa haheshimu katiba waa sheria pale zinapokinzana na anachokitaka yeye, mfano haki ya kufanya siasa kwa vyama vya siasa iliyokuwepo kikatiba hakuiheshimu
13. Magufulu hakuthubutu na wala hakujali kufanya uchunguzi juu ya kupotea kwa Ben Saanane, Azory Gwanda, Kanguye na waliompiga risasi Lissu
Kwa hiyo mimi nakichukulia kifo cha Magufuli kama nafasi muhimu ili Taifa letu lipone.
Na sisi kama Taifa, tumeona kwa macho yetu namna katiba ya sasa ilivyokuwa hatari kama tunampata mtu mmoja asiyejali, ambaye ana element za udikteta, basi tuitumie nafasi hii kuliponya Taifa
Tangulia Magufuli, uwongo mbaya sitokumiss na sijawahi kukupenda kwa style ya uongozi wako, ninatamani Taifa lisipate Kiongozi mwenye mapungufu ya aina yako, ni mapungufu hatari kabisa
Sikuwahi kuwa na ushabiki kwa Aliyekuwa Rais wa Tanzania Marehemu John Pombe Magufuli. Sikuwahi kuwa mshabiki au mfuasi wa mwanasiasa yeyote nchini au Chama chochote cha Siasa.
Nlimkosoa na kumsifia pale nilivyoona. Kwa haya Mazishi yaliyofanyika na jinsi watu wa hali ya chini wanavyohuzunika na kuomboleza. Nikiangalia mafisadi na wafanyabiashara ambao hakuwa waamininifu wakisheherekea. Naanza jiuliza mara nyingi nyingi.
Inawezekana tutakuja juta hapo baadaye.naona jinsi ambavyo waliaji wakubwa ni maskini na wa kipato cha chini. Na wanaofurahia ni wafanyabiashara ambao hawakuwa waaminifu.
Naona watu wanavyolia,wanavyoumia,wanavyohangaika na huu msiba. Na hakuna aliyewawezesha. Nasema moyoni "hakika huyu alikuwa ni mwanaafrika, mwananchi"
Nimejiwa na simanzi kubwa. Na ninaomba msamaha kwa yale ambayo nilimkosea kwa njia moja au nyingine. Naye kama kuna ambayo alinikosea nmemsamehe. Alikuwa binadamu kama mimi na wewe.
Nimesikitika sana na kuumia.