Mbowe bado angekuwa uhamishoni
Sabaya na wenzake kina Chawamila, porepore na bashiru bado wangekuwa ofisini au pengine kupandishwa cheo kabisa
Tanzania ingekuwa salama zaidi kuhusu Corona
Gwajima wa kike angekuwa ameshakunywa lita kadhaa za mchanganyiko wa tangawizi, limao, saumu, kitunguu maji na pilipili
Ng'ombe wote wa chato wangekuwa wameshafungwa site mirror kwaajili ya kuwaongoza kwenye barabara za chato
Gas ya kupikia ingekuwa bei nafuu kuliko sasa
Miamala ingekuwa vilevile kama awali, huku vifurushi vingekuwa vimepanda bei
Sheria ndogondogo zingekuwa zimeshatungwa kwaajili ya kuibana mitandao zaidi 😬
Jokate na Samia wangekuwa hawajadungwa chanjo ya majaribio
Bado tungekuwa hatujasikia sauti ya mstaafu Kikwete labda tungeona Picha zake akilima mananasi kule mkoani Pwani
Tungekuwa hatupati changamoto ya kukatika umeme mara kwa mara
Kuna watu wangekuwa wameshauawa kwa kuwa kinyume na matakwa yake
Tungekuwa tumeshapata misamiati mipya kutoka kwake 🤣🤣🤣
Na kubwa zaidi Tanzania ingekuwa inatrend duniani kwa kujitenga kabisa na propaganda za korona huku tukipiga kazi wakati huohuo tukiwa tumeongeza imani kwa jiwe kutokana na misimamo yake isiyoyumba kuhusu mabeberu 🏃♂️🏃♂️🏃♂️🏃♂️🏃♂️🏃♂️