Unajua fikra na mawazo ya Mheshimiwa ilikuwa kuifikisha Tanzania pale ambapo mwananchi wa kawaida atakuwa anafurahia maisha ya uswahilini na hana kudhalilishwa wala kubugudhiwa na anaheshimika kwenye taasisi zote,
Wakati wake mwananchi hata alievaa mararu nguo za viraka akifika kwenye taasisi za serikali yake akipokelewa na hata kukaribishwa maji ya kunywa na haichukui muda anasikilizwa shida zake na kuahidiwa kufanyiwa kazi ,siku mbili ilikuwa unapata passport ,siku mbili unapata kadi ya Uraia au kitambulisho cha utaifa,leo nenda kajaribu utaambiwa mashine hazifanyi kazi na haijulikani zitatengenea lini maana kimeagizwa kutoka Japan na ndege siku hizi kama unavyojua haziendi kutokana na korona ,njoo ukiulizia au tutakupigia simu.
Shida zimeanza kurudi na kuzaana,usilete habari za kisiasa hizo ni kazi kama kazi zingine mambo ya wanasiasa na majilabu na majigambo hayahusiani na shughuli za kiutawala.
Katika utawala na uongozi na usimamizi Mheshimiwa Magufuli aliweza. Ila huyu dada naona anazingua tu. Vyombo vya huduma za kijamii katika serikali yake zimeanza kusua sua.
Nikimtazama naona anavutwa na mkondo wa shughuli za kisiasa ambazo Magufuli alizipiga chenga na kuwaacha wapinzani wakipiga makelele kwenye vyumba.