Ninawasalimia nyote, ninakiri pamoja na kwamba bwana yule aliyetangulia mbele za haki tangia Marchi 17, 2021 kama tulivyotangaziwa, kuna mazuri kadhaa ambayo kwayo tutakuwa tumeya mis.
Mojawapo ni kukatikakatika kwa umeme kwa muda mrefu haikuwepo, kasi ya kuwekewa umeme kwenye nyumba zetu, mfumko na kasi ya kupanda bei za bidhaa kama vile: mafuta ya aina zote, vifaa vyote vya ujenzi, tozo za miamala za simu, kupanda kwa bei ya mbolea kwa 100%, gesi ya kupikia majumbani bei juu, kurejea kwa kasi matukio ya ujambazi, nidhamu ya kazi imepungua! Kwa ujumla ni mambo mengi mno sitoweza kuorodhesha yote.
By the way, the late nilikuwa simkubali kwa vitendo vyake vya kikatili kwa waliokuwa wanaepingana naye kama akina TL,Saa nane, na wengi wengineo wengi tu!