Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?
Leo nimemkumbuka Hayati Magufuli, unafikiri angekuwepo hai, leo jambo gani lingekuwa pengine ndio stori ya nchi?

Nabashiri, pengine leo hii angekuwa zake anakagua mradi wa reli ya kisasa akitoa na maagizo kwa kandarasi
Na corona hii angekuwa amejificha chini ya chaga huko Chato..
Bora limeondoka hilo shenzi.
 
Mkuu Chahali, kuna aina kuu tatu za kumbukumbu za binadamu katika matendo yake aliyotenda wakati wa uhai wake hapa duniani: 1. Binadamu ambae matendo yake aliyatenda kwa ufanisi na kwa upendo kwa maendeleo yote, huyu atakumbukwa kwa muda mfupi kudogo. 2. Binadamu ambae matendo yake aliyatenda kwa ufasani, upendo na kushikiana na watu katika maendeleo yao bila upendeleo wa aina yeyote, huyu naye atakumbukwa kwa muda wote na wapenda uwazi na maendeleo. 3. Binadamu ambaye matendo yake aliyotenda ni kwa maendeleo ya nchi yake kwa ufasini lakini kwa mateso kwa watu wake, huyu atakumbukwa na watu wote (wa kikazi chake na kizazi tarafajiwa) duniani.
Mfano mzuri ni kwa Rais John Kennedy na Rais Hitler.
Ntamkumbuka kwa haya:1 Bwawa la umeme (Lingeitwa kwa jina lake)
2.Reli ya SGR.
3.Barabara.
Nchi itafunguka vizuri.
 
Kuna Mengi ya kumkumbuka ila zaidi ntamkumbuka kwa barabara ya Lami na Maji huku gongo la mboto ndani ndani...25yrs since wazee wahamie g'mboto ilikua ni mwendo wa visima tu na barabara zenye mashimo km mabwawa ya samaki, mwamba kaingia miaka mi3 tu kamaliza biashara.
R.I.P Mwamba.
 
Yaani Mheshimiwa alikuwa na msimamo wa chuma cha pua, Mlingoti chuma, bendera chuma chama chuma na kiongozi ndio usiseme, aliiweza Tanzania na kuiweka katika mstari. Huduma zilikuwa straight forward hakuna kuzunguushwa zunguushwa, leo Tanzania imerudi kuliko zamani.

Hakuna kinachofanyika zaidi ya teuzi zisizo na miguu wala vichwa, basi mliopo jitahidini japo mlikubali hili la Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi. Wananchi walikuwa wapo poa kabisa kwani mambo yao yalikuwa yakifanikiwa bila mizengwe.

Leo akifufuka kama Yesu sujui atasema kitu gani, waliopo wanazidi kuvuruga yaani hata Gwajima sasa anaitesa serikali? Ndugu zangu Samia zigo haliwezi.
 
akifufuka si ataitwa msukule! unafkiri nani atalaumiwa
Unajua fikra na mawazo ya Mheshimiwa ilikuwa kuifikisha Tanzania pale ambapo mwananchi wa kawaida atakuwa anafurahia maisha ya uswahilini na hana kudhalilishwa wala kubugudhiwa na anaheshimika kwenye taasisi zote,

Wakati wake mwananchi hata alievaa mararu nguo za viraka akifika kwenye taasisi za serikali yake akipokelewa na hata kukaribishwa maji ya kunywa na haichukui muda anasikilizwa shida zake na kuahidiwa kufanyiwa kazi ,siku mbili ilikuwa unapata passport ,siku mbili unapata kadi ya Uraia au kitambulisho cha utaifa,leo nenda kajaribu utaambiwa mashine hazifanyi kazi na haijulikani zitatengenea lini maana kimeagizwa kutoka Japan na ndege siku hizi kama unavyojua haziendi kutokana na korona, njoo ukiulizia au tutakupigia simu.

Shida zimeanza kurudi na kuzaana,usilete habari za kisiasa hizo ni kazi kama kazi zingine mambo ya wanasiasa na majilabu na majigambo hayahusiani na shughuli za kiutawala.

Katika utawala na uongozi na usimamizi Mheshimiwa Magufuli aliweza. Ila huyu dada naona anazingua tu. Vyombo vya huduma za kijamii katika serikali yake zimeanza kusua sua.

Nikimtazama naona anavutwa na mkondo wa shughuli za kisiasa ambazo Magufuli alizipiga chenga na kuwaacha wapinzani wakipiga makelele kwenye vyumba.
 
Akifufuka na akaona yanayoendelea atakufa tena hapo hapo kwa hofu
 
Akifufuka hatapata muda wa kuongea na mtu kwani kila atakayekutana naye atakimbia kwa hofu! Mtu aliyekufa kufufuka!!!! Hatari!!!!
 
Yaani Mheshimiwa alikuwa na msimamo wa chuma cha pua, Mlingoti chuma, bendera chuma chama chuma na kiongozi ndio usiseme, aliiweza Tanzania na kuiweka katika mstari. Huduma zilikuwa straight forward hakuna kuzunguushwa zunguushwa, leo Tanzania imerudi kuliko zamani.

Hakuna kinachofanyika zaidi ya teuzi zisizo na miguu wala vichwa, basi mliopo jitahidini japo mlikubali hili la Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi. Wananchi walikuwa wapo poa kabisa kwani mambo yao yalikuwa yakifanikiwa bila mizengwe.

Leo akifufuka kama Yesu sujui atasema kitu gani, waliopo wanazidi kuvuruga yaani hata Gwajima sasa anaitesa serikali ? Ndugu zangu Samia zigo haliwezi.
Sema hayati jk Nyerere akifufuka atasema nn!!
 
Nipeni huyu mama awe Makamu wangu,sio mnaona alivyo mweupe? Ninasema uongo ndugu zangu?
 
Back
Top Bottom