Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?
Aisee.
JamiiForums-85016129.jpg
 
Mtu akiwa Masikini ndio asilipi Kodi?
Mtu akiwa Masikini ndio asitoe Zaka?

Hakuna kitu Kama hicho.
Kodi iwekwe katika mfumo wa percentage.
Kama ni 10%
Basi Masikini mwenye Tsh 1000/= atatoa Kodi Tsh 100/=
Tajiri mwenye 1,000,000/= atatoa 100,000/=

Magufuli alikuwa kiongozi ambaye alitaka kuleta ubaguzi katika ujenzi wa Nchi. Alitaka kuwapendelea Masikini Jambo ambalo Kwa Kiongozi sio sifa njema.

Biblia inasema;

Kumbukumbu la Torati 25:13
Usiwe na mawe ya kupimia mbalimbali, kubwa na dogo, katika mfuko wako.

Kumbukumbu la Torati 25:14
Usiwe na vipimo mbalimbali, kikubwa na kidogo, katika nyumba yako.
Kumbukumbu la Torati 25:15
Uwe na jiwe timilifu la haki, uwe na kipimo kitimilifu cha haki; zipate kuwa nyingi siku zako, katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako.
Kumbukumbu la Torati 25:16
Kwa kuwa wote wayatendao mambo kama haya, wote watendao yasiyo haki, ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako.

Kodi lazima kila mtu alipe Kwa uwezo wake. Zikiletwa Tozo kila mtu alipe Kwa uwezo wake.
Sio huyu alipe alafu mwingine asilipe.

Biblia inamaliza Kwa kusema;

Mambo ya Walawi 19:15
Msitende yasiyo haki katika hukumu, usimpendelee mtu maskini, wala kumstahi mwenye nguvu; bali utamhukumu jirani yako kwa haki.

JPM amepumzika tuache apumzike lakini kuhusu clip hiyo Hakuwa sahihi, kwamba mtu akiwa Masikini basi ndio apendelewe au asikupe Kodi kisa umasikini wake.

Kodi iwekwe katika mfumo rahisi na nafuu Kwa kila mtu, katika namna ya percentage.
Ukiuza mchicha wa Buku basi hamsini iwe Kodi. Fresh.

Huko kunaitwa kuwajibika
 
Huyu mzee alikua comred haswaaa... na alijua kuinyoosha hii nchi nidhamu makazini ilirejea kwa kiasi chake, ubadhilifu ulipungua kama sio kuisha kabisa

Mafisadi, walanguzi, wezi, wa kwepa kodi, vibaraka wa mabeberu alijua kuwawajibisha vilivyo.

Naamini walipambana sana mpaka mauti yakamkuta , Pamoja na yote ipo siku walamba asali ita wapalia manina zao. [emoji849]
 
kweli mama anaweza kuwa na mapungufu yake ila magu hapana aicee....never never & never again alisikika mtu mmoja
 
Magufuli hapana mnisamehe tu. Alikuwa mkali ikafikia hatua hata watu wa karibu yake kama idara ya usalama wa taifa ilianza kufanya kazi kwa matakwa yake, kuteka watu, kuua, kutesa, kubambikia makosa ya jinai, uhujumu uchumi nakadhalika. Kuna machache alithubutu ila am sure jamaa angeendelea kuwepo kuna watu tungeumia mara mbili. Amesababisha hadi leo tunateseka kitaa sababu yake plus ndugu zetu he was good at some point but at the same time was evil. Nilifurahi sana alipodanja

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom