Mimi hua sishushi vioo hata kidogo....inakera pale unapompa mtu lift halafu ile kupanda tu anaanza na kupunguza au kuongeza sauti ya redio,akimaliza hapo anabonyeza button ya vioo sasa kwa vile ume-lock button utasikia "bro shusha vioo basi tupate fresh air".
Sent from my iPhone using JamiiForums
RRONDO;
umewahi kukaa kwenye foleni??? Kama upo Highway sawa, pandisha vioo, weka AC. Hapo sawa sawia kabisa, lakini kwenye foleni, mafuta ya lita 2 uweke AC?
Ni kweli kabisa langu cylinder 6 ukikaa kwenye foleni ya Mbagala mjini basi viwese vyote vinakwisha hapo.
Hivi sasa AC ina matatizo sifungui basi nina afueni kubwa ya mafuta.
Kwa muda mrefu watu wengi wamekuwa wakiamini ukitumia AC unatumia mafuta mengi kuliko ukiendesha bila AC[vioo wazi].
Kiufundi ili AC ifanye kazi inahitaji nguvu ya ziada kutoka kwenye engine ili compressor izunguke,sitaingia kiundani kwasababu mimi sio mtaalam wa AC. Na kwa kuzingatia hili watu wengi wanaamini ukitumia AC unatumia mafuta mengi kuliko ukiendesha bila AC.
Hili si kweli. Ukitumia AC gari inatumia nguvu zaidi LAKINI ukiacha vioo wazi gari inatumia nguvu zaidi ya ukifunga vioo na kuwasha AC. Vioo vikiwa wazi gari inatengeneza kitu kinaitwa 'DRAG' yaani upepo unajaa ndani ya gari na kuifanya iwe nzito kwahio inatumia nguvu nyingi kutembea kuliko ukifunga vioo na kutumia AC.
Kwenye speed ya 80kph ukifungua vioo unatumia mafuta 20% zaidi ya ukifunga vioo na kuwasha AC. Kwa maelezo haya nahitimisha kuwa UKITUMIA AC GARI INATUMIA MAFUTA KIDOGO KULIKO USIPITUMIA AC NA KUACHA VIOO WAZI.
CC: OLESAIDIMU MANI Kaizer Kalamzuvendi Titans
Kwa hypothesis yako Mabasi yote wangekuwa wanatumia AC ili kubana mafuta.
Ila kama unaenda safari ndefu kwa uzoefu wangu ukiwasha AC mafuta hutumika sana kuliko kufungua vioo hata hiyo dragforce unayosemea ukiwa katika spidi kubwa hutaweza kufungua vioo hadi mwisho
ukikaa kwenye foleni as long as engine iko on inakula mafuta.....hapa unajipa moyo tu
Siyo kujipa moyo lakini hiyo ni uhakika maana wakati AC ilipokuwa inanguruma ilikuwa inakula kama lita 50 diesel kwa wiki, lakini sasa bila AC zinabaki na kuendelea mpaka wiki ya pili.
Na dereva ni mimi tu kwa hivyo kufanya monitoring ni rahisi.
Ni kweli kabisa langu cylinder 6 ukikaa kwenye foleni ya Mbagala mjini basi viwese vyote vinakwisha hapo.
Hivi sasa AC ina matatizo sifungui basi nina afueni kubwa ya mafuta.
mimi kigari changu hata sijuagi vioo vinafunguliwaje nijuzeni wadau.full kipupwe.
Mimi hua sishushi vioo hata kidogo....inakera pale unapompa mtu lift halafu ile kupanda tu anaanza na kupunguza au kuongeza sauti ya redio,akimaliza hapo anabonyeza button ya vioo sasa kwa vile ume-lock button utasikia "bro shusha vioo basi tupate fresh air".
Umenena mkuu, watu wengine si wastaarabu kabisa anapewa lift na masharti juu.
Mkuu asante kwa taarifa yako japo na mimi nilishaisoma miaka 4 iliopita kwenye link hiyo hiyo uliotupa. Humu kuna watu wabishi wanaamini walichozoea na stori za mitaani kua AC inakula sana mafuta.
Japo wameshauri kwenye hiyo makala kua kama unaendesha kwenye jam kubwa gari inapokwenda kwa mwendo mdogo sana ni bora ukashusha vioo na kuzima AC kama unataka kusevu mafuta .