Je utumwa ilikua mipango ya Mungu ana ilitokea bahati mbaya?

Je utumwa ilikua mipango ya Mungu ana ilitokea bahati mbaya?

Kwa hiyo mungu hahusiki kabisa mkuu na yaliyotokea na wala hakuyajua?
Inategemea unaamini nini kama ni Imani (huo ndio ukweli wako wala mimi sina jinsi ya kukupinga) sababu hicho ndicho unachoamini hata ukiwa unaamini kwamba wewe ndio Muumba umekuwa incarnated kama wewe....

Ila tukija kwenye logic, known facts na vitu sensible basi hata uwepo wa mpenda wote na mpenda Amani haviendani na kinachoendelea sasa hivi...; Anyway kama ni kweli Mbinguni tutakuwa tunachoma wenzetu au tunakula bata wakati wengine wanapata shida bora niendelee kulala / kufa kuliko kushiriki kwenye hio barbarism
 
Story za Mungu zimetungwa na binadamu baada ya kujiuliza maswali mengi asiyoweza kuyapatia majibu yake , mpka sasa hakuna hata dalili ya kiumbe kinachoitwa Mungu wala shetani.
1707273722415.jpg
 
Watu wa dini husema kila kitu ni mipango ya Mungu. Kwamba hakuna jambo linatokea tu from no where, lazima lilishapangwa kutokea huko kabla.

Sasa ningependa kufahamu, je utumwa ambao tulifanyiwa waafrika kwa karibu niaka 400 na mataifa mengine ya Ulaya na Asia, ilikua imepangwa hivyo kwamba waafrika tutachukuliwa utumwani ama ilitokea bahati mbaya?

Kila mtu anajua maovu na mabaya ambayo waafrika tulitendewa chini ya utumwa, vizazi vyetu vilivyotangulia walifanyiwa unyama usio na kifani, mfano kulishwa simba huku wakiwa hai, watoto wao kulishwa mamba na kenge wa kufungwa na matukio mengine mabaya mabaya.

Haya yote yalitokea chini ya uangalizi wa Mungu, kwa maana yakitokea huku Mungu akiwa anaangalia na kushuhudia huo unyama ulitokea kwa watu weusi.

Swali langu ni kwamba, je utumwa kwa watu weusi ilikua ni jambo lililokua tayari limepangwa na Mungu kutokea ana lilitokea bahati mbaya tu?
Vipi kuhusu Papa na baraka zake? Ni mpango wa shetani?
 
Back
Top Bottom