Tupe figures.Hapana, wahindi wapo 1.5B, na Tz ndio tuna export zaidi India kuliko nchi yeyote duniani, kwa hio utaona ni suala jema sana kuwa na mahusiano nao mazuri ili kuweza kuongeza biashara baina yetu,
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tupe figures.Hapana, wahindi wapo 1.5B, na Tz ndio tuna export zaidi India kuliko nchi yeyote duniani, kwa hio utaona ni suala jema sana kuwa na mahusiano nao mazuri ili kuweza kuongeza biashara baina yetu,
Sio kuwa nyie mmeshindwa kujiendeleza hasha
Ni umasikini changanya na uroho na wizi, husda, uzembe, uvivu, kutosaidiana na kukataa maendeleo kabisa
Laiti ungejua wahindi wanavyofanya kazi na kujituma usingeleta haya bali ungeenda na kuwasoma kidogo tu
Mimi najua matajiri wakubwa wengi sana duniani na wahindi wamo sana
Kwa mfano UK pekee kuna billionaires 22 na anaeongoza utajiri UK anaitwa Gopi Hinduja hawa kama ni majizi au wanaiba serikali ya hapa haina utani na kukwepa tax na wahindi wanalipa kodi zao kama wengine
Wapo matajiri hapa kama Prakash Lohia tycoon huyu na Muhsin na Zuber Issa hawa ndugu wana supermarkets za Asda na wanamiliki filling Station na convenient stores 🇺🇸, Australia, Europe na 🇬🇧 na wameajiri watu Elfu 44
Hawa ni wawili tu katika 22 matajiri sasa imagine wote hao wameajiri watu wangapi duniani?
Sisi hata vyungu hatuwezi kutengeneza tumekalia majungu tu na kubinua midomo
Fursa hizi ni za kulilia Ulaya wanaleta makampuni kila kukicha na sasa wanawapa wachina kutengeneza magari ya Umeme
Nyie kama mna akili waiteni wahindi watengeneze kiwanda kikubwa cha Batteries za magari ya Umeme na kuajiri hata vijana 1000 acheni roho mbaya na umasikini
Wanangu mliopo humu hamjambo?
Leo nimesoma habari kuwa Muigizaji wa kihindi Sanjay Dutt atapewa ubalozi wa heshima ili kuitangaza Tanzania India. Kilichonishangaza ni ile hali ya Dutt mwenyewe kusema kuwa amekuwa akija Tanzania kila mwaka lakini hajawahi kuwa na hamu ya kuitangaza kama walivyo magabacholi wenzake ambao hupenda kuinyonya na kuwabagua watu wake pamoja na kwamba walikuja maskini wanatoka matajiri.
Je kwa tamaa na upofu, Tanzania imeamua kujigeuza koloni la wahindi wazungu na waarabu upya? Rais alipoteza mabilioni ya shilingi akifanya kazi za waziri wa utalii kwenye Royal isiyo royal chochote tua huku Marekani. Juzi ametuletea Deep Weed kuendesha bandari zetu. Kama haitoshi, sasa tunaletewa wahindi na kuwapa ubalozi wa heshima. Je huu ubalozi hauwezi kutumika kama chambo cha kutunyonyea kama alivyofanya Chavda alipopewa vibali haramu kuishi nchini wakati hatakiwi?
Je wewe kama mwenye nchi unasemaje kuhusu huu ubalozi wa heshima wenye kutia mashaka? Wahindi na ubaguzi wao wanaweza kufanya utalii gani Tanzania zaidi ya kuja kupiga madili? Je tumekuwa wa hovyo hivi kiasi cha kushindwa kujitangaza? Nini kazi ya wizara husika kama haiwezi kitu hadi itegemee wamanga na magabacholi?
Je tumeamua, kwa hiari, kujigeuza koloni la wageni kwa sababu ya ujinga na umaskini wetu?
Naomba kuwasilisha.
---
Dar es Salaam. Serikali imeeleza sababu ya kumwandaa kuwa balozi wa heshima msanii wa filamu kutoka nchini India, Sanjay Dutt kutokana na mapenzi yake kwa nchi na kuwa na wafuasi wengi watakaoona na kusikia kuhusu fursa za utalii nchini.
Hayo yameelezwa jana Septemba 18 na Mkurugenzi wa Utalii wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Thereza Mugobi baada ya kumpokea msanii huyo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam.
Amesema lengo la kumchagua Dutt ni kuingia kwenye soko la India yenye idadi ya zaidi ya watu 1.4 bilioni.
“Msanii huyu ni mkubwa nchini India, ukifuatilia mitandao yake ya kijamii ana wafuasi zaidi ya 200 milioni. Kwa hiyo akituma kuhusu Tanzania, fikiria kuhusu wafuasi wote hao na siyo Wahindi peke yake bali pia ni dunia nzima, hata mimi pia ni mfuasi wake. Hivyo tunaamini kwamba kituo cha Tanzania kitasikika katika soko la India na soko kubwa la Asia, ambako pia tunalenga kufikia huko,” amesema.
Maelezo hayo yameungwa mkono na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Damas Mfugale akisema kwa kumchagua msanii huyo watafanikiwa kupenya kwenye soko la utalii la India.
“India ina idadi ya watu 1.4 bilioni na ni soko la watu wanaopoenda utalii. Takwimu zinaonyesha kuwa kuna watu milioni 200 wanasafiri kwenda nje kweye maeneo mbalimbali, kwa hiyo tumeliona kama ni soko la kimkakati.
“Huyu kuwa balozi wetu katika kutuwakilisha kama wananchi ni fursa kubwa kwetu. Tumeweka malengo kuwa ifikapo mwaka 2025 tunatakiwa tuwe tumefikisha watalii milioni tano, kwa hiyo katika kipindi cha miaka mwili mitatu ijayo tukiongeza watalii milioni 1.5 kutoka India tutakuwa tumefikisha malengo,” amesema.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), idadi ya watalii kutoka nje ya nchi waliotembelea vivutio mbalimbali vya utalii katika kipindi cha Januari hadi Mei 2022 wameendelea kuongezeka hadi 458,048 ikilinganishwa na watalii 317,270 walioingia nchini kipindi kama hicho mwaka 2021, ikiwa ni sawa na asilimia 44.4.
Akizungumzia ujio wake, msaanii huyo amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuweka mazingira wezeshi ya utalii na amekubali ombi la kuwa balozi wa heshima kwa kuwa anaipenda Tanzania.
“Nimekuwa nikija Tanzania kwa miaka 30 iliyopita, nakuja kila mwaka, naipenda hii nchi. Sikuwahi kuitangaza hii kwa miaka yote lakini kwa sasa nitaitangaza Tanzania sana na nitaitambulisha kwa mashabiki wangu, watu wa nchi yangu na watu wengine wote duiani,” amesema.
Amesema mbali na maeneo maarufu kwa utalii kama hifadhi ya Serengeti na Ngorongoro, anakusudia pia kutangaza maeneo mapya kama Katavi na Ruaha.
Mmoja wa wenyeji wa msanii huyo ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Africab Group Tanzania, Yusuf Hatimali amesema ujio wa msanii huyo ni matokeo ya Rais Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi ya kutangaza utalii duniani.
“Kwa hiyo matunda yote haya ni kutokana na filamu ya Royal tour, ndio tunaona msanii huyu amekuja Tanzania. Kwa kuwa ana wafuasi wengi, ataziweka utalii wetu kwenye Instagram watu wote duniani wataona, kwa hiyo atatusaidia Watanzania,” amesema.
Umetawaliwa sana na ubaguzi,ubaguzi unakutafuna bila hata ya wewe kujijua,
Unaonekana ni mtu uliyejikatia tamaa ya maisha,una mawazo ya kimasikini sana.
African victims of racism in India share their storiesUmetawaliwa sana na ubaguzi,ubaguzi unakutafuna bila hata ya wewe kujijua,
Unaonekana ni mtu uliyejikatia tamaa ya maisha,una mawazo ya kimasikini sana.
African victims of racism in India share their storiesKama wewe huzioni fursa wenzako wanaziona na kuzitumia.
Wacha roho mbaya.
African victims of racism in India share their storiesMfumo wa caste siyo wakubaguana ni sawa na uliopo kanisani, kuna askofu, kuna padri, kuna shemasi, kuna wazee wa kanisa,kuna mabikira feki na kuna wajinga ndiyo waliwao.
African victims of racism in India share their storiesEndelea tu na hizi ngonjera zako hapa JF halafu uje ulalamike unanyonywa wakati wenzako wanachapa kazi wewe unaandika ngonjera,umasikini ndio unakufanya uone kila aliyefanikiwa ni mwizi,fanya kazi wewe.
African victims of racism in India share their storiesHistoria yako mbovu kupita kiasi, Muingereza kaja hapa kamkuta Muhindi yupo.
Wewe unajinyonya nafsi yako tu.
African victims of racism in India share their storiesToka usingizini usije ukawapa watu wengine kazi ya kukulea uzeeni mwako,chuki za ukabila haziwezi kukusaidia kitu,
Amini aliwafukuza Wahindi Uganda,je baada ya wahindi kuondoka, Uganda kilibadilika kitu gani? Wale wahindi walienda UK na Canada wakaendelea na biashara na life likaenda,Muhindi ni mfanyabiashara hata umpeleke wapi,
Chuki zitakuletea vidonda vya tumbo tu,tafuta fursa kamata fursa.
African victims of racism in India share their storiesNyie ndo kigwangala alikuwa anawazubgumzia kwamba mnashida mbabet tu na stress za maisha kibao
African victims of racism in India share their stories"Baniani mbaya kiatu chake dawa".
Kumbuka wakati nchi hii inapata uhuru, madakatari, mapolisi, viwandani, wajenzi, mapolisi, wenye maduka. wahasibu, wapigania uhuru wengi walikuwa hao unaowaita leo majina ya kiajabu ajabu.
Wabunge, mawaziri, wachumi, wafanyabiashara tunao tokea uhuru wa nchi hii mpaka leo hii.
Pengine mama;ko au baba'ko walipozaliwa kama ni hospitali basi kama si daktari, mkunga alikuwa ni hao hao leo unawaita majina ya kiajabu.
Kama hiyo haitoshi, mpaka mapinduzi ya kwanza aliyofanyiwa Nyerere mwanajeshi aliyedinda kishujaa na kuzuwia wanajeshi walioasi mpaka lilipokuwa jesshi la Uingereza kwa manowari, alikuwa ni Mhindi aitwae Kanal Kashmir.
Ikiwa wazee wako wa nchi hii wote, kuanzia Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Mwendazake na sasa mama Samia wanawaheshimu na kuwakubali, wewe ni kama nani wa kuwa na chuki za kijinga?
Hivi wewe umetokea mkoa upi Tanzania hii?
Leo hao ndiyo wamekuwa wabaya? Kwa lipi zaidi walilokufanyia au kukosea?
African victims of racism in India share their storiesWahindi wako mbali wewe kijana. Wanaongoza ma giant ya makampuni duniani, waziri mkuu wa uingereza ni muhindi na asili kutoka Tanzania. Fikiria Tanzania ikipata kiongozi kama huyo.
Kuwa na uhusiano na wahindi ni kwa manufaa ya Tanzania.
Hawa wasomi wetu uchwara hatukuona la maana wamefanya na sasa unataka kusingixia wageni.
Dubai 90% ya watu wake ni wageni wakiwemo wahindi matajiri wawekezaji na angalia miujiza Dubai iliofanya kwa muda mchache.
Punguza dukuduku moyoni la ubaguzi na roho mbaya utaona faida ya kujihusisha na wenye akili.
African victims of racism in India share their storiesWalikubagua nini? Au una shemeji wa kihindi kakutenda?
Upo mkoa gani?
Nijuavyo wazungu ndiyo walitutawala hapa wakatubaguwa.
Babu yako kanisa la mzungu alikuwa haingii, wewe je?
Mkuu ubaguzi upo kila sehemu duniani![]()
African victims of racism in India share their stories
‘The law of mobs is always there,’ says one student, describing racist attacks on Africans in Greater Noida.www.aljazeera.com
Maendeleo na ubaguzi ni vitu viwili tofauti kabisa![]()
African victims of racism in India share their stories
‘The law of mobs is always there,’ says one student, describing racist attacks on Africans in Greater Noida.www.aljazeera.com
Prejudice, Discrimination and Racism against Africans and Siddhis in India - Cambridge Scholars Publishing
Prejudice, Discrimination and Racism against Africans and Siddhis in India - Cambridge Scholars Publishingwww.cambridgescholars.com
Mkuu, mimi niliishi pale UK na kwa kweli mfumo wao wa biashara haujali mtu atoka wapi ili mradi ana pesa ya kuwekeza na atatoa ajira kiasi gani na atalipa kodi.Sio kuwa nyie mmeshindwa kujiendeleza hasha
Ni umasikini changanya na uroho na wizi, husda, uzembe, uvivu, kutosaidiana na kukataa maendeleo kabisa
Laiti ungejua wahindi wanavyofanya kazi na kujituma usingeleta haya bali ungeenda na kuwasoma kidogo tu
Mimi najua matajiri wakubwa wengi sana duniani na wahindi wamo sana
Kwa mfano UK pekee kuna billionaires 22 na anaeongoza utajiri UK anaitwa Gopi Hinduja hawa kama ni majizi au wanaiba serikali ya hapa haina utani na kukwepa tax na wahindi wanalipa kodi zao kama wengine
Wapo matajiri hapa kama Prakash Lohia tycoon huyu na Muhsin na Zuber Issa hawa ndugu wana supermarkets za Asda na wanamiliki filling Station na convenient stores 🇺🇸, Australia, Europe na 🇬🇧 na wameajiri watu Elfu 44
Hawa ni wawili tu katika 22 matajiri sasa imagine wote hao wameajiri watu wangapi duniani?
Sisi hata vyungu hatuwezi kutengeneza tumekalia majungu tu na kubinua midomo
Fursa hizi ni za kulilia Ulaya wanaleta makampuni kila kukicha na sasa wanawapa wachina kutengeneza magari ya Umeme
Nyie kama mna akili waiteni wahindi watengeneze kiwanda kikubwa cha Batteries za magari ya Umeme na kuajiri hata vijana 1000 acheni roho mbaya na umasikini
Watanzania walikuwa wakiambiwa sie si maskini hawakuwa wanaamini.Maendeleo na ubaguzi ni vitu viwili tofauti kabisa
Sasa tutaacha hata kununua bajia zao kisa ubaguzi
Ubaguzi unaweza kupambana nao au ku ignore ila jukumu letu na sisi tuwe maendeleo basi
Hivi tutakuwa masikini mpaka lini?
Asante mwanangu. Nakubaliana nawe kuwa ni waafrika pekee ambao hawabagui watu kwa rangi isipokuwa upuuzi mwingine kama dini, kabila na kipato. Nimetoa ushahidi ili kuwakata ngebe waliokuwa wanadhani naongea kwa sababu ya chuki. Ubaguzi kwenye biashara ndiyo usimabiwe. Hebu nenda Kariakoo au posta uanzishe biashara karibu na wahindi utajua nisemacho. Jiulize wahindi wanavyonunuzana wakiepuka waafrika hata kutotaka wafanye biashara kama zao kama siyo roho mbaya na ubaguzi vya kunukaMkuu, mimi niliishi pale UK na kwa kweli mfumo wao wa biashara haujali mtu atoka wapi ili mradi ana pesa ya kuwekeza na atatoa ajira kiasi gani na atalipa kodi.
Pili, mtu ambae ataendesha na kusimamia hiyo biashara si mtu wa kawaida ni vichwa khasa.
Kwa mfano yapo yale maduka madogomadogo yaitwa "Discount Chains" mojawapo ni Poundland.
Poundland huuza kila kitu kwa pauni moja tu! lakini ina maduka nchi nzima na mwaka 2016 ilinunuliwa na kampuni ingine yaitwa Pepco Group. Hawa Pepco Group waitwa kitaalam Institutional Investors yaani ni wawezekezaji ambao wamejikita katika biashara hizo za maduka ya bei ndogo.
Hawa Pepco nao ni kampuni tanzu tu kwamba nao iko chini ya kampuni kubwa ya kimataifa iitwayo Steinhoff International ambayo ni ya Afrika Kusini. CEO wa zamani wa Asda ndie asimamia Pepco Group na hii kampuni imeajiri watu 30,000.
Poundland UK ana maduka yapatayo 500 na hawa Pepco Group pia wana kampuni ingine iitwayo Dealz ipo Ireland.
Kwenye hizi biashara ni lazima utumie kampuni zenye mitaji mikubwa au Equity Firms ambazo zote hupata fedha kutoka kwa mazee Rothschild.
Walichofanya wenzetu wahindi na waarabu au wachina ni kujipenyeza hadi ndani yaani "centre of operations" ya hizi shughuli za fedha na ndani kabisa ya viambaza vyao hawa maglobalists.
Sie waafrika yatubidi kwanza tufanye mapinduzi makubwa ya kiakili na kijamii ijitambue kisha tujiweke sawa na tuone twaanzia wapi.