Je, uwekezaji unaifanya Tanzania koloni jipya la kujitakia?

Hapana, wahindi wapo 1.5B, na Tz ndio tuna export zaidi India kuliko nchi yeyote duniani, kwa hio utaona ni suala jema sana kuwa na mahusiano nao mazuri ili kuweza kuongeza biashara baina yetu,
Tupe figures.
 
Sio kuwa nyie mmeshindwa kujiendeleza hasha
Ni umasikini changanya na uroho na wizi, husda, uzembe, uvivu, kutosaidiana na kukataa maendeleo kabisa

Laiti ungejua wahindi wanavyofanya kazi na kujituma usingeleta haya bali ungeenda na kuwasoma kidogo tu

Mimi najua matajiri wakubwa wengi sana duniani na wahindi wamo sana
Kwa mfano UK pekee kuna billionaires 22 na anaeongoza utajiri UK anaitwa Gopi Hinduja hawa kama ni majizi au wanaiba serikali ya hapa haina utani na kukwepa tax na wahindi wanalipa kodi zao kama wengine

Wapo matajiri hapa kama Prakash Lohia tycoon huyu na Muhsin na Zuber Issa hawa ndugu wana supermarkets za Asda na wanamiliki filling Station na convenient stores 🇺🇸, Australia, Europe na 🇬🇧 na wameajiri watu Elfu 44

Hawa ni wawili tu katika 22 matajiri sasa imagine wote hao wameajiri watu wangapi duniani?

Sisi hata vyungu hatuwezi kutengeneza tumekalia majungu tu na kubinua midomo

Fursa hizi ni za kulilia Ulaya wanaleta makampuni kila kukicha na sasa wanawapa wachina kutengeneza magari ya Umeme
Nyie kama mna akili waiteni wahindi watengeneze kiwanda kikubwa cha Batteries za magari ya Umeme na kuajiri hata vijana 1000 acheni roho mbaya na umasikini
 
 
 
African victims of racism in India share their stories

Prejudice, Discrimination and Racism against Africans and Siddhis in India - Cambridge Scholars Publishing
 
African victims of racism in India share their stories

Prejudice, Discrimination and Racism against Africans and Siddhis in India - Cambridge Scholars Publishing
 
African victims of racism in India share their stories

Prejudice, Discrimination and Racism against Africans and Siddhis in India - Cambridge Scholars Publishing
 
Mkuu ubaguzi upo kila sehemu duniani
Hujaona news leo kuna polisi uk alimpiga risasi jamaa black baada ya maandamano ya kila wakati na kudai haki ndio wameamua kumpeleka mahakamani
Jamaa alieuwawa alikuwa anaitwa Chris Kaba, 24
Racial discrimination ipo hata kwetu na kila siku tunayaona hata kwenye makabila yetu wenyewe kwa wenyewe kwa hiyo usiwasontee kidole wao tu
Mbona tunawaaita kanjibai kila siku na kuwasema kuwa wanaachia shit kwenye mitaro wakati wa mvua? 😄
 
Maendeleo na ubaguzi ni vitu viwili tofauti kabisa
Sasa tutaacha hata kununua bajia zao kisa ubaguzi
Ubaguzi unaweza kupambana nao au ku ignore ila jukumu letu na sisi tuwe maendeleo basi
Hivi tutakuwa masikini mpaka lini?
 
Mkuu, mimi niliishi pale UK na kwa kweli mfumo wao wa biashara haujali mtu atoka wapi ili mradi ana pesa ya kuwekeza na atatoa ajira kiasi gani na atalipa kodi.

Pili, mtu ambae ataendesha na kusimamia hiyo biashara si mtu wa kawaida ni vichwa khasa.

Kwa mfano yapo yale maduka madogomadogo yaitwa "Discount Chains" mojawapo ni Poundland.

Poundland huuza kila kitu kwa pauni moja tu! lakini ina maduka nchi nzima na mwaka 2016 ilinunuliwa na kampuni ingine yaitwa Pepco Group. Hawa Pepco Group waitwa kitaalam Institutional Investors yaani ni wawezekezaji ambao wamejikita katika biashara hizo za maduka ya bei ndogo.

Hawa Pepco nao ni kampuni tanzu tu kwamba nao iko chini ya kampuni kubwa ya kimataifa iitwayo Steinhoff International ambayo ni ya Afrika Kusini. CEO wa zamani wa Asda ndie asimamia Pepco Group na hii kampuni imeajiri watu 30,000.

Poundland UK ana maduka yapatayo 500 na hawa Pepco Group pia wana kampuni ingine iitwayo Dealz ipo Ireland.

Kwenye hizi biashara ni lazima utumie kampuni zenye mitaji mikubwa au Equity Firms ambazo zote hupata fedha kutoka kwa mazee Rothschild.

Walichofanya wenzetu wahindi na waarabu au wachina ni kujipenyeza hadi ndani yaani "centre of operations" ya hizi shughuli za fedha na ndani kabisa ya viambaza vyao hawa maglobalists.

Sie waafrika yatubidi kwanza tufanye mapinduzi makubwa ya kiakili na kijamii ijitambue kisha tujiweke sawa na tuone twaanzia wapi.
 
Maendeleo na ubaguzi ni vitu viwili tofauti kabisa
Sasa tutaacha hata kununua bajia zao kisa ubaguzi
Ubaguzi unaweza kupambana nao au ku ignore ila jukumu letu na sisi tuwe maendeleo basi
Hivi tutakuwa masikini mpaka lini?
Watanzania walikuwa wakiambiwa sie si maskini hawakuwa wanaamini.

Ila kiukweli umaskini upo vijijini kuanzia barabara mbovu, ukosefu wa umeme, na hali duni ya maisha.
 
Asante mwanangu. Nakubaliana nawe kuwa ni waafrika pekee ambao hawabagui watu kwa rangi isipokuwa upuuzi mwingine kama dini, kabila na kipato. Nimetoa ushahidi ili kuwakata ngebe waliokuwa wanadhani naongea kwa sababu ya chuki. Ubaguzi kwenye biashara ndiyo usimabiwe. Hebu nenda Kariakoo au posta uanzishe biashara karibu na wahindi utajua nisemacho. Jiulize wahindi wanavyonunuzana wakiepuka waafrika hata kutotaka wafanye biashara kama zao kama siyo roho mbaya na ubaguzi vya kunuka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…