Je, Uzinduzi Royal Tour ungekuwa na maana kama Rais Samia angetua kwa Dreamliner & ATC kuzindua Direct Flights from DAR-JFK-DAR/JRO-JFK-JRO?

Tuna Dreamliner na Airbus 2 zote ni jet engine, bombardier ya jet unakuja. kati ndege zetu 15, 5 ndio za pangaboi, 10 ni jet engine.
P

Mkuu, Mayalla, it’s more complicated than that! Air route authority is valuable; haitolewi kirahisi rahisi, kwasababu ina direct impact on the market shares of the major players. Remember, home countries of the major players in the aviation industry have bilateral treaties that essentially serve to protect the interests of the major players involved. Kwa ATCL kupewa hiyo air route authority itabidi iruke viunzi vingi.
 
Kaka pasco naomba kazi kwenye kampuni yako, kijana wako nina professional ya PR.
 
Kuingiza ndege USA direct kutoka Tanzania sio rahisi kama unavyodhani. Kenya walikua na hiyo ruhusa sijajua kwa sasa wanaendeleaje.
Kuna michakato mingi sana ya kiusalama before kupewa hicho kibali.

Nitashangaa sana kama hata hili haulifahamu.
Ni kweli kuwa na direct route to the US kuna mambo mengi ya kuhitimu hasa kiusalama. Lakini penye nia pana njia. Kenya wao waliweza, lakini wakapumzika wakati wa Corona. Na sasa wameanza tena na wanaendelea vizuri. Wao KQ pia wanarusha Dreamliner yao direct. Jumamosi May 7 nitakuwa mmoja wa abiria kwenye KQ kutoka Nairobi mpaka JFK
 
Nakuomba siku hiyo ikitangazwa tangazo la Ku board, nakuomba simama pembeni ya boarding gate, then wahesabu abiria walio board from Dar, wewe uwe the last to board, ukifika ndani, wahesabu abiria business wao wana board from lounge na VIP, wajumlishe na wale wa economy, then get the total, ili tuwaeleze hawa vichaa wetu wa ATCL, what a wasted opportunity they are missing!. Wakenya wanatubebea watalii wetu, wanatusombea kazi zetu, kule Rombo wanatubebea wake zetu, sasa hata kwenda Marekani, wanatubebea abiria wetu!, kwenye soko la AGOA wanatuingizia bidhaa zetu, hata kwenye kuutangaza utalii wa mlima Kilimanjaro, wanatutangazia mlima wetu kuwa uko kwao, ila unapandwa upande wa Tanzania!. Watanzania tutaendelea kulala mpaka lini?.
P
 
P unasema kweli nilishangaa maajabu EK 726 inaondoka full. Na fikiria wale jamaa wanakomaa na DAR tu bhaasi. TZ watu wanasafir aisee...Bado Turkish, Oman, Fly Dubai, Egypt Air, KLM, Swiss Air, Rwandair, KQ, Air Zimbabwe, Uganda Airlines, Malawian Airlines,Ethiopian airlines etc
 
ATCL kwa sasa haina uwezo huo wa kupata slots ya direct flight to NY ama DC wacha mbwembwe ng’wanone
Hili ndio tatizo kubwa la sisi Watanzania, we don't believe in ourselves, always negative and negativity!. Ndege tunazo, fedha tunazo, mkataba wa anga huria tunao, tatizo lilikuwa moja tuu, kupata abiria wa kuishibisha hiyo direct flights to New York, Royal Tour inakwenda kufungua!, what else do we need?.
P
 
Hapo KQ ananuna maana ATC ikisimama ni maumivu kwake. Ona Route ya Mumbai inavyoleta Neema
 
Mkuu BRN ikianzishwa ni vyema uwepo/upewe nafasi.una mawazo mengi sana na wakupe uhuru wa kumleta yeyote ili ufanye kazi vyema.
 
Hiyo cha mtoto. Ipo ile ya Australia to US, masaa 21 non-stop.

Zamani hizo nilipanda ndege PANAM kutoka Dar Mpaka Dakar. Pale Dakar tukaconnect to New York. Kufika New York nikaambiwa safari yangu bado[ ilikuwa mara yangu ya kwanza kwenda U.S] masaa nane tena kutoka New York Mpaka Seattle!!

Sijasafiri safari ndefu namna hiyo tena!!!
 
Hongera sana Mkuu. Naamin kwa kusafir angalau mawazo yako si Kama ya kina Hawa vijana ambao hawajawahi kuvuka border
 
Ikawa hajazindulia Serengeti wala ngorongoro isipokuwa picha za Serengeti ..vivyo hivyo Dreamliner zetu hao wazungu wazione tu kwa picha kuwa tunazo na wakiwa na utashi zitawafuata tu
 
Mkuu bado ujajibu swali ..umesema mama alipaswa kuzindua na route na abiria ungempa kama ungepewa tenda ..Je una consistency ya kutoa hao abiria 500 kwa uzinduzi tu au kila siku ya route?Sidhani kama hao ATCL hawajaona hio fursa ukute wamechambua gharama za kuihudumia ndege kwenye hiyo route na abiria ambao wanaweza kuwapata wameona ni hasara …Tudadavulie
 
Mimi napenda safari za ku connect, ndege yangu ya sasa ni Quatar, wakati wa booking inaonyesha huna haraka hivyo connection ni more than 6 hours, ukifika Doha unakuwa shifted kwenye a 5 star hotel near airport na umelipwa full board. Unasafiri Kwa raha tuu.
Nikiamua kupanda KQ ni ili ku save money.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…