Je, Uzinduzi Royal Tour ungekuwa na maana kama Rais Samia angetua kwa Dreamliner & ATC kuzindua Direct Flights from DAR-JFK-DAR/JRO-JFK-JRO?


Hata mimi nilienda kupandia ndege Nairobi kutoka Dar
 

NIMEPENDAAA
 
Nice uchambuzi mzuri
 
Kuingiza ndege USA direct kutoka Tanzania sio rahisi kama unavyodhani. Kenya walikua na hiyo ruhusa sijajua kwa sasa wanaendeleaje.
Kuna michakato mingi sana ya kiusalama before kupewa hicho kibali.

Nitashangaa sana kama hata hili haulifahamu.
KQ wapo chali kwenye hiyo route, walijaza siku ya kwanza tu na sasa route wameifuta
 
Swali ni Kati ya Tanzania na Kenya, Nani wana abiria wengi wa US?. Ni sisi na ndio maana ndege ya direct inaanzia DAR, Nairobi to JFK.

Inachofanya KQ ni wamegundua fursa wakaichangamkia. Angalia kwenye utalii, Tanzania ndio tunaongoza Kwa vivutio vya utalii Ila half ya watalii wetu wanapitia Kenya!.

Kenya wanatutangazia mlima Kilimanjaro uko Kenya Ila kuupanda ndio unapandia Tanzania!. Sisi watalii wetu wa kupanda mlima Kilimanjaro wanashukia KIA ni 90 min to kupandia route ya Machame na 2 hrs route ya Marangu. Sasa Kenya wanajenga uwanja wa ndege pale Taveta, just 30 min drive to route ya Marangu!. Uwanja ukikamilika Nani watashukia KIA?.

Biashara ni kujipanga na matangazo
Tanzania lazima tuamke, kama Kenya wanaweza, kwanini sisi tushindwe?.
P.
 
Ningefurahi sana kama uzinduzi wa royal tour ungeanzia nyumbani kabla ya kuvuka boarder, nahisi ingependeza sisi wananchi kuwa mabalozi wa kwanza wa vivutio vyetu vya utalii.. Ila ni mawazo yangu tu
 
Ningefurahi sana kama uzinduzi wa royal tour ungeanzia nyumbani kabla ya kuvuka boarder, nahisi ingependeza sisi wananchi kuwa mabalozi wa kwanza wa vivutio vyetu vya utalii.. Ila ni mawazo yangu tu
Angefuturu burger saa ngapi sasa kama angezindua hapa.
Hiyo filamu ni moja ya kamba kati zile kamba zinazopaswa watu kula kwa urefu wake.

Urefu wa kamba ya mzindua filamu ni Marekani.
 
Dah hakika mkuu maana ilo jopo lililoenda america si la watu wachache
Wekeni orodha ya waliokwenda kwenye huo msafara tuone isiwe mnasingizia watu mwezi mtukufu wa Ramadhan mkifikiri hawawezi jibu shutuma zenu!
 
Kwanini isingeitwa "The Royal Safari". Hii ingeleta mashiko zaidi coz naona asilimia 90 ni mbugani.
 
Kila mtu ale urefu wa kamba yake wengi hapa kamba yetu inaishia kitongoji cha jirani Mama kamba yake hadi Newyork
 
Nyie si mlipandishaga wasanii mlima Kilimanjaro, mkakodia mademu zenu ndege wakaja mbugani uko eti mnatangaza utalii 😂😂😂😂 sema kigwangala sijui alituonaje watanzania dah eti Tanzania unforgettable
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…