Je, Uzinduzi Royal Tour ungekuwa na maana kama Rais Samia angetua kwa Dreamliner & ATC kuzindua Direct Flights from DAR-JFK-DAR/JRO-JFK-JRO?

Je, Uzinduzi Royal Tour ungekuwa na maana kama Rais Samia angetua kwa Dreamliner & ATC kuzindua Direct Flights from DAR-JFK-DAR/JRO-JFK-JRO?

Nakuomba siku hiyo ikitangazwa tangazo la Ku board, nakuomba simama pembeni ya boarding gate, then wahesabu abiria walio board from Dar, wewe uwe the last to board, ukifika ndani, wahesabu abiria business wao wana board from lounge na VIP, wajumlishe na wale wa economy, then get the total, ili tuwaeleze hawa vichaa wetu wa ATCL, what a wasted opportunity they are missing!. Wakenya wanatubebea watalii wetu, wanatusombea kazi zetu, kule Rombo wanatubebea wake zetu, sasa hata kwenda Marekani, wanatubebea abiria wetu!, kwenye soko la AGOA wanatuingizia bidhaa zetu, hata kwenye kuutangaza utalii wa mlima Kilimanjaro, wanatutangazia mlima wetu kuwa uko kwao, ila unapandwa upande wa Tanzania!. Watanzania tutaendelea kulala mpaka lini?.
P

Hata mimi nilienda kupandia ndege Nairobi kutoka Dar
 
Maiden trip ni excursion American tour kumsindikiza Mama kuzindua her movie The Royal Tour, na kazi itafanywa na a Tanzanian Tour Company na an American counterpart, the cost will be US $ 5,000 per person, Kwa Tanzania na US $. 10,000 for Americans, the cost cover a round trip, it includes US Visa, 5 days 4 nights in New York, 2** hotel,and a tourist hotel in Arusha Tanzania for US Tourists. My role ni publicity only kuhamasisha. Nitawapata [emoji817] Bongo Movies na Bongo Music Stars wakiongozwa na Mondi, Kiba, Chinga, Mpoto ToT etc. [emoji817] journalist, [emoji817] ma pedejee wa Bongo ambao hawawezi kupata US visa wenyewe. [emoji817] wana CCM kumsindikiza Mwenyekiti, na [emoji817] wajasiriamali. There will be two trips, ndege itakwenda na Watanzania, na kugeuza na 240 rich American tourist to Serengeti, Ngorongoro and Mt. Kilimanjaro.

The maiden trip ikifanikiwa tunaanza na a monthly. Na ili ndege isiende tupu naweza kuuza tuu a Disney Land School Trips Watanzania wanaosomesha watoto wao Academy, wengi watawalipia.

The only setback ni how to control the storeaways watakao taka kuzamia US!
P.

NIMEPENDAAA
 
Wanabodi,

Naendelea na zile makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa, makala ya Leo ikiwa ni makala ya swali la hypothetical question (swali la kufikirika), Kwa njia ya "thinking aloud", yaani unawaza kwa sauti.

Hii ni makala mwendelezo wa makala hii Hongera Rais Samia, Kwenda US, Kuhutubia UN, Safari ya Kuzindua Filamu Yako ya Royal Tour, Tunaomba Tukusindikize, Dreamliner Yetu Itue New York

Ambayo pia niliandikia makala kwenye gazeti la Nipashe

View attachment 2188185

Swali ni hili "Jee uzinduzi wa filamu ya Royal Tour, unaofanyikia nchini Marekani, upi ungekuwa na maslahi zaidi kwa taifa kama Rais Samia angetua nchini Marekani kwa dege letu la Dreamliner, huku ATC ikizindua Direct Flights from DAR-JFK-DAR/JRO-JFK-JRO? au kuendelea kwenda kwa ndege za watu, kuzindua, kushangaa na kurejea, then what?.

Japo mimi sio mtaalam usafiri wa anga, lakini kusafiri nchi mbalimbali na katika misafa mbalimbali kumenipa exposure ya kutosha kuwaza kwa sauti.

Rais Samia na ujumbe wake, wako nchini Marekani, ambapo pamoja na mambo mengine, Rais Samia atafanya uzinduzi wa filamu yake ya Royal Tour.

Kwanza nitoe pongezi Kwa Sterling wa movie hiyo, mtu kuwa sterling wa movie yoyote kiukweli sii mchezo, ni kipaji!. Na kwa jinsi nilivyo ziona zile pati gazeti zake, "trailers", angekuwa ni Nyerere, asingeweza, Mwinyi, asingeweza, Mkapa ndio kabisa, na JPM asinge kubali hata huruhusu, mtu mwingine ambaye angalau angeweza kuwa starling wa movie kama hii ni JK, tena angepatia zaidi kwa sababu JK ni "hechibii" kumkaribia Steven Kanumba, Will Smith, Denzel Washington or Sidney Pointer.

Uzinduzi wa Royal Tour kufanyikia Marekani, ni mahali sahihi Kwa sababu huko ndio a catchment areas za watalii wenye fedha.

Kwa mawazo yangu, kwa vile lengo , pamoja na mambo mengine, ni ku promote utalii, hakuna kitu kinacho ongoza Kwa kupromote utalii kama usafiri wa ndege wa direct flights.

Na hakuna kitu kinaitangaza nchi kimataifa kama kupeperusha bendera ya nchi moja kwenye nchi nyingine, hakuna kitu kinaipeperusha vizuri bendera ya nchi kimataifa kama the national flag carriers, yaani ndege za mashirika yakitaifa kutua viwanja vya nchi nyingine.

Hii ni mara ya pili rais Samia kwenda Marekani, mara zote anakwenda Kwa ndege za mashirika ya ndege ya kibiashara ya nchi nyingine.

Rais Samia hasafiri safari za mbali Kwa ndege zetu ili kukwepa gharama. Kuliamsha Dreamliner letu kutua Marekani ni gharama kubwa. Lakini kama ni kweli tumedhamiria kwa dhati kuutangaza utalii wetu kimataifa, hatuwezi kukwepa gharama, lazima tuutangaze vivutio vyetu kimataifa. Namna bora ya kujitangaza kimataifa ni kupitia usafiri wa ndege wa kimataifa.

Tanzania na Marekani, tuna mkataba wa anga huria, hatuhitaji kuomba landing rights kwenye viwanja vyovyote vya Marekani, tunachohitaji ni kutoa tuu taarifa ili tutengewe a parking slot but we have a free access.

Dreamliner yetu ya Boeing 787 - 8 inabeba abiria 248 ambapo abiria ni 240 na 8 crew. Tuki reserves nafasi 40 kwa rais na ujumbe wake, halafu tukabeba abiria 200, kila abiria alipe nauli ya full package price ya US $ 5,000 kumsindikiza Mama Kuzindua Royal Tour, hao wasanii tuu wa Bongo Movies na Bongo Fleva wangeweza kuijaza. Ukijumlisha na wafanyabiashara, kampuni yangu ingepewa tender ya uhamasishaji hiyo trip, ningewapa abiria 500!.

Hii ni a Maiden trip, ya kitu kinachoitwa an "excursion" American tour kumsindikiza Mama kuzindua her movie The Royal Tour, na kazi itafanywa na a Tanzanian Tour Company ,aki partner na an American counterpart, the cost will be US $ 5,000 per person, Kwa Tanzania na US $.10,000 for Americans, the cost cover a round trip, includes a US Visa, 5 days 4 nights in New York, on a 2** hotel for Tanzanians and a 5***** tourist hotel in Arusha for the US Tourists. My role ni publicity only kuhamasisha. Nitawapata [emoji817] Bongo Movies na Bongo Music Stars wakiongozwa na Mondi, Kiba, Chinga, Mpoto ToT etc. [emoji817] journalist, [emoji817] ma pedejee wa Bongo ambao hawawezi kupata US visa wenyewe. [emoji817] wana CCM kumsindikiza Mwenyekiti, na [emoji817] wajasiriamali. There will be two trips, ndege itakwenda na 240 Watanzania, na kugeuza na 240 rich American tourist to Serengeti, Ngorongoro and Mt. Kilimanjaro.

The maiden trip ikifanikiwa tunaanza na a scheduled monthly monthly trips, then by-mothly ikibamba inakuwa weekly!. Na ili ndege isiende tupu US, naweza kuuza tuu a Disney Land School Trips Watanzania wenye uwezo wanaosomesha watoto wao Academy, wengi watawalipia. Na ikitokea tukakosa abiria wa Tanzania kujaza a scheduled direct flights, then tunafanya a monthly dege linaruka empty kuwabeba matajiri hao, kuwasubiria na kuwarudisha kama ile midege ya Kitaliano inayotua Zanzibar.

The only setback ni how to control the storeaways watakao taka kuzamia US!

Hivyo uzinduzi huo wa Royal Tour Nchini Marekani, would've made more sense kama Rais Samia angetua kwa Dreamliner na ATC kuzindua Direct Flights from JRO -JFK -JRO or from DAR-JFK-DAR.

Hakuna kitu kizuri kama Rais Samia angetua JFK Kwa Dreamliner na kupokelewa uwanjani hapo na Watanzania waishio Marekani kisha kuja nae hadi hotel aliyofikia.

Nikisema Watanzania ni wavivu kuchangamkia fursa, nitakuwa ninawaonea?. Kama ndege tunazo, abiria tunao, na soko lipo, hivi tuliinunua hii midege ya nini?!. Kweli ATC wanaona raha hii midege ya long distance haul, ikiruka domestic routes huku ikibeba vile vindoo vya samaki Sato kutokea Mwanza kuja Far na kwenda KIA pekee?. Tukisema pomoja na mambo mengine yote, lakini shirika letu la ndege kuendelea kupata hasara mwaka hadi mwaka kunachangiwa na menejinent kukosa wataalamu wa strategic thinking and planning kwenye airline business?.

Nawatakia uzinduzi mwema wa Royal Tour hiyo tarehe 18 na Pasaka Njema

Wasalaam.

Paskali
Rejea
Nice uchambuzi mzuri
 
Kuingiza ndege USA direct kutoka Tanzania sio rahisi kama unavyodhani. Kenya walikua na hiyo ruhusa sijajua kwa sasa wanaendeleaje.
Kuna michakato mingi sana ya kiusalama before kupewa hicho kibali.

Nitashangaa sana kama hata hili haulifahamu.
KQ wapo chali kwenye hiyo route, walijaza siku ya kwanza tu na sasa route wameifuta
 
Kwanza unapata wapi abiria 200 plus wa kujaza ndege inayoenda Marekani direct toka Tanzania?!
Airlines zinatumia mtindo wa “Hub and Spoke”, yaani abiria wanakusanywa toka sehemu mbalimbali kwenye point(Hub) moja kama vile pale Dubai (Emirates) na kupelekwa sehemu husika.
Pia kukidhi masharti ya kuingia US kama airline sio mchezo. Kenya Airways waliona shughuli yake.
Swali ni Kati ya Tanzania na Kenya, Nani wana abiria wengi wa US?. Ni sisi na ndio maana ndege ya direct inaanzia DAR, Nairobi to JFK.

Inachofanya KQ ni wamegundua fursa wakaichangamkia. Angalia kwenye utalii, Tanzania ndio tunaongoza Kwa vivutio vya utalii Ila half ya watalii wetu wanapitia Kenya!.

Kenya wanatutangazia mlima Kilimanjaro uko Kenya Ila kuupanda ndio unapandia Tanzania!. Sisi watalii wetu wa kupanda mlima Kilimanjaro wanashukia KIA ni 90 min to kupandia route ya Machame na 2 hrs route ya Marangu. Sasa Kenya wanajenga uwanja wa ndege pale Taveta, just 30 min drive to route ya Marangu!. Uwanja ukikamilika Nani watashukia KIA?.

Biashara ni kujipanga na matangazo
Tanzania lazima tuamke, kama Kenya wanaweza, kwanini sisi tushindwe?.
P.
 
Ningefurahi sana kama uzinduzi wa royal tour ungeanzia nyumbani kabla ya kuvuka boarder, nahisi ingependeza sisi wananchi kuwa mabalozi wa kwanza wa vivutio vyetu vya utalii.. Ila ni mawazo yangu tu
 
Ningefurahi sana kama uzinduzi wa royal tour ungeanzia nyumbani kabla ya kuvuka boarder, nahisi ingependeza sisi wananchi kuwa mabalozi wa kwanza wa vivutio vyetu vya utalii.. Ila ni mawazo yangu tu
Angefuturu burger saa ngapi sasa kama angezindua hapa.
Hiyo filamu ni moja ya kamba kati zile kamba zinazopaswa watu kula kwa urefu wake.

Urefu wa kamba ya mzindua filamu ni Marekani.
 
Dah hakika mkuu maana ilo jopo lililoenda america si la watu wachache
Wekeni orodha ya waliokwenda kwenye huo msafara tuone isiwe mnasingizia watu mwezi mtukufu wa Ramadhan mkifikiri hawawezi jibu shutuma zenu!
 
Kwanini isingeitwa "The Royal Safari". Hii ingeleta mashiko zaidi coz naona asilimia 90 ni mbugani.
 
Kila mtu ale urefu wa kamba yake wengi hapa kamba yetu inaishia kitongoji cha jirani Mama kamba yake hadi Newyork
 
Nyie si mlipandishaga wasanii mlima Kilimanjaro, mkakodia mademu zenu ndege wakaja mbugani uko eti mnatangaza utalii 😂😂😂😂 sema kigwangala sijui alituonaje watanzania dah eti Tanzania unforgettable
 
Back
Top Bottom