Wanabodi,
Naendelea na zile makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa, makala ya Leo ikiwa ni makala ya swali la hypothetical question (swali la kufikirika), Kwa njia ya "thinking aloud", yaani unawaza kwa sauti.
Swali ni hili "Jee uzinduzi wa filamu ya Royal Tour, unaofanyikia nchini Marekani, upi ungekuwa na maslahi zaidi Kwa taifa kama Rais Samia angetua nchini Marekani kwa dege Letu la Dreamliner, huku ATC ikizindua Direct Flights from DAR-JFK-DAR/JRO-JFK-JRO? au kwenda Kwa ndege za watu, kuzindua kushangaa na kurejea, then what?.
Japo mimi sio mtaalam usafiri wa anga, lakini kusafiri nchi mbalimbali na katika misafa mbalimbali kumenipa exposure ya kutosha kuwaza kwa sauti.
Rais Samia na ujumbe wake, wako nchini Marekani, ambapo pamoja na mambo mengine, Rais Samia atafanya uzinduzi wa filamu yake ya Royal Tour.
Kwanza nitoe pongezi Kwa Sterling wa movie hiyo, mtu kuwa sterling wa movie yoyote kiukweli sii mchezo na kwa jinsi nilivyo ziona zile pati gazeti, "treilers", angekuwa ni Nyerere, asingeweza, Mwinyi, asingeweza, Mkapa ndio kabisa, na JPM asinge kubali hata huruhusu, mtu mwingine ambaye angeweza kuwa starling wa movie kama hii ni JK, tena angepatia zaidi kwa sababu ni "hechibii" kumkaribia Steven Kanumba, Will Smith, Denzel Washington or Sidney Pointer.
Uzinduzi wa Royal Tour kufanyikia Marekani, ni mahali sahihi Kwa sababu huko ndio a catchment areas za watalii wenye fedha.
Kwa mawazo yangu, kwa vile lengo , pamoja na mambo mengine, ni ku promote utalii, hakuna kitu kinacho ongoza Kwa kupromote utalii kama usafiri wa ndege wa direct flights.
Na hakuna kitu kinaitangaza nchi kimataifa kama kupeperusha bendera ya nchi moja kwenye nchi nyingine, hakuna kitu kinaipeperusha vizuri bendera ya nchi kimataifa kama the national flag carriers, yaani ndege za mashirika yakitaifa kutua viwanja vya nchi nyingine.
Hii ni mara ya pili rais Samia kwenda Marekani, mara zote anakwenda Kwa ndege za mashirika ya ndege za mashirika ya kibiashara ya nchi nyingine.
Rais Samia hasafiri safari za mbali za ndege zetu ili kukwepa gharama. Kuliamsha Dreamliner letu kutua Marekani ni gharama kubwa. Lakini kama ni kweli tumedhamiria Kwa dhati kuutangaza utalii wetu kimataifa, hatuwezi kukwepa gharama.
Tanzania na Marekani, tuna mkataba wa anga huria, hatuhitaji kuomba landing rights kwenye viwanja vyovyote vya Marekani, tunachohitaji ni kutoa tuu taarifa ili tutengewe a parking slot.
Dreamliner yetu ya Boeing 787 - 8 inabeba abiria 248 na Airbus ambapo abiria ni 240 na 8 crew. Tuki reserves nafasi 40 kwa rais na ujumbe wake, halafu tukabeba abiria 200, kila abiria alipe nauli ya US $ 5,000 kumsindikiza Mama Kuzindua Royal Tour, hao wasanii tuu wa Bongo Movies na Bongo Fleva wangeweza kuijaza. Ukijumlisha na wafanyabiashara, kampuni yangu ingepewa tender ya uhamasishaji hiyo trip, ningewapa abiria 500!.
Hivyo uzinduzi huo wa Royal Tour Nchini Marekani, would've made more sense kama Rais Samia angetua kwa Dreamliner na ATC kuzindua Direct Flights from JRO -JFK -JRO.
Hakuna kitu kizuri kama Rais Samia angetua JFK Kwa Dreamliner na kupokelewa uwanjani hapo na Watanzania waishio Marekani kisha kuja nae hadi hotel aliyofikia.
Nikisema Watanzania ni wavivu kuchangamkia fursa, nitakuwa ninawaonea?. Kama ndege tunazo, abiria tunao, na soko lipo, hivi tuliinua hii midege ya nini?. Kweli ATC wanaona raha hii midege ya long distance haul, ikiruka domestic routes huku ikibeba vile vindoo vya samaki Sato kutokea Mwanza kuja Far na kwenda KIA pekee?. Tukisema pomoja na mambo mengine yote, lakini shirika letu la ndege kuendelea kupata hasara mwaka hadi mwaka kunachangiwa na menejinent kukosa wataalamu wa strategic thinking and planning kwenye airline business?.
Nawatakia uzinduzi mwema wa Royal Tour hiyo tarehe 18 na Pasaka Njema
Wasalaam.
Paskali