Kongole Mkuu ,
Wewe ni THIK TANK, lakini Serikali ya CCM haina Utamaduni huu wa kuchukua Mafikara ya Raia wema.
Nchii hii inafeli kwa kutokuwatumia vema watu wake.
Akili za Watanzania zingeliweza kikwamua nchi katika mambo mengi, lakini hawakuwekewa Canel.
Kila kitu tunaamini kuwa Wabunge eti ndio wataishauri serikali, Hata kama wengine hawa kubarikiwa Vipaji ?
TAIFA LINAKUHITAJI Pascal
Kongole.
Ila nina wasi wasi kuwa
ATCL Haina ruhusa kurusha ndege zake nje ya nchi mpaka ilipe deni la miaka mingi inalodaiwa na IATA
Tokea enzi za Nyerere hadi mkapa alipoamua kuliuza shirika kwa matapeli wa SOUTH.
Yamkini deni ni kubwa mno.
kumbuka sasa tumeporomoka sana kiuchumi na sio Tanzania tu bali kila nchi kwa sasa imetikisika.
Katika kipindi hiki Rais katumia busara na weledi na mbinu ya hali ya juu mbele ya Mataifa Tajiri,
Nchi masikini kama yetu unaanzaje kuonyesha mbwembwe za ukwasi "uchwara" eti wa matajiri wa muziki na bongo movi na matajiri wachache wakuokoteza mbele ya giant?!
kwa sasa bado tunahangaika.........
Mama anapambana ili angalau tutoboe.....hakuna haja ya mbwembwe!
Nchi yetu bado ni masikini, watu wake bado ni masikini wa kutupwa!!,
Mama kabana matumizi, hakuna haja ya ufahari wakati bado tunpmbana.
Kila jambo linaenda kwa hatua, kwa sasa wacha Mama kwanza atangaze Vivutio vya kitalii tulivyo navyo, kwakuwa ndege tunazo hakuna shida Muda ukifika ndege zitapiga kazi na zingine zitaongezwa.
Mungu mbariki Raisi wetu kwa kazi nzuri ya kuitangaza nchi na kuinua utalii wa nchi.
The maiden trip ikifanikiwa tunaanza na a monthly. Na ili ndege isiende tupu naweza kuuza tuu a Disney Land School Trips Watanzania wanaosomesha watoto wao Academy, wengi watawalipia.
The only setback ni how to control the storeaways watakao taka kuzamia US!
Mshauri Raisi auze Hisa za ATC ili aruhusu Patnership na tafute wataalamu BINGWA wa Airliner duniani ili waendeshe shirika ,tuongeze Mtaji na Ndege kubwa , kwani Safari za Kimataifa unatakiwa kuwa na Ndege za Kutosha kwa Dharura ili ikitokea moja kufeli nyingine ichekua nafasi
Mshauri Raisi auze Hisa za ATC ili aruhusu Patnership na tafute wataalamu BINGWA wa Airliner duniani ili waendeshe shirika ,tuongeze Mtaji na Ndege kubwa , kwani Safari za Kimataifa unatakiwa kuwa na Ndege za Kutosha kwa Dharura ili ikitokea moja kufeli nyingine ichekua nafasi
Wanabodi, Naendelea na zile makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa, makala ya Leo ikiwa ni makala ya swali la hypothetical question (swali la kufikirika), Kwa njia ya "thinking aloud", yaani unawaza kwa sauti.
Swali ni hili "Jee uzinduzi wa filamu ya Royal Tour, unaofanyikia nchini Marekani, upi ungekuwa na maslahi zaidi kwa taifa kama Rais Samia angetua nchini Marekani kwa dege letu la Dreamliner, huku ATC ikizindua Direct Flights from DAR-JFK-DAR/JRO-JFK-JRO? au kuendelea kwenda kwa ndege za watu, kuzindua, kushangaa na kurejea, then what?.
Japo mimi sio mtaalam usafiri wa anga, lakini kusafiri nchi mbalimbali na katika misafa mbalimbali kumenipa exposure ya kutosha kuwaza kwa sauti.
Rais Samia na ujumbe wake, wako nchini Marekani, ambapo pamoja na mambo mengine, Rais Samia atafanya uzinduzi wa filamu yake ya Royal Tour.
Kwanza nitoe pongezi Kwa Sterling wa movie hiyo, mtu kuwa sterling wa movie yoyote kiukweli sii mchezo, ni kipaji!. Na kwa jinsi nilivyo ziona zile pati gazeti zake, "trailers", angekuwa ni Nyerere, asingeweza, Mwinyi, asingeweza, Mkapa ndio kabisa, na JPM asinge kubali hata huruhusu, mtu mwingine ambaye angalau angeweza kuwa starling wa movie kama hii ni JK, tena angepatia zaidi kwa sababu JK ni "hechibii" kumkaribia Steven Kanumba, Will Smith, Denzel Washington or Sidney Pointer.
Uzinduzi wa Royal Tour kufanyikia Marekani, ni mahali sahihi Kwa sababu huko ndio a catchment areas za watalii wenye fedha.
Kwa mawazo yangu, kwa vile lengo , pamoja na mambo mengine, ni ku promote utalii, hakuna kitu kinacho ongoza Kwa kupromote utalii kama usafiri wa ndege wa direct flights.
Na hakuna kitu kinaitangaza nchi kimataifa kama kupeperusha bendera ya nchi moja kwenye nchi nyingine, hakuna kitu kinaipeperusha vizuri bendera ya nchi kimataifa kama the national flag carriers, yaani ndege za mashirika yakitaifa kutua viwanja vya nchi nyingine.
Hii ni mara ya pili rais Samia kwenda Marekani, mara zote anakwenda Kwa ndege za mashirika ya ndege ya kibiashara ya nchi nyingine.
Rais Samia hasafiri safari za mbali Kwa ndege zetu ili kukwepa gharama. Kuliamsha Dreamliner letu kutua Marekani ni gharama kubwa. Lakini kama ni kweli tumedhamiria kwa dhati kuutangaza utalii wetu kimataifa, hatuwezi kukwepa gharama, lazima tuutangaze vivutio vyetu kimataifa. Namna bora ya kujitangaza kimataifa ni kupitia usafiri wa ndege wa kimataifa.
Tanzania na Marekani, tuna mkataba wa anga huria, hatuhitaji kuomba landing rights kwenye viwanja vyovyote vya Marekani, tunachohitaji ni kutoa tuu taarifa ili tutengewe a parking slot but we have a free access.
Dreamliner yetu ya Boeing 787 - 8 inabeba abiria 248 ambapo abiria ni 240 na 8 crew. Tuki reserves nafasi 40 kwa rais na ujumbe wake, halafu tukabeba abiria 200, kila abiria alipe nauli ya full package price ya US $ 5,000 kumsindikiza Mama Kuzindua Royal Tour, hao wasanii tuu wa Bongo Movies na Bongo Fleva wangeweza kuijaza. Ukijumlisha na wafanyabiashara, kampuni yangu ingepewa tender ya uhamasishaji hiyo trip, ningewapa abiria 500!.
Hii ni a Maiden trip, ya kitu kinachoitwa an "excursion" American tour kumsindikiza Mama kuzindua her movie The Royal Tour, na kazi itafanywa na a Tanzanian Tour Company ,aki partner na an American counterpart, the cost will be US $ 5,000 per person, Kwa Tanzania na US $.10,000 for Americans, the cost cover a round trip, includes a US Visa, 5 days 4 nights in New York, on a 2** hotel for Tanzanians and a 5***** tourist hotel in Arusha for the US Tourists. My role ni publicity only kuhamasisha. Nitawapata 💯 Bongo Movies na Bongo Music Stars wakiongozwa na Mondi, Kiba, Chinga, Mpoto ToT etc. 💯 journalist, 💯 ma pedejee wa Bongo ambao hawawezi kupata US visa wenyewe. 💯 wana CCM kumsindikiza Mwenyekiti, na 💯 wajasiriamali. There will be two trips, ndege itakwenda na 240 Watanzania, na kugeuza na 240 rich American tourist to Serengeti, Ngorongoro and Mt. Kilimanjaro.
The maiden trip ikifanikiwa tunaanza na a scheduled monthly monthly trips, then by-mothly ikibamba inakuwa weekly!. Na ili ndege isiende tupu US, naweza kuuza tuu a Disney Land School Trips Watanzania wenye uwezo wanaosomesha watoto wao Academy, wengi watawalipia. Na ikitokea tukakosa abiria wa Tanzania kujaza a scheduled direct flights, then tunafanya a monthly dege linaruka empty kuwabeba matajiri hao, kuwasubiria na kuwarudisha kama ile midege ya Kitaliano inayotua Zanzibar.
The only setback ni how to control the storeaways watakao taka kuzamia US!
Hivyo uzinduzi huo wa Royal Tour Nchini Marekani, would've made more sense kama Rais Samia angetua kwa Dreamliner na ATC kuzindua Direct Flights from JRO -JFK -JRO or from DAR-JFK-DAR.
Hakuna kitu kizuri kama Rais Samia angetua JFK Kwa Dreamliner na kupokelewa uwanjani hapo na Watanzania waishio Marekani kisha kuja nae hadi hotel aliyofikia.
Nikisema Watanzania ni wavivu kuchangamkia fursa, nitakuwa ninawaonea?. Kama ndege tunazo, abiria tunao, na soko lipo, hivi tuliinunua hii midege ya nini?!. Kweli ATC wanaona raha hii midege ya long distance haul, ikiruka domestic routes huku ikibeba vile vindoo vya samaki Sato kutokea Mwanza kuja Far na kwenda KIA pekee?. Tukisema pomoja na mambo mengine yote, lakini shirika letu la ndege kuendelea kupata hasara mwaka hadi mwaka kunachangiwa na menejinent kukosa wataalamu wa strategic thinking and planning kwenye airline business?.
Nawatakia uzinduzi mwema wa Royal Tour hiyo tarehe 18 na Pasaka Njema
Wanabodi, Kila nipatapo fursa, huwaletea mfufululizo wa makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" Makala ya leo ni bandiko la pongezi na ombi. Pongezi ni kwa Rais Samia, kusafiri kwa kukwea pipa la watu, kwenda nchini Marekani, na kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA. Ombi ni kwa...
Wanabodi, Lile Shirika letu la Ndege, ATCL, lililokuwa mkao wa kifo, baada ya kuwa hoi bin taaban huku jeneza la kuizika rasmi likiwa limeishaandaliwa, hatimaye sasa litafufuka, kwa kuibuka kisasa zaidi, kwa nguvu zaidi na kurejea katika utawala wa soko la biashara ya ndege nchini (regain the...
Wanabodi, Japo mimi ni miongoni mwa wale tuliopinga ununuzi wa ndege kwa cash money, na serikali yetu kufanya matumizi makubwa kama haya ya manunuzi makubwa kwa kutumia fedha za umma bila idhini ya Bunge, kwa sababu fedha za umma zinaongozwa na sheria, taratibu na kanuni, mtu hata ukiwa nani...
Niliwahi kusikia route ya Mumbai,mara nikasikia ya DAR-Heathrow hivi hizi ziliishia wapi?? Ukitaka kuona hili shirika menejiment yake haipo serious waulize hizi Route kwanini zilikatishwa?
Tatizo si abiria japo nalo lipo kwa shirika lisilokuwa na jina, kama mchaguavyo mabasi ya mikoani kwenye ndege ni zaidi kwani hauanzia kwenye marubani.
Ni juzi tu ndani ya bunge ilisikika sauti ikiongelea kuhusu kunguru wetu kuwindwa kutokana na utamu wa nyama zake! Hivyo wamelazimika warukeruke karibu na viota vyao.
Tukumbuke mdada alikwenda Dubai huko kwenye maonesho angeweza kuongea na mashirika makubwa yenye ujuzi kuingia ubia kwa japo kuwakodisha ndege ili zianze kufahamika, nilichosikia toka huko tukijivunia picha yake kuonekana kwenye jengo refu duniani, sijui mpaka sasa tumeingiza faida kiasi gani! Je, hayakuwepo mashirika makubwa ya ndege yaliyokuwepo yakijitangaza? Nina uhakika yalikuwepo. Tunapoiuza Tanzanite kwanini tusiiwekee logo ya ATCL kuwa mdhamini wake angalau ianze kujulikana hata kama si mahali pake. Mimi binafsi tangu mwaka uanze sijawahi kuliona tangazo lolote la ATCL hata kwenye maguta ukiacha mabasi yanayokwenda nje ya nchi.
Mwisho dawa ya deni ni kulipa si kibadili njia, tulipe ili ndege zetu ziwe huru kuwafuta mtama kukote duniani.
Kuingiza ndege USA direct kutoka Tanzania sio rahisi kama unavyodhani. Kenya walikua na hiyo ruhusa sijajua kwa sasa wanaendeleaje.
Kuna michakato mingi sana ya kiusalama before kupewa hicho kibali.
Mimi napenda safari za ku connect, ndege yangu ya sasa ni Quatar, wakati wa booking inaonyesha huna haraka hivyo connection ni more than 6 hours, ukifika Doha unakuwa shifted kwenye a 5 star hotel near airport na umelipwa full board. Unasafiri Kwa raha tuu.
Nikiamua kupanda KQ ni ili ku save money.
P
Wow! More than 6 hoursbkupewa accommodation kwenye 5 star hotel ipo kisheria au discretion ya Carrier? Kuna kipindi niliwahi kupewa Accommodation Addis Ababa, kufika hotelini wajasiriamwili Kama wote
Kuingiza ndege USA direct kutoka Tanzania sio rahisi kama unavyodhani. Kenya walikua na hiyo ruhusa sijajua kwa sasa wanaendeleaje.
Kuna michakato mingi sana ya kiusalama before kupewa hicho kibali.
unataka kusema Safari ya mama ni dharula Kama sio dharula uandaaji wa Safari ulitakiwa uliangalie asemalo mayala nawewe kuhusu huo usalama wako unataka
Mbona Delta wanaruka OR Rambo, RSA wanatua Kotoka International Airport (Ghana) wanapakia tena abiria na kujaza mafuta then mwendo mdundo to Atlanta!
**Pichani KLM ikikata wingu Atlantic turbulence Kama yote.
Halafu kuna mtu alitaka eti tuongeze somo la historia ya Tanzania tuendelee kujaza upuuzi tu kichwani kwa sababu na yeye alitaka atajwe badala hata ya kuinvest kwenye knowledge ya science and technology tuendelee kuwajaza watoto wetu story za kina kinjekitile Ngwale karne hii
Halafu kuna mtu alitaka eti tuongeze somo la historia ya Tanzania tuendelee kujaza upuuzi tu kichwani kwa sababu na yeye alitaka atajwe badala hata ya kuinvest kwenye knowledge ya science and technology tuendelee kuwajaza watoto wetu story za kina kinjekitile Ngwale karne hii
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.