Je, Uzinduzi Royal Tour ungekuwa na maana kama Rais Samia angetua kwa Dreamliner & ATC kuzindua Direct Flights from DAR-JFK-DAR/JRO-JFK-JRO?

Je, Uzinduzi Royal Tour ungekuwa na maana kama Rais Samia angetua kwa Dreamliner & ATC kuzindua Direct Flights from DAR-JFK-DAR/JRO-JFK-JRO?

Mbona Delta wanaruka OR Rambo wanatua Kotoka International Airport (Ghana) wanapakia na kujaza mafuta then mwendo mdundo to Atlanta!
**Pichani KLM ikikata wingu Atlantic turbulence Kama yote
Huwa wengi wanatengeneza route ya hivyo ili wapakie na kushusha, hapo hakuna tatizo.

Shida inakuwa pale ukisema ni direct flight halafu ushuke kupakia mafuta.

Sasa ATC ataweza kuwa na route ya Accra au Dakar? Kwa abiria wepi?
 
Rwandair waliwezaje? Routes za West Africa kuunganisha na Middle East/southern Africa ni strategic. Rwandair anayo Kigali-Accra-Lagos...KQ anayo NBO-Accra-Freetown-Monrovia
 
Hizo route (direct flight) wanaziweza waarabu (Kutokea Dubai, Abu Dhabi au Doha) vinginevyo Lazima unnye (stop) sehemu kabla ya kukatiza Atlantic. Hata enzi za South African Airlines ilikua inachutama Accra
 
Rwandair waliwezaje? Routes za West Africa kuunganisha na Middle East/southern Africa ni strategic. Rwandair anayo Kigali-Accra-Lagos...KQ anayo NBO-Accra-Freetown-Monrovia
Paskali aliongelea direct route na ndio argument ikawa kwenye range ya hizo ndege zetu.

Inawezekana kabisa kufanya hizo route endapo business case ita make sense.
 
Nakuomba siku hiyo ikitangazwa tangazo la Ku board, nakuomba simama pembeni ya boarding gate, then wahesabu abiria walio board from Dar, wewe uwe the last to board, ukifika ndani, wahesabu abiria business wao wana board from lounge na VIP, wajumlishe na wale wa economy, then get the total, ili tuwaeleze hawa vichaa wetu wa ATCL, what a wasted opportunity they are missing!. Wakenya wanatubebea watalii wetu, wanatusombea kazi zetu, kule Rombo wanatubebea wake zetu, sasa hata kwenda Marekani, wanatubebea abiria wetu!, kwenye soko la AGOA wanatuingizia bidhaa zetu, hata kwenye kuutangaza utalii wa mlima Kilimanjaro, wanatutangazia mlima wetu kuwa uko kwao, ila unapandwa upande wa Tanzania!. Watanzania tutaendelea kulala mpaka lini?.
P
Mkuu Paskal umeongea Jambo muhimu sana, ni Kama tumefungwa ufahamu.
 
Paskali aliongelea direct route na ndio argument ikawa kwenye range ya hizo ndege zetu.

Inawezekana kabisa kufanya hizo route endapo business case ita make sense.
Okay. Tatizo naliona Aina ya menejimenti iliyopo. Exposure (experience ya aviation/travel industry business) hamna, wengi walistahili kuwa Halmashauri hukooo Manyoni Vijijini. Kuna Waziri aliletwaga na jiwe ndo akawa anaendaga Canada kwenye zile Mbanga, kajaza watu wake humo balaa. Marketing strategy ya ATC ni kizungumkuti
 
KLM pia rahisi kwa watalii mana straight Schipol/Amsterdam to JRO/KIA
All flights lazima zipite kwenye base yake na ku connect. Kwa Tanzania direct flights ni KQ only inaanzia DAR as a regional route to Nairobi, na ndipo inapiga shoot ndefu ya JFK. Ukipanda ndege nyingine yoyote, lazima upite base yake na ku connect, Ethiopia lazima upite Addis, BA lazima upite London, KLM lazima upite Amsterdam, Emirates unapita Dubai, SAA, unapita Joburg. Hakuna ndege yoyote ya US inayokuja direct hapa Bongo. Hiyo KQ ya direct New York, inategemea abiria kibao wa Tanzania, Royal Tour ni Fursa ya kuifungua Tanzania kwa soko kubwa tajiri la utalii wa Wamarekani.

Kuna watalii matajiri na watalii masikini, watalii matajiri hawataki shida, ndio wanaopanda direct flights na Arusha wanafikia 5 star hotels. Marekani ni Watalii matajiri. Watalii masikini wanasafiri hata magari ya watalii na kulala campsites.

To me itakuwa ni aibu kwa Tanzania, kama Mama anaifungua nchi kwa fursa kama hii fursa ya Royal Tour, halafu ATC ukashindwa kuchangamkia fursa, watalii wakaletwa na KQ!.
P
 
biashara ya kurusha ndege kimataifa ni ngumu sana kwa serikali yetu. Nchi yetu haijulikani sana duniani hilo ni swala gumu sana ktk biashara ya anga. mwaka 1982 tulifungua route ya London. serikali ilikula hasara mbaya sana. Ilifikia mahala ndege inaondoka DSM bila abilia na kurudi kutoka London tupu! Tangaza nchi na fanya urafiki na bepari utavuna ngawila za biashara ya anga.
 
Back
Top Bottom