MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,996
Takriban wiki ya tatu tokea Kamati maalumu ya tathmini ya ugonjwa wa Corona (COVID-19) nchini kukamilisha kazi yake na kukabidhi ripoti kwa Rais Samia Suluhu Hassan.
Tume hiyo ilikuja na mapendekezo zaidi ya 19 ambapo mpaka sasa ukiondoa pendekezo ya kuagiza chanjo ya Corona ambalo serikali imeishalifanya, hakuna pendekezo lingine ambalo limeishafanyiwa kazi kikamilifu.
Hata pendekezo la kuvaa barakoa na kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka au vitakasa mikono halifuatwi achilia mbali kutoa takwimu za maambukizi ya ugonjwa wa Corona kwa wananchi na uhamasishaji wa chanjo kwa wananchi.
Ukichunguza hata uvaaji wa barakoa umebakia Ikulu peke yake na pindi viongozi wanapotoka Ikulu, wanazitupa barakoa kwenye geti za Ikulu! Hakuna cha social distancing hata Ikulu
Ukienda kwenye ofisi zingine za serikali, hakuna cha barakoa au maji ya kunawa/vitaka mikono.
Ukichunguza vizuri hata Rais Samia havai vizuri barakoa bali anafunika mdomo tu huku pua yake ikiwa nje ya barakoa! Ni kama anajilazimisha kuvaa barakoa ili aonekane amevaa lakini kiuhalisia hajavaa.
Mtu mwenye fikra pana atajiuliza, kulikuwa na sababu gani kwa serikali kutumia pesa kama posho kwa kamati ya watu zaidi ya 10 ambayo serikali hiyo hiyo inapuuza mapendekezo yake?
Kama hoja ilikuwa ni kuagiza chanjo ya Corona, haikuhitaji mpaka kuunda kamati ya watu zaidi ya 10 ambayo imekuja na vitabu vikubwa kama misahafu vinne vyenye mapendekezo ambayo ni pendekezo moja tu mpaka sasa ndilo limefanyiwa kazi. Ni kama ulikuwa ni usanii fulani ambao matokeo yake yalikuwa yanajulikana bali kilichokuwa kinatafutwa ni uhalalisho wa kuagiza chanjo ya corona na kukopa pesa za kukabiliana na ''janga la Corona''.
Kuagiza chanjo hakukuhitaji tume ya watu zaidi ya 10 bali kilichohitajika kwanza ni elimu ya corona kwa watanzania.
Ni ukweli kuwa mapendekezo ya Kamati ya Corona yamepokelewa kwa hisia hasi na watanzania wengi.
Kwa sasa tunakuwa na serikali ambayo inatoa ishara zisizoeleweka kwa wananchi kwa sababu viongozi hawana ujumbe/mwelekeo mmoja kwa wananchi kuhusu suala la Corona.
Serikali wanatakiwa watuambia kama Corona ipo na tujiandae kwa chanjo au watuambia corona haipo na chanjo iwe kwa wasafiri wa nje ya nchi.
Serikali kukaa kimya hakuwezi kuondoa ''tatizo'' ambalo kiuhalisia wameliasisi wao wenyewe baada ya kuunda Kamati ya Corona.