Mkuu, Mimi bado naziamini hoja zote zinazo ongoza humu kuhusu hayati JPM, naziamini Kwa sababu kila mtu anahoja nzito na inahitaji majibu ya kina,
Wale wenye Mashaka na namna alivyotuaga, wako na sababu zao na hoja zao sio tu mtu uwaropokee na kuwakaripia wakati ukiwajibu, lakini pia Kwa hao wengine wanaoamini kinyume na wenye msimamo wa mashaka juu ya kutuaga kwake JPM, Wana hoja vilevile na huwezi tu kukaa unawatukana Kwa sababu ya intereste za hao wenye msimamo mwingine
Na ili kuondoa hii misimami miwili tofauti, ni ama ibaki hivi hivi Kwa kuwa hawezi kuwepo mshindi juu ya hilo, na endapo kunahitajika apatikane mshindi wa hoja mbili kinzani hizi, basi uchunguzi ni wa lazima, tena uwe ni uchunguzi huru kutoka huko Kwa wasioweza kuhongwa