Hiyo Kamati ya Corona kwa mtazamo wangu ingependeza iundwe wakati ule wa mwendazake wakati Corona ilikuwa inamaliza watu haswa, hasa baada ya kuibuka kile kirusi toka SA.
Pale ndio ingefaa hiyo kamati ije na hayo mapendekezo ya kuvaa barakoa na mengine kwasababu kweli wananchi walikuwa kwenye allert na huo ugonjwa kutokana na taarifa za vifo zilivyokuwa zinatoka kila dakika, mara profesa fulani kaondoka, mara daktari fulani.
Sasa hivi tension kuhusu Corona imeshuka sana, hata kama ugonjwa bado upo, lakini kwa ujumla sio kwa kiwango kile cha mwanzo, hivyo kuhimiza watu wavae barakoa wakuelewe lazima pawepo na taarifa nyingine za kuthibitisha ugonjwa bado upo na unaua, lakini kusema tu ugonjwa upo wakati mtaani pamepoa inakuwa ngumu kueleweka.
Ndio maana hata huko serikalini unaona wanaovaa barakoa ni wale wa ikulu tu, tena hawavai muda wote, tukio fulani kavaa tukio linalofuata hajavaa; mawaziri, manaibu wao, makatibu wakuu na wengine wote hadi kule bungeni hakuna tena anaevaa barakoa kwa sasa, hiyo kamati ni kama inepoteza pesa tu.