Je, Viongozi wa Idara ambao ni Wachagga waachie ngazi!??

Je, Viongozi wa Idara ambao ni Wachagga waachie ngazi!??

Status
Not open for further replies.
Mwanakijiji hebu kuwa serious. Na wewe nenda kapige buku ufaulu then uombe uCEO, ukurugenzi uone kama haupata.
Acha chuk u na wachagga.ni haki yao na bado wanajuhudi kubwa sana ya kusoma na wataendelea kupata nafasi kubwa wewe unaona wivu.
Kama muda umeenda basi watoto wako nao wapige buku. Juhudi za wachaga ndio zinazofanya watoke. angalia tanzania nzima wapo, kabila lako wapo hivyo? wanaenda huko kutafuta kama sio kazi ni biashara.
 
Mwanakijiji Post yako ingawa ina sura mbaya ina mantiki na kupotray hali halisi. Kwanza suala la elimu, jamii nyingi imeweka nyuma ukilinganisha na wachaga hilo halina mjadala mimi nikiwa mchaga nathibitisha kwa hapo hamtuwezi. Mchaga ni mvumilivu na mtafutaji hasa kiasi hata cha baadhi ya ndugu zetu wahindi kujipa majina ya Utani ya kichaga. Nawaambia nimekwenda kaskazini kabisa ya Sweden mji unaitwa Kiruna kilometre chache tu kufika north pole kwa wanaojua nimekuta mchaga ana duka la vifaa vya umeme. Mzaramo hata hapo Chalinze hana kitega uchumi. Tukiingia kwenye mifumo ya mabenki wachaga ndio wanaongoza kuchukua mikopo na ndio wanaoongoza kulipa MIKOPO second to wahindi. Hawa ni risk takers wakubwa na kawaida the higher the risk the higher the return hivyo wao kufanikiwa ni WAZI KABISA. Tuache kulalama tuwaige kwa kasi wachaga na ndio tutafanikiwa. KUPIGA VITA WACHAGA HAKUANZI LEO , HATA NYERERE ALIJARIBU AKAKUTA NDIO ANAWAONGEZEA MAENDELEO YAANI NI KAMA KUKPIGA CHURA TEKE. I AM PROUD KUWA MCHAGA.
 
ianzishwe directorate ya kuajiri kwa ajili serikali na agency zake zote. Nafasi zote za kazi ziwe zinapelekwa kwenye hiyo directorate ambayo [Iitazitangaza na kufanya usaili kwa kuhusisha experts from the appropriate unit inayotaka mfanyakazi. [/I]

KWA TAARIFA TU HIYO DIRECTORATE ITAKUWA INAONGOZWA NA MCHAGA AU NAFASI KUBWA ZITAKUWA ZINASHIKILIWA NA WACHAGGA.
MNAJUA KWENYE AJIRA HAKUNA UBAGUZI. KINACHOKUPA KAZI NI QUALIFICATIONS ZAKO TU HIVYO WACHAGA WATAKUWEPO. LABDA WATANGAZE KUWA WACHAGA HAWATAKIWI KUOMBA KAZI KWENYE HIYO DIRECTORATE LAKINI SHERIA YA KAZI IPO, INASEMAJE? WATAKOSHAURI MUUNDO WA HIYO KITU KWA MKUU WA KAYA WAMO WACHAGGA.

NASHAURI MJADILI MAMBO YA MAANA. MKITOKA WACHAGGA MTAKUJA WAHAYA :whoo:
 
Je Wachagga wanyanywe Biashara zao? Kwa sababu mimi naona wachagga wameshikilia sehemu kubwa ya biashara Tanzania especially transportation,tourism na communication. Mimi naona hapa ndiopo matizo lipo. Hawa wachagga wakihamua kufunga hoteli zao au wafanye mgomo wa usafiri wa anga au nchi kavu, inchi itakuwa kwenye hali mbaya saana. Kwa hivyo mimi naona Tatizo siyo wachagga kuwa serekalini, tatizo wachagga shikilia biashara nyeti za nchi.

Vile vile wakati Mwalimu Nyerere alipo to order ya kwamba uwiano wa shule/elimu uwe sawa miaka ya 80, kwa kuwafanya wachagga wasifaulu darasa la saba, Wachagga walianzisha private school. Ndio maana uchaggani kuna shule nyingi za private kuliko sehemu yetote TZ. Hata Dar. haina private school nyingi kama Kilimanjaro. Nashule hizi zinafundisha vizuri kuliko shule za serekali; matokeo yake, wachagga walipata elimu bora kuliko sisi tulio kwenda shule za sekondari wakati wa Mwalimu. Matokeo yake, viongozi wa serekali walianza kupeleka watoto wao uchaggani kupata elimu bora kama wachagga.

Mwisho, ningependa kusema kama tuta fanya chochote kuwazuia wachagga, tuwe makini kwa sababu wana weza kutafuta njia nyingine ambazo zitawafanya wa endelee kuliko jamii nyingine ya Tanganyika.
 
Mwanakijiji,

..actually kuna mpango ambao unakaribiana na mapendekezo yako ulitekelezwa ktk sekta ya ELIMU.

..mpango huo wa serikali ulijulikana kama QUOTA-SYSTEM ktk kuchagua wanafunzi wanaokwenda shule za sekondari za serikali.

..quota-system iliweka pass-mark ya chini ktk mikoa ya pembezoni, kulinganisha na pass-mark ktk mikoa ya kilimanjaro,kagera,mbeya,..

..lengo lilikuwa kutoa nafasi zaidi kwa wanafunzi wanaochaguliwa kwenda sekondari toka mikoa ya pembezoni.

..ilifika kipindi watoto wa kichaga wakalazimika kubadili majina na kuhamia mikoa mingine ili kupata nafasi kusoma ktk sekondari za serikali.

NB:

..hii uliyoleta hapa kwa kweli ni CHANGAMOTO. nategemea watu watakuja na short-term pamoja na long-term proposals za jinsi ya kushughulikia tatizo hili.


Hawa jamaa ni wabishi, watoto wao huwa wanajitahidi kusoma lakini inakuwa si bahati kwao kufaulu, ila hata tukisema tuwaondoe kwenye madaraka mbalimbali ya serikali wanaweza kuwa wafanyabiashara wakubwa wenye makampuni makubwa na wakaanza tabia zao zile zile.
 
Mwanakijiji

hebu kachungulie ppf

1. Idara ya fedha, mkurugenzi ni mchaga, amejaza wachaga wa kutoka wilaya yake. Wasio wachaga washida na kuondoshwa, anawatukana kama watoto wadogo, mkurugenzi mkuu anaangalia tu watanzania wanatukanwa kama watumwa

2. Mkurugenzi mkuu sio mchaga ila kalelewa mchaga ambaye ni mke wa mjomba wake. Yeye anaajiri watu wa mtwara hasa kwenye nafasi nyeti.

3. Ppf pia ichunguzwe hasa ajira zinazoendelea kuanzia 2007, wanawake wana pata shida na wakware hawa wakiongozwa na mkurugenzi mkuu. Usalama wa taifa wamchunguze anavyotumia u dg kupata wanawake wa kujifurahiha.

Ppf kunatisha

kama kwa hiari haiwezekani, rais anaweza kutoa agizo (executive order) na kutaka wachagga waachie ngazi na wakae pembeni kwa angalau miaka mitano ili watu wa makabila mengine wapate nafasi. Hili linaweza kuwahusu wanyakyusa na wahaya vile vile. Kama hawatafanya kwa hiari tunaweza kufanya kwa nguvu hata kwa kutunga sheria maalum ya kuwalazimisha.
 
aliyetoa posti kama na yeye ni mchaga, naiona kama kejeli
Mimi pia ninahisi hivyo.
By the way, hebu tufanye tu kama maigizo, hiyo siku ikitokea itakuwa kichekesho sana. tunawezakuta maCEO wanachukuliwa watu kwa kupima uwezo wa kusoma na kuandika tu basi.Intermarriage zinazohusisha wachaga ni nyingi sana haswa kwa viongozi. Surely kama ikatokea hivyo naamini kuna baadhi ya idara zita collapse, maana kabila si kigezo cha watu kupewa hizo nyadhifa.
 
Mimi pia ninahisi hivyo.
By the way, hebu tufanye tu kama maigizo, hiyo siku ikitokea itakuwa kichekesho sana. tunawezakuta maCEO wanachukuliwa watu kwa kupima uwezo wa kusoma na kuandika tu basi.Intermarriage zinazohusisha wachaga ni nyingi sana haswa kwa viongozi. Surely kama ikatokea hivyo naamini kuna baadhi ya idara zita collapse, maana kabila si kigezo cha watu kupewa hizo nyadhifa.
usiposoma kwa makini hutamuelewa MMM... either ameaddress ukabila au yeye ni mkabila but pia yawezekana yeye ni third part tu

Ingawa most likely kuna element yenye ukweli kwa namna moja au nyingine na yaweza kuwa pia kwa wahaya, wanyakyusa, wasukuma nk
 
Mwanakijiji na tungo tata, ni lazima uwe mzima kwenye fasihi ndio utamuelewa vizuri huyu mwandishi.
 
Very amazing thread!!! Lakini cha ajabu zaidi ni kwamba MODs wengi humu wameunga mkono!!!! Mmmmhhhhh huu mwendo sio kabisa!!! Anyway tuyaache hayo, tuje kwenye hoja..In my view, it's very asinine to believe in that!!!

Nadhani inabidi kina Mangi Mareale warejee harakati zao za kuomba uhuru wa Wachagga maana washaanza kunyanyapaliwa ndani ya nchi yao... Naogopa yanaweza kutokea yale waliyofanyiwa Wayahudi kule Ujerumani ya zama za Hitler. Ni kweli kwamba kuna hisia mbaya sana dhidi ya Wachagga sasa hivi tofauti na zamani kama MK anavyosema. Hii 'PREJUDICE AGAINST CHAGGA' ifanyiwe kazi haraka laa sivyo kunaweza kukatokea 'CHAGGA GENOCIDE' kama ile ya Bosnia.

Binafsi kuna vitu vinanishangaza sana kuhusu dhana hii ya UCHAGGA. Kuna wakati mwingine unaenda kufanya job interview hata kama unatumia surname ya kisukuma ( na pengine ndio kabila lako) bado unajengewa hisia kuwa wewe ni mchagga eti kwasababu una muonekano wa sura za watu wa kaskazini!!!!

Kuna makabila ambayo watu wake wana sura zenye muonekano wa Kichagga. Mfano ni Wapare, Wanyaturu, Wanyiramba, Wameru na baadhi ya watu wa makabila ya mkoa wa Tanga (kama Wasambaa). Wasiwasi wangu ni kwamba any Prejudice against Chagga itadhuru watu hao pia.

Lakini swali kubwa la kujiuliza ni Je kwanini chuki hii imeshika kasi sasa???
 
Haki mwanajiji umefisika kimawazo na sio siri tena mwenzangu heshima yangu kwako imefikia kikomo kutokana na hizi pumba ulizo wakilisha hapo. Na muomba mungu akusamehe bure.
 
Siamini unaweza kuandika thread kama hii yenye mtazamo potovu. Kwa bahati kwangu mimi nimekuelewa kuwa una "unfounded bitterness". Mungu alichokujalia usikitapanye ukawapa nguruwe au kunguru. Peleka watoto wako shule washindane na wachaga na wengine kwenye nafasi unazozitamani.
 
nilikuwa na imani kubwa sana kwako mkuu M.M.M
sasa naanza kuipoteza.Tukumbuke kuna baadhi ya wanaforum na wale guest wanatutegemea sana kwa maoni na ushauri wetu kwa matatizo tunayopambana nayo kama taifa.And when you come will such post mzee....! naishiwa maneno ya kusema zaidi ya kusisitiza kuwa KILA MMOJA WETU AELEWE NAFASI YAKE KATIKA KULIJENGA NA KULIBOMOA TAIFA HILI.Kama huna cha kupost mzee......... siku nyingine uwe msomaji tu.
Thanks.
 
A MODEST PROPOSAL

Na. M. M. Mwanakijiji

Kuna vumbi la chuki, fitina, wivu, kisasi, na hisia za kibaguzi dhidi ya jamii ya Wachagga nchini. Kuna kila dalili kuwa jamii ya Wachagga nchini siyo tu inaanza kutengwa lakini uwepo wake katika nafasi mbalimbali za uongozi inazua hoja ya ukabila kwa haraka zaidi yawezekana kuliko kabila jingine lolote nchini. Katika Tanzania yetu, wachagga wameanza kunyoshewa kidole siyo kwa siri tena bali kwa wazi kabisa tena na watu ambao wakati mwingine hawapati hata kigugumizi.

Ubaguzi huo msingi wake mkubwa ni idadi ya wachagga katika nafasi mbalimbali za uongozi na hasa kuhusiana na elimu yao. Kuanzia mara tu baada ya uhuru jamii ya wachagga mojawapo ya jamii ambayo watu wake wengi wamesoma sana na kufanikiwa kielimu na kiuchumi imekuwa ikinyoshewa kidole cha kupendelewa.

Mtu yeyote ambaye anaweza akafanya uchambuzi yakinifu hatoshangaa kukuta wataalamu wa kichagga katika nafasi mbalimbali za uongozi au taaluma nchini. Kwenye vyuo vikuu, kwenye idara za serikali na hata kwenye taasisi binafsi kumejaa watu wenye asili ya mkoa wa Kilimanjaro na hususan watu wa jamii ya Kichagga.

Endapo itatangazwa nafasi yoyote ya kitaalamu usishangazwe ukiona kuwa waombaji wengi wana majina ya "Kichagga".

Ni kwa sababu hiyo basi kuna kila dalili kuwa kutokana na wingi wao katika nafasi muhimu na vyeo mbalimbali (hata ndani ya Jeshi la Polisi) Wachagga siyo tu ni wengi lakini wanaonekana kufanikiwa zaidi. Hili ni tishio kwa baadhi ya watu. Ni tishio kwa watu ambao hawako tayari kuangalia jitihada za watu katika kufanikiwa kwao na matokeo yake kushutumu ukabila kila idadi ya Wachagga kwenye kitengo fulani inazidi mmoja.

Ushauri wangu ni kuwa, kwa vile Wachagga wameshasoma sana na kuendelea katika biashara karibu mikoa mingi nchini. Na kwa vile wanaendelea kufanikiwa pia katika nafasi mbalimbali za uongozi nchini, basi itakuwa vizuri kama watajitolea kuachilia nafasi hizo ili kuwapa nafasi watu wa makabila mengine.

Kwa vile ni wao wanaonekana kulalamikiwa kutokana na mambo ya kifisadi aidha kwa moja kwa moja au kwa kuashiria basi ni vizuri wawape watu wengine nafasi hizo hata kama watu hao hawajasoma sana. Hii yote itakuwa ni katika kudumisha mshikamano, umoja na udugu wa Taifa letu.

Endapo Wachagga wataachilia nafasi mbalimbali kama UCEO, Ukurugenzi, Ukuu wa Idara n.k watasababisha watu wawapende na kuwakubali kuwa ni wazalendo wa kweli. Sitoshangaa kuwa ndugu zetu wa Jamii ya Kichagga wakikaa pembeni, basi ufisadi utakoma serikalini, idara zitaongozwa na watu wazuri, na mara moja na daima Tanzania itaanza kukua katika uongozi.

Kwa kupendekeza nashauri wabunge wote ambao ni Wachagga au wana asili ya mkoa wa Kilimanjaro kuachia ngazi mara moja ili watu wa makabila mengine wapewe nafasi hizo. Siyo wao tu bali pia wabunge ambao wameoa au kuolewa uchagani vile vile wafuate nyazo hizo.

Wakishamaliza hao, wakuu wote wa idara za serikali ambao wana asili ya mkoa wa Kilimanjaro na hasa wa jamii ya kichagga (wamarangu, wamachame, wa Rombo, na wa Kibosho) na wao waamue kuachilia nafasi hizo kwa ndugu zao Wamakua, Wamwera, Wa Ndali, Wadigo n.k Katika hili Wapare hawahusishwi.

Tukishamaliza wakuu hao wa idara za serikali ningependekeza madaktari wote wenye kumiliki hospitali binafsi ambao ni wachagga au wameoa/kuolewa uchagani na wenyewe waamue kuingia ubia na watu wa makabila mengine kama wangengereko, wambuu, na wanjiro ili hayo makabila madogo na wenyewe wapate nafasi ya kujifunza fani hizi muhimu.

Zaidi ya yote, majaji na mahakimu wote ambao wana asili ya Uchaggani na wenyewe waamue kujitoa katika nafasi hizo kwani wingi wao pia unaonekana sana na hivyo kuwa kikwako kwa watu wa makabila mengine kufanikiwa zaidi katika nyanja ya sheria. Kwanza kabisa wale majaji wa Kichagga wa mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu wawe wa kwanza kuweka manyanga chini.

Katika kufanya hivyo jamii ya Watanzania ambao inaona ukabila wa wachagga katika sehemu nyingi itaridhika kwani kwa mara ya kwanza tutakuwa tumeshughulikia chanzo cha matatizo yetu mengi
MMKJ
Mimi si Mchaga.
Lakini kwa hakika mawazo kama haya ni hatari kwako,kwa watanzania wengi na hasa wachaga unaowabagua
Matatizo ya kijami(Social inequality is every where in this world)Na kushauri utafute Sociologist akusafishe mawazo hayo.
Nawapa moyo wote wanaopiga vita hatred kama hii.
 
Mwanakijiji vipi?

Mwanahalisi, Raia mwema hamuoni madudu PPF?

Mbona kimya? Au ndio semina za wahariri zimewanyamazisha, mara Bagamoyo, mara Zanzibar, Arusha na... na...


Mwanakijiji

hebu kachungulie ppf

1. Idara ya fedha, mkurugenzi ni mchaga, amejaza wachaga wa kutoka wilaya yake. Wasio wachaga washida na kuondoshwa, anawatukana kama watoto wadogo, mkurugenzi mkuu anaangalia tu watanzania wanatukanwa kama watumwa

2. Mkurugenzi mkuu sio mchaga ila kalelewa mchaga ambaye ni mke wa mjomba wake. Yeye anaajiri watu wa mtwara hasa kwenye nafasi nyeti.

3. Ppf pia ichunguzwe hasa ajira zinazoendelea kuanzia 2007, wanawake wana pata shida na wakware hawa wakiongozwa na mkurugenzi mkuu. Usalama wa taifa wamchunguze anavyotumia u dg kupata wanawake wa kujifurahiha.

Ppf kunatisha
 
Nonsense. Stupid topic. Erase those hateful idea of yours frm inside u o,u wl hate Chagga' tu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom